Bwana Tundu Lissu, Hoja ya Chato na Maendeleo ya sasa inajibika Kimantiki

Bwana Tundu Lissu, Hoja ya Chato na Maendeleo ya sasa inajibika Kimantiki

Jaduong, maswali gani ya kitoto? Ahaaaa
Kuna mambo ya kimkakati yalitakiwa kufanyika makao makuu ya mkoa , na yasingeleta manung'uniko. Lakini haya ya kuyakimbiza kijijini kwetu chato lazima pafananishwe na Gbadolite . Kwani unadhani Mobutu kuyapeleka maendeleo Gbadolite alikuwa na nia mbaya ?!.

Natamani na rorya wangetujali namna hiyo. Ukizingatia kila uchaguzi tunawapa wabunge.

Odhis *
 
We unaweza kujua kama JPM asingekuwa rais huu uwanja usingejengwa? Mbona Chafo ina barabara ya lami kwenda Bk ambayo inathamani kubwa kuliko huu uwanja? Chochote kinaweza kutokea.

Barabara thamani yake inapimwa kwa urefu wake, unaweza kufananisha na uwanja wa ndege? Hii inaonyesha umekosa la kutetea hayo matumizi mabaya ya madaraka, ndio maana unatoa mifano isiyobeba utetezi wako.
 
Na hata hiyo barabara, nayo ilileta manunguniko kwa nini ilichepushwa bila kupita makao makuu ya wilaya wakati huo (biharamulo).

Kumbuka ni nani alihusika na mabarabara wakati huo.

Uwanja wa ndege Chato ni runway ambayo inaweza kubeba ndege kubwa. Na hapo ndio mnachanganya mambo mpaka mnajidharirisha. Tofauti ya runway ya ndege na barabara ni kidogo sana.
 
Na hata hiyo barabara, nayo ilileta manunguniko kwa nini ilichepushwa bila kupita makao makuu ya wilaya wakati huo (biharamulo).

Kumbuka ni nani alihusika na mabarabara wakati huo.

Odhis *
Jaduong nacheka tu, hivi milima ya Geita mjini ilivyo wapi tungeweka kiwanja cha ndege? Barabara kupita Chato ili kupunguza umbali wa kuzungukia Biharamulo ni kosa?
 
Jaduong nacheka tu, hivi milima ya Geita mjini ilivyo wapi tungeweka kiwanja cha ndege? Barabara kupita Chato ili kupunguza umbali wa kuzungukia Biharamulo ni kosa?
Haikuleta maneno maneno ?

Nilishakujibu swali uwanja wa ndege ulitakiwa kuwa wapi. Miezi kama mitano nyuma, sijui ilikuwa uzi wa nani !!. Nyuma ya milima hiyo ya Geita eneo ni kubwa na ya kumwaga .

Jaduong unajua, ndege kubwa inavyoruka na kutua,unadhani Airbus inaweza kutua kwenye milima ya Geita kama unaenda Nzera? Acha ushabiki wa kisiasa.
 
chato ni sehemu ya Tanzania hamna shida kukiwa na miradi ya maendeleo,mbona hamlalamiki kuhusu maendeleo yanayofanyikaa Da es saalamu,dodoma fungeni midomo yenu
 
Mtu asipopaendeleza kwao shida
Akipaendeleza napo shida[emoji23][emoji23][emoji23]
Ubinadam kazi sana

Ova
Rais wa nchi kwao ni TANZANIA sio Chato.

Alichaguliwa na watanzania
Uchaguzi ulifanyika kwa kodi za watanzania
Akaapa kuilinda katiba ya JM Tanzania
Kuwatumikia Watanzania sio wanachato

Anachokifanya Rais kwasasa analigawa Taifa, anaweka rehani upendo, umoja na mshikamano. Tunu muhimu walizopigania waasisi wa Taifa hili kwa jasho na damu.
Anaweka rekodi mbaya kuwahi kutokea kama Rais, kibaya zaidi hili litatumika kama Precedence (marejeo) kwa Marais watakaofuata
Tusipokemea sasa hatutaweza kukemea baadae.

Yeyote mwenye akili timamu ni lazima akemee uovu huu.
 
Kijiji kimoja kijulikanacho kama Chato ndani ya miaka mitano kimefanyiwa yafuatayo tofauti na kijiji kingine chochote Tanzania:-

1. International airport imejengwa
2. Taa za kuongozea magari barabarani zimewekwa.
3. Chuo cha utumishi wa umma kinajengwa.
4. Uwanja wa kimataifa wa michezo unajengwa (kijijini!)
5. Mabenki yamejengwa
6. Hospitali ya kimataifa ya rufaa inajengwa.
7. Mbuga ya kimataifa ya wanyamapori imeanzishwa.
8. Dhifa za kitaifa za kuwapokea wakuu wa nchi na serikali zinafanyika.
9. Viongozi wakuu wa nchi wanaapishwa.

Ni katika kijiji kipi kingine Tanzania japo robo ya hayo yamewahi kufanyika? Halafu huoni tatizo? Hata kama ni kunywa maji ya kijani sio kwa upofu huo!
Bandari ya nyamirembe?
Daraja la Busisi?
Bohari ya dawa?
Kijiji cha Nyantimba kinachosadikika kuwa na dhahabu GN ya Biharamulo?

Asiyependa kwao ni mtumwa!!!
 
Kwahiyo huo wa Geita umejengwa ili kushika nafasi ya huo wa Mwanza kwakuwa ni mdogo?
Usiniulize mimi muulize anayepiga kambi kujenga Chato kwanza, Morogoro nasikia mizimu ya mababu ilikataza kujenga uwanja wa ndege. Ni vigumu kuelewa madhumuni ya serikali kupigana kambi Chato na kuitelekeza Dodoma! Ghatama nchi inayoingia kuwalipa mania ya watumishi wa umma ambao wamekwenda Chato kupokea wageni na magwaride hazina tija kwa taifa.
Wakati wa East African Airways Kenya ililalamika ndege kwenda kila mkoa kasoro Morogoro bila abiria wa kushuka wala kupanda zaidi labda kuacha barua mbilitatu!
 
chato ni sehemu ya Tanzania hamna shida kukiwa na miradi ya maendeleo,mbona hamlalamiki kuhusu maendeleo yanayofanyikaa Da es saalamu,dodoma fungeni midomo yenu
Dodoma na Dar ni miji ya kiserikali IMO ndani ya sheria za nchi kiutawala, usidhani serikali na mashirika ya umma yapo kwenye miji hiyo kimagumashi.
 
Kwa kifupi ni kwamba MAGUFULI anajenga miradi nchi nzima.
Na huyo LISSU analijua sana hilo.

Ndio maana kwenye uchaguzi ulioisha alikuwa akisema wao chadema wanataka maendeleo ya watu na sio vitu.

Anajitoa akili kuandika makala ndefu isiyo na uhalisia ili mradi tu mabwana zake (mabeberu)wasimuoe kama amebweteka na kula bure.
Kumbukeni kwamba ile story ya ICC imegonga mwamba. Ni baada ya kutokidhi vigezo vya hadhi ya ukubwa wa mahakama hiyo.(hili sisemi mimi bali toka kinywa chake LISSU ambaye amekaririwa na vyombo vya habari duniani).
Kwa sasa Amsterdam amekwisha tia kibunda chake mfukoni na anaendelea na maisha yake.

Viva #JPM [emoji1241]
 
Jibu hoja, acha mipasho
 
Kwa kuwa Mwanza kuna uwanja ndio Geita usijengwe uwanja? Unajua umbali wa Chato to Mwanza

Mimi sitetei, sioni sababu za msingi kunishawishi kupinga Chato kuwa na uwanja.
Changu wa madoa acha utoto. Huoni sababu za msingi. Unaona zipi? Unajua umbali? Dar mpaka terminal 3 wakati Kibaha au Kisarawe hakuna uwanja! Pengine huo uwanja ungejengwa Geita ingeeleweka. Hata ungetupwa Katoro bado shida ingekuwepo. Tunazungumzia uwanja wa kimataifa! Chato hata wa wilaya si muafaka. Kete ya Katoro hiyo. Tena acha ufala Geita si Chato. Hovyo!
 
Salaam Wana JF.

Nimesoma na kuona andiko la Bwana Tundu AM Lissu kutoka Ubelgiji akijenga hoja juu ya maendeleo ya vitu na watu ndani ya eneo la Chato anapotoka rais wa sasa Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Sijaona mantiki ya Lissu kupotosha umma wa Watanzania dhidi ya maendeleo ya sasa kwa Chato. Aidha, kabla ya kujenga hoja zangu dhidi ya hoja za Lissu, nitumie jukwaa hili kukanusha upotoshaji wa kumfananisha Rais Magufuli na Madikteta wa Kiafrika akina Mobutu Sese Seko, Felix Houphouet-Boigny, Hastings Kamuzu Banda na wengineo, Kwa hoja hii Lissu umepotosha umma na awatake radhi Watanzania na Rais Mwenyewe, kamwe uwezi kuzifananisha sifa za Mobutu na JPM labda kama hujui uovu na ukatili wa Mobutu Sese Seko.

Aidha Bwana Lissu unaporejea Kitabu cha Peter Kenyon "Dictatorland, The Men Who Stole Africa" Anachokiongelea Mwandishi Peter kwa viongozi wa Kiafrika walionajisi nchi zao hakina uhalisia na kinachofanywa na Rais Magufuli kwa sasa ndani ya eneo la Chato, Mantiki ya Peter Kenyon ni kuwamulika viongozi waliotawala Afrika na kujitajilisha wao wenyewe kimaendeleo dhidi ya Umma yaani wenye nchi, Rais Magufuli anatajilisha Umma kimaendeleo badala yake binafsi ndipo hoja iliposimama hapa.

Bwana Lissu kama unavyojua ni ngumu sana kuzuia watu kusema lakini linapokuja suala la upotoshaji ni sharti tujenge hoja kuepusha kikombe hiki kutamalaki, Bwana Lissu kinachofanywa na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli katika Mkoa wa Geita wilayani Chato ni Jambo la kawaida kwa mantiki kuwa kusudio la Maendeleo hayo ni kwa manufaa ya Watanzania wote bila kujali eneo unalotoka, Umerejea awamu zilizopita ukiwataja viongozi wa awamu hizo nne kuwa hawakufanya kinachofanywa kwa sasa, Bwana Lissu nikujulishe kuwa kila nyakati na mambo yake.

Wakati wa Mwl. Nyerere alifanya kulingana na uhitaji na mipango ya wakati ule lakini pia alinyoshewa kidole na wakosoaji wake wa masuala ya maendeleo, Hivyo hivyo kwa Mwinyi, Mkapa na Kikwete kwahiyo lawama za namna hii hazikuanza leo na kamwe huwezi kuzimaliza lakini zinapopotosha zinajibiwa kimantiki, hata hivyo kila utawala utofautiana kiutawala, tunachokiona sasa sio kile tutakachokiona awamu ijayo ya sita.

Tunge jenga hoja za kumushambulia Rais Magufuli endapo tu kama angekuwa anafanya maendeleo ya namna hii nje ya Tanzania, hata mimi ningeunga mkono hoja kwa kitendo hicho lakini kinachofanywa ni ndani ya ardhi ya Tanzania, Aidha ninge hoji na kukosoa endapo tu Rais Magufuli angekuwa anafanya kwa maslahi yake binafsi na familia yake, lakini kinachofanywa ni kwa maslahi ya umma, Je nongwa inatoka wapi? Au ni husuda tu wa kisiasa kwa sababu ya itikadi za vyama vyetu?

Bwanba Lissu unadriki kulinganisha Mobutu Sese Seko ,Felix Houphouet-Boigny na Rais Magufuli, Je unajua viongozi hawa walitumia kodi za walala hoi kufanya starehe na anasa nyingine za kufuru hata zilizokuwa kinyume na amri kumi za Mungu kwa kujenga majumba ya kifahari kwa familia zao na kuwekeza mapesa mengi kwenye makampuni yaliyo je ya mataifa yao, Kinachofanywa Chato ni uwekezaji wa anasa au kwa mustakabari wa maendeleo ya watu kwa kizazi cha leo na hapo badae? Je baada ya rais muda wake yote yaliyofanyika ndani ya geita yatakuwa mali ya serikali au familia ya Magufuli?

Je, hoja ya kupinga maendeleo ya Chato inatoka wapi na ina mantiki ipi? Hata hivyo bwana Lissu unapo ongelea kisa cha Rais wa zamani wa Afrika Kusini bwana Zuma aligeuza kijiji chake cha Nkandla kuwa kama ambavyo Magufuli anaigeuza Chato Si kweli, Tuhuma za Zuma ni kujenga Jumba la Kifahari na baadhi ya mambo mengine ya anasa kwa kutumia kodi ya Wana Afrika Kusini badala ya kutumia pesa yake binafsi, na ndo maana mahakama iliamuru arudishe hela na akarudisha, Je ufanano wa Zuma na Magufuli upo wapi hapa bwana Lissu?

Nihitimishe andiko hili kwa kusema kinachoendelea mitandaoni kuhoji na kushambulia kile kinachofanyika Mkoani Geita wilayani chato kama kitu kisichokubalika kwa umma ni upotoshaji ambao sharti Watanzania tuupuuze na tuungane kwa pamoja kuendelea kuijenga nchi yetu katika dhana ya maendeleo na watu wake, Maendeleo hayana ukanda ilimradi tu kinachofanyika kiwe ndani ya ardhi ya Tanzania.

Deogratias Mutungi
Utopolo fc...
 
Unatumia muda mwingi kutetea ujinga. Sijui hata wazazi wako au wanao wakijua kuwa baba anatetea pumba za Magu watakuelewaje. Too low for a scholar
Bado siamini kwamba CCM hii nayoijua imekosa watu wa kujenga hoja kiasi hiki.... hii ni takataka!!
 
Back
Top Bottom