BWANA MUNGU amempa Mwanadamu akili kichwani, macho, masikio, mikono, na miguu. Tena akaijaza dunia na raslimali za kila aina.
Cha ajabu zaidi Mwanadamu huyo aliyepewa uwezo na raslimali bado anarudi kwa MUNGU na kumlilia shida.
Lakini, wapo Wanadamu waliolitambua hilo mapema, wakatumia uwezo waliopewa na MUNGU kuzibadili fursa zilizopo kuwa kipato.
Wale wavivu wa kufikiri, waoga na wasiotaka kujifunza wanaogelea kwenye dimbwi la ufukara na ndio hao wanajazana kwa manabii wa uongo wakitafuta "miujiza".