Bwana Tundu Lissu, Hoja ya Chato na Maendeleo ya sasa inajibika Kimantiki

Mkuu,kuna binadamu walitakiwa wawe "mifugo" badala ya wanyama au binadamu. Huyu ni kielelezo tosha.
 
Ninajua una uwezo mdogo wa kuelewa mambo, nimesema kujenga uwanja wa kiwango hicho. Nimerudia zaidi ya mara kuwa uwanja wa kiwango hicho haukupaswa kujengewa umbali huo na uwanja wa Mwanza. Inaonekana umekuwa brainwashed kiasi huangalii mambo kwa mantiki tena, bali unalazimisha utetezi wa kijuha.
 
We mutungi, waliosema ni wengi,mbona umeelekeza majibu yako kwa lisu tu?
Hata huku mitaani wanasema,ulitakiwa kusema ngoja nitow ufafanuzi kwa watanzania tu.lisu Yuko huko wanakoishi watu.
 
Ahaaaa! Mwanza ni international airport,unataka iwe na backup ya airstrip?

Huu uwanja ungejengwa Kisarawe usingelalamika. Acha siasa za kizandiki
 
Yule aliyetoka kusini kwao watu walimsema
Oh mbona kuko ovyo
Tatizo sisi wanadamu hatueleweki kabisa

Ova
Mkubali sasa kuwa kuna upendeleo unafanyika Chato,baada ya hapo tutajadili hayo mengine!
 
Hebu,
Toa vigezo vya kutojenga uwanja wa ndege Geita na badala yake kwenda kujenga Chato umbali wa kilometa takribani 90 ambako kuja population ya watu wasiozidi 130,000/- ilhali geita kuna population inayozidi 300,000 sambamba na wafanyabiasha wengi na wakubwa kuliko chato???

Tueleze sababu zilizopelekea kujenga hospitali ya rufaa chato wakati kuna nyingine ipo hatua za mwisho mjini Geita lakini mji kama tabora au kigoma hauna hospitali zenye sifa hata ya angalau geita??

kinachofanyika chato ni aibu kwa taifa.
 
Ahaaaa! Mwanza ni international airport,unataka iwe na backup ya airstrip?

Huu uwanja ungejengwa Kisarawe usingelalamika. Acha siasa za kizandiki

Pembeni ya Kilimanjaro airport kuna uwanja wa kiwango cha huo wa Chato kama Backup? Kumbuka Kilimanjaro ni mkubwa zaidi ya huo wa Mwanza. Hapa unajichoresha tu boss kwa Utetezi huu.
 
Pembeni ya Kilimanjaro airport kuna uwanja wa kiwango cha huo wa Chato kama Backup? Kumbuka Kilimanjaro ni mkubwa zaidi ya huo wa Mwanza. Hapa unajichoresha tu boss kwa Utetezi huu.
Pembeni ya kilimanjaro unamaanisha nini?
 
Kuna hoja ya msingi hujaijibu,umekurupuka tu,
Swali liliulizwa,Kwanza hakuna ubaya anapotoka Raisi kuwa na vyote hivyo,swali je ni vipaumbele vya nchi?vipo kwenye irani?vipo kwenye mipango?au ni vipaumbele vya Raisi?Wilaya nzima Haina hata Timu ya mpira,unaenda kujenga uwanja wa mabilioni!?
Wakati inajengwa Mloganzira hospital,Uwanja wa Mkapa,na terminal three inapanuliwa hakuna aliyepiga kelele,hata mkazi wa Masasi,au Kyelwa,au N'gara,au masumbwe,u kalumwa,akisikia haimpi shida kuona kwamba Dar inapendelewa,
Sasa wewe unajenga uwanja wa Ndege Chato kwa shughuri gani za kiuchumi zilizopo ambazo zitaleta faida?
Tundu Lisu,ametoa mfano wa uwanja wa Ndege wa mpanda,ulijengwa wakati Pinda ni PM,Tena kwa mbwembwe,sasa hv,unaota nyasi,kupata hata Ndege moja kwa wiki,ni hanasa,haya ndio matumizi ya hovyo,wewe thibitisha airport ya Chato inaingiza pesa ngapi ukilinganisha na KIA.
Maiti ziliokotwa Coco Beach zikiwa kwenye viroba,azory gwanda,ben saa nane,wamepotea Kama upepo,.
Lisu alikula shaba 18!mchana kweupeee,Tena kwenye viunga vya bunge.harafu unasema jiwe hafanani na Mobutu!!
Mtoto wa Dada ndio boss hazina,Shemeji akapewa tenda ya kujenga uwanja bila kufata taratibu,kwa taarifa yako mwaka jana kwenye uchaguzi mtandao ulizimwa,Ili jiwe afanye yake,
 
Mkubali sasa kuwa kuna upendeleo unafanyika Chato,baada ya hapo tutajadili hayo mengine!
Hiyo ni nature ya mwadamu mkuu hata wewe ungekuwa kwenye nafasi kubwa ungependelea kwenu...lakini kama hauna ubinafsi na unapotoka!

Ova
 
Wangekuwa wabinafsi wangejenga kwao!Sasa siasa za nchi hii zinachukua sura mpya,tutaanza kuchaguana kikabila ili tu maendeleo yawahi maeneo ya ukanda wa kabila la Rais!Huku ndiko mnataka tufike?
Ukiona hivyo hawakupathamini kwao

Ova
 
Rais amehamia Chato kusimamia miradi ya kwao, unaposema itawanufaisha watanzania wote ni kuwafanya watanzania ni mabwege, ni vipi daraja lijengwe Chato mtu wa Katavi anufaike! Vivuko vinavyojengwa Chato havijawahi kuwanufaisha watu wa Kigoma, acha siasa za kitoto. Dodoma inahitaji haraka uwanja wa ndege na haitafaidika kwa uwanja wa Chato. Kama haki ingekuwa kama usemavyo basi hakuna sababu ya kujenga miradi sehemu tofautitofauti ingekuwa rahisi na nafuu miradi yote kujengwa Dar na nchi mzima kufaidika! Huu ni ujinga. Tetea mambo ya msingi usitetee huku wengine wamekuwa wakiomba zahanati na maji tangu Uhuru hawapati kwa sababu Rais hajatoka kwao.
 
Chukua like ya moyo wangu [emoji120]

Odhis *
 
Hiyo ni nature ya mwadamu mkuu hata wewe ungekuwa kwenye nafasi kubwa ungependelea kwenu...lakini kama hauna ubinafsi na unapotoka!

Ova
Ok,sasa tunaongea lugha moja!Chato inapendelewa kwasababu Rais anatoka huko!
Ova!
 
Pembeni ya Kilimanjaro airport kuna uwanja wa kiwango cha huo wa Chato kama Backup? Kumbuka Kilimanjaro ni mkubwa zaidi ya huo wa Mwanza. Hapa unajichoresha tu boss kwa Utetezi huu.
Arusha na Moshi kuna viwanja vya ndege ambavyo ni vidogo, viwanja hivi vilijengwa kwenye kila mji wakati wa ukoloni na KIA ukajengwa kushika nafasi ya hivyo viwili, usipotoshe.
 
Ukitoa ushabiki kichwani ukauweka pembeni ukabaki na akili Yako timamu utagundua Yanayofanyika huko kyato ni mbegu ambayo matunda yake yatakuwa ili uwe kiongozi wa eneo fulani Basi ni lazima pia uwe mzawa wa eneo hilo.

Watu wengi wataamini ili nipate maendeleo lazima nimchague wa kwetu. Naunga mkono hoja za Lisu, haya Yanayofanyika ni vipaumbele binafsi vilivyovikwa vazi la maendeleo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…