Geti litakalofungwa(jaribu kuzoom na ulinganishe ukubwa wa lori na watu wanaoonekana kwa mbali)
Pamoja na ukweli kuwa sikuwa mshabiki sana wa JPM, lakini kwa bwawa la Nyerere alipiga bingo.
Kwamba Mama Samia atabonyeza kitufe kama ishara ya kuziba lile Diversion Tunnel ili kuanza kujaza bwawa maji ya kufua umeme, hiyo ni hatua kubwa sana.
Hongera TANESCO na TANROADS kwa kusimamia kazi hii muhimu kwa Taifa.
Geti lenyewe ndiyo hilo kwenye picha, na huo mto mxima wa zRufiji kwa sasa ulikuwa unapita humo.
Kuna waliibeza, waliosema hakuna cha geti wala nini.
Hilo geti tunaloliona karibia lote litakuwa chini ya maji bwawa likijaa.
Hongera nchi yangu Tanzania.