Bunge liitishe kikao cha dharura kujadili kufungwa kwa ubalozi wa Denmark 2024

Kwa walinzi hawahawa wa amani yetu,walioshindwa kumkamata mshambuliaji wake,au walio mshambulia m.kiti pale Dom na hatimae kumbambikia?hawa wanaonyanyasa raia wanaokusanyika kujadili upatikanaji wa katiba na mikutano mingine halali ya kisiasa ina haramishwa na waliotakiwa kuwapa ulinzi.?Hawa ambao ni walinzi wa chama korokocho usiku na mchana,jua,mvua masika?Hawa wanaosimamia na kuwezesha wizi wa kula/uchafuzi/guzi?
 
Kumbe bado mabeberu yanatakiwa?
 
Nikitukana watu humu huwa naonekana kuwa ni mtu mbaya sana!Huu uzi ni kituko,unahitaji PhD ili kujua kuwa Tanzania haina bunge?!WTF!!!
 
Ni matokeo ya Tundu Lissu kuichafua nchi nje ya nchi, Bunge msipoteze muda kwa ujinga kama huu, waTZ tutaprevail tu, hawa wapinzani uchwara wanaoomba nchi yao ikose hela kwa manufaa yao ya kisiasa watashindwa tu, TZ will stand always

Mamlaka zinakobambikiza kesi zikadhudulumu watu haki, hujichafua zenyewe
 
Denmark wanasema wanataka kuhakikisha watu wao wako SAFE kwenye Dunia inayozidi kupoteza muelekeo wa kidemokrasia na HAKI za Binadamu.

Wameamua kufunga ubalozi wao Tanzania kutokana na mambo ya hovyo tunayoyashuhudia Tanzania sasa hivi kama vile uvunjaji mkubwa wa haki za binadamu, ukandamizaji wa demokrasia, kukosekana kwa utawala bora, kukosekana kwa utulivu na usalama,ugaidi(fake) na kadhalika.

Wa kulaumiwa katika hili ni hii serikali fake ya CCM ambayo haina kibali cha wananchi ambayo imefikia hadi hatua ya kutengeneza ugaidi fake ili tu kutengeneza uhalali wa kubakia madarakani kwa mabavu.
 
Watanzania janjajanja imezidi,democrasia ipo,huku uhuni, na uharamia unaratibiwa na wanaoiimba democrasia midomoni, uchaguzi unafanyika, kumbe janjajanja na uhuni unaoratibiwa na wenye maslahi yao binafsi kwa mgongo wa uzalendo uchwara. Nabado sehemu ya uratibu wa uovu ni misaada.
 
Probably, kuna sababu ya msingi ya ndani zaidi kuliko iliyozungumzwa.
Iko wazi tu, mipango yao imekamilika, walichokuwa wanakitafuta wameshakioata. Tanzania haina kazi tena kwao.
 
Iko wazi tu, mipango yao imekamilika, walichokuwa wanakitafuta wameshakioata. Tanzania haina kazi tena kwao.
Kikao cha dharura cha kuitishwa hivi sasa ni chakutafuta katiba mpya basi,mengine janjajanja kama kawaida ya mtanzania.
 
Sasa Denmark itaitwa Beberu.
 

Beberu ni mtu serious:

1. Kwamba alituonaje kwenye upigaji nyungu?
2. Kwamba hakusikia tukisema alikuwa na vita vya kiuchumi dhidi yetu?
3. Kwamba hakusikia tulikuwa nchi tajiri?
4. Kwamba hakusikia tukimtuhumu kupanga kutumaliza kwa chanjo?
5. Kwamba hakutusikia tukijishasha kuwa beberu alilenga kujipatia pesa toka kwetu kwenye janga hili?
6. Kwamba haoni ukiukwaji wa haki za binadamu unaoendelea?
7. Kwamba haoni wizi kwa mujibu CAG?
8. Kwamba haoni tusivyojitahidi hata kupambana na Corona hata leo?
9. Kwamba anaona tunashaurika?
10. Kwamba anaona tuna utu?
11. Nk

Huoni ndege wa kufanana huruka pamoja? Burundi ni mwenzetu KIMKAKATI.
 
Wadanish sio mabeberu ni washirika wa maendeleo kupitia shirika la DANiDA

Beberu ni nani basi maana kote kuna ma SIDA, JICA, KONICA, USAID, DFID, NORAD, SAREC, NUFFIC, DAAD nk?
 
Hiyo uturuki unayoizungumzia sasa ivi currency yao ipo hoi baada ya kuwekewa vikwazo na marekani.

Hapa tulipo tutaongea maneno mengi ya kupeana moyo.lakini ukweli utabaki pale pale kwamba wazungu wameushikilia uchumi wa dunia na wana uwezo wa kuyumbisha uchumi wa nchi yoyote wakiamua.
 
Ni matokeo ya Tundu Lissu kuichafua nchi nje ya nchi, Bunge msipoteze muda kwa ujinga kama huu, waTZ tutaprevail tu, hawa wapinzani uchwara wanaoomba nchi yao ikose hela kwa manufaa yao ya kisiasa watashindwa tu, TZ will stand always
Hebu na wewe weka hapa mchango wako kwa taifa ni upi ili tujue taifa litakacho pata mbadala wa madenishi.
 
Hili Bunge halina ubavu wa kuzungumzia suala hili. Inteligensia ya Denmark sio mchezo, ni high level, wameshaona kabisa muelekeo wa Nchi, kwahiyo hawataki yawapate ya kuwapata.

Wameona kabisa kuna kupoteza muelekeo kama Nchi na hawakutegemea hali kama hii kwa Tanzania. Hizi ni Nchi zinazojitambua sana.

Ni alert kwa Serikali yetu, watafuata wengi kufunga Balozi zao.p
 
Wewe Katambi karai tulia
 
Uamuzi wa Dernmark kufunga baadhi ya balozi zake duniani ni KUJITAFAKARI.....wameelezea bayana tu........

Wanafunga balozi zao ikiwemo ya ARGENTINA ,CHINA ,UHISPANIA na kwengineko....."issue" siyo Tanzania tu.......
 

Haya mambo yanahitaji kujadiliwa bungeni na si gengeni. Bahati nzuri ni kwamba, ninazidi kuthibitisha mtazamo wangu wa tangu zamani kwa watu wenye vichwa vyenye maumbo kama la kichwa cha yule. Usitegemee mjadala wa masuala ya maana, ufikie hitimisho la maana chini yake.
 
Tuache UPOTOSHAJI......

Ni hivi....

Bayana iliyoelezwa na WIZARA YAO YA MAMBO YA NJE inatokana na wao kutaka kutafakari baada ya WATALIBANI kuichukua tena nchi ya Afghanistan wiki chache tu zilizopita......

Ikumbukwe hawa DERNMARK walishawahi kuambiwa na msemaji wa Taliban aitwaye Zabihullah Mujahid kuwa kama hawatochagua(kura) chama/vyama vyenye sera ya kupeleka vikosi nchini Afghanistan basi HAWATOPATWA NA KITISHO CHOCHOTE....

Itoshe kusema kuwa Dernmark wameamua KUJITAFAKARI na sera zao za nje baada ya muda mrefu kuwekeza katika DEMOKRASIA na mengineyo na si "issue" ya kutengenezwa visingizio feki kwa Tanzania....

#SiempreJMT
 
Si mmesema ni mabeberu..!?
 
Bunge la ndugai au bunge lipi hilo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…