BullDoza Mwamposa Ana Powers za Mvuto wa Ajabu, Aleta Balaa Kubwa Kawe na Maeneo ya Jirani, Mkesha Wake, Kawe, Mikocheni, Mbezi Beach, Wote Tumekesha!

BullDoza Mwamposa Ana Powers za Mvuto wa Ajabu, Aleta Balaa Kubwa Kawe na Maeneo ya Jirani, Mkesha Wake, Kawe, Mikocheni, Mbezi Beach, Wote Tumekesha!

Na wewe ni tapeli unamhamasisha tapeli mwenzio, hiyo nyomi inaonesha watanzania umaskini ni mkubwa sana na watu wanatafuta mafanikio kwenye kukanyaga mafuta au kutafuta mafanikio kwa mtu..na nyie socialites badala mkemee watu wafanye kazi kama wachina nchi mwao, mmekaa mmekalisha matako yenu mnahamasisha tu..shenzi kabisa.
Rudia kumsoma utaelewa, usikaze fuvu litauma.
 
BWANA MUNGU amempa Mwanadamu akili kichwani, macho, masikio, mikono, na miguu. Tena akaijaza dunia na raslimali za kila aina.
Cha ajabu zaidi Mwanadamu huyo aliyepewa uwezo na raslimali bado anarudi kwa MUNGU na kumlilia shida.

Lakini, wapo Wanadamu waliolitambua hilo mapema, wakatumia uwezo waliopewa na MUNGU kuzibadili fursa zilizopo kuwa kipato.

Wale wavivu wa kufikiri, waoga na wasiotaka kujifunza wanaogelea kwenye dimbwi la ufukara na ndio hao wanajazana kwa manabii wa uongo wakitafuta "miujiza".
 
Wanabodi,

Huyu Pasta Bulldoser, Mwamposa.. sio mchezo...
inaendelea...

Paskali
Hapo sasa ndipo uone aina ya waumini wanaotaka mambo yawaendee kwa 'njia za mkato' kama wakati ule wa 'kikombe cha babu'. Ukiona watu wanamiminika kwenye maombi ya namna hii, ujue wana shida mbalimbali ambazo wanaona utatuzi wake ni kwa njia ya miujiza. Na Yesu alikuwa akiwaambia wanaomsikiliza wasiwe watu wa kutegemea miujiza, lakini kizazi chetu kimekuwa cha kutegemea miujiza. Maana yake ni nini? Maana yake ni kwamba tumeweka mafundisho ya Yesu pembeni, na kufuata mafundisho ya akina Mwamposa, ambayo ndiyo yamekuwa mbadala wa mafundisho ya Yesu. Kwenye mikutano kama hii watu hawaendi kukutana na Yesu, bali kukutana na akina Mwamposa. Hapo ndipo ninapotofautiana na hawa watu wanaojiita mitume na manabii. Zamani walikuwa wakichaguliwa na Mungu, siku hizi wanajichagua wenyewe maana wanaona wakisubiri wachaguliwe huenda wanaweza wasiwe.
 
mtapigwa sana huko, endeleeni kwenda kutafuta simulizi, Pale ukiwaambia waumini wafungue Bible wanaweza anza kutawanyika, hawataki kusikia kitu kinaitwa Bible wao wape hadithi za miujiza fake
Mimi nimeona miujiza ya Yesu live bila chenga maishani mwangu utaniambia nini,tunamwabudu aliye hai.Tunafurahi na kuwa na ujasiri kwakuwa tunapata haja za mioyo yetu tukiomba sawa na atakavyo yeye.
 
Hakika huu mji una watu wengi. Mi.nilisikia tu tangazo mtaani nikapuuzia tu. Nilichukulia tu kama matangazo mengine ya serikali za mtaa au promo. Watu kumbe walifurika? Hata kipindi kile uwanja wa Mkapa, sikuwahi kusikia tangazo ila baadae nasikia tu uwanja ulifurika. Haya bana
 
Hao mliojazana hapo karibu asilimia 90 ni watu mliokata tamaa ya maisha pamoja na watu mafukara. Hiyo asilimia 10 iliyobaki ni watu wanaojificha kwenye kivuli cha huyo jamaa ila nyuma ya pazia ni mashetani waliobobea. Wewe upo kundi lipi?
Kwa mantiki hio Watanzania wana matatizo mengi sana ambayo yamekosa utatuzi wa kiserikali na kukimbilia kwenye Imani, Nadhani pia viongozi wasishangae kujaza kwa Mwamposa bali watumie kusanyiko hilo kama evaluation ya kinachoendelea kwa ground.
 
Back
Top Bottom