Eti wakuu, kwa Karne ya sasa kuna umuhimu gani wa kuendelea kuwa na Primary Schools kama Bunge pale kati kati kabisa ya Mji?? Lengo ni nini?? Tena shule ya serikali, shule zinazofahamika kwa kuwa na wanafunzi wachafu wasio na maadili hakuna mfano.
Eneo potential la kuweka investments za maana, wewe unaweka shule ya msingi? Hata kama ilijengwa zamani, Je, bado kuna uhalali wa kuendelea kuwepo pale?
Ni mtoto yupi anayesoma primary ya Bunge ni mkazi wa eneo lile lililojaa ofisi za serikali?
Uwepo wa shule kama Bunge huleta msuguano tu wa kimaslahi kwa maana ikifika December, kila mzazi anayefanya kazi Posta, mwenye IST anataka mwanae akasome Bunge. What for.
Hata kama ni shule, basi mpeni muwekezaji binafsi atakayeweza kumaintain mazingira pamoja na usafi wa wanafunzi kama zilivyo shule zingine za private za English Medium lakini sio kuweka shule uchafu katika eneo potential kama Posta Mpya (A few kilometers from the state house)
SHULE YA BUNGE CITY CENTER NI UCHAFU MWINGINE UNAOFUMBIWA MACHO NA VIGOGO..