Mwamuzi wa Tanzania
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 15,486
- 45,256
Ila kweli ni ushenzi.BOT fungieni hawa watu hakuna manufaa yoyote kwa mtanzania kwa sababu madhara ni makubwa kuliko faida.Sisi waathitika tunashauri muwafungie hii biashara.Sisi watanzania wenye nchi tunasema fungieni hii biashara ambayo inafanywa na wachina pamoja na wakenya wakishirikiana na watanzania wachache.Tumeona madhara yake ikiwemo kuwa na madeni lukuki hivo inabidi uendelee kukopa kwenye app zao mbalimbali ili ukamilishe madeni ya APP zingine wakati huo riba ni kubwa sana na siku ni chache (5-6)hivo unabaki kuwa mtumwa wa madeni ambayo hayalipiki na hakuna faida unayopata zaidi ya kugombana na ndugu zako, marafiki,wafanyakazi wenzio kwa sababu ili uweze ku maintain pressure za hawa wachina na wakenya wa APP za mikopo inakubidi ukope na kwa watu wako wa karibu hivo husababisha ugomvi na chuki miongoni mwa jamii wakati huo huo aliekopa akiendelea kuwa na madeni kwa sababu inafikia wakati hayo madeni hayalipik tena.kUMBUKA kuwa utapigiwa simu kuanzai saa kumi na moja alfajir hadi usiku wa manake ukipokea vitisho na maneno ya kejeli muda wote unakuwa huna amani badala ya mkopo inakuwa SHARI sasa.Hebu fikiria saa saba usiku mkeo anapigiwa simu eti anaambiwa tunajua uko na jamaa hapo mwambie alipe ! Saa saba usiku wakati umelala na mkeo ! Hii ni zaidi ya ushenzi !
Nawashauri BOT wafanye reseach katika jamii juu ya suala hili ili waujue ukweli na research yenyewe iwe direct one to one na wale walioathirika watapata A to Z ya tatizo hili kubwa.
Narudia tena BOT funga hii biashara ya mikopo ya APP mitanadaoni.
CCM waelekezeni BOT wafunge hii biashara tafadhali.
Na pia wakati BOT wakivuta miguu kufunga biashara hii TRA fuatilieni hizi APP , pesa nyingi sana mapato ya serikali zinaenda kwa wajanja wachache bila kulipa kodi wakati hawana ofisi ya kuwa trace wala kuwa hold responsible.
Huu ni UHUJUMU UCHUMI
Narudia tena BOT na serikali ya sikivu ya CCM fungia hawa watu !
Hii mikopo imewahi kuninyoosha mda fulani.
Jamaa ni freemasons. Kujinasua kunahitaji maombi mazito