Bwawa la Stiegler's Gorge kuanza kujengwa na kampuni ya Misri

Kampuni ya nchini Misri inayomilikiwa na serikali, Arab Contractors imeshinda tenda ya kubuni/kusanifu na kujenga bwawa la Stiegler's Gorge katika maporomoko ya mto Rufiji.

Baada ya Kampuni hiyo kushinda tenda, Rais wa Misri, Abdel-Fattah al-Sisi amempigia simu Rais Magufuli na kutoa shukrani huku akimwambia kama atamkaribisha atapenda kuhudhuria katika sherehe ya uwekaji wa jiwe la Msingi la ujenzi wa bwawa hilo kuonyesha mahusiano ya karibu ya kiuchumi kati ya nchi yake na Tanzania.

Rais Abdel-Fattah al-Sisi aliwahi kutembelea Tanzania mwaka 2017. Kabla ya Al Sisi, Rais wa mwisho kutoka Misri kuitembelea Tanzania ilikuwa mwaka 1968.

Kampuni ya Al Moqaweloon Al Arab iliyoshinda tenda inasifiwa kwa kazi mbali mbali za ujenzi ambazo inazifanya hasa katika nchi nyingi za Mashariki ya Kati na barani Afrika.

Hii ni kampuni ambayo imejenga bwawa linaloitwa Aswan high dam mwaka 1970 ambalo liko nchini Misri. Bwawa hili liligharimu zaidi ya US $1 bilioni.

Inakadiriwa bwawa la Stiegler's Gorge likimalizika kujengwa litatoa umeme wa zaidi ya 2,100 MW. Kwa sasa Tanzania ina uwezo wa kuzalisha umeme wa 1,540 MW nchi nzima.

Good Thing; Like Grand Ethiopia Rennaisance Dam 6,000 MW, China 3 Gorges Dam (22,500MW) and DRC - Grand Inga 39,000 MW
 
Big up
Kwa kweli Egyptians wanastahili kupata hiyo tender
Wako mbali sana wenzetu na taifa la zamani na uzuri ni wenzetu.

Tujifunze mengi kutoka kwao na kama Al Sisi atakuja wafungue tu biashara na Misri
 
Swali la msingi hapo ni mkopo umepatikana?
Hakuna mfadhili wowote aliyeonyesha nia ya kutoa mkopo kwenye uo mradi na nchi za magharibi ndiyo kabisa hawawezi maana walitaka kuuzuia ila Rais kaukomalia na Mh alishasema tutfanya hata kwa fedha zetu za ndani! Ujenzi wa uo mradi ghalama zake sawa tu na Kipande cha Reli ya SGR toka Dar mpaka Morogoro ambacho tumeghalamia kwa fedha zetu za ndani.
 
Kampuni ya nchini Misri inayomilikiwa na serikali, Arab Contractors imeshinda tenda ya kubuni/kusanifu na kujenga bwawa la Stiegler's Gorge katika maporomoko ya mto Rufiji.

Baada ya Kampuni hiyo kushinda tenda, Rais wa Misri, Abdel-Fattah al-Sisi amempigia simu Rais Magufuli na kutoa shukrani huku akimwambia kama atamkaribisha atapenda kuhudhuria katika sherehe ya uwekaji wa jiwe la Msingi la ujenzi wa bwawa hilo kuonyesha mahusiano ya karibu ya kiuchumi kati ya nchi yake na Tanzania.

Rais Abdel-Fattah al-Sisi aliwahi kutembelea Tanzania mwaka 2017. Kabla ya Al Sisi, Rais wa mwisho kutoka Misri kuitembelea Tanzania ilikuwa mwaka 1968.

Kampuni ya Al Moqaweloon Al Arab iliyoshinda tenda inasifiwa kwa kazi mbali mbali za ujenzi ambazo inazifanya hasa katika nchi nyingi za Mashariki ya Kati na barani Afrika.

Hii ni kampuni ambayo imejenga bwawa linaloitwa Aswan high dam mwaka 1970 ambalo liko nchini Misri. Bwawa hili liligharimu zaidi ya US $1 bilioni.

Inakadiriwa bwawa la Stiegler's Gorge likimalizika kujengwa litatoa umeme wa zaidi ya 2,100 MW. Kwa sasa Tanzania ina uwezo wa kuzalisha umeme wa 1,540 MW nchi nzima.

Halafu wakimaliza kujenga, mbali ya malipo yao wanayostahili kupewa kama haki yao, tunawatafutia na zawadi!
 
Big up
Kwa kweli Egyptians wanastahili kupata hiyo tender
Wako mbali sana wenzetu na taifa la zamani na uzuri ni wenzetu.

Tujifunze mengi kutoka kwao na kama Al Sisi atakuja wafungue tu biashara na Misri
Kwa tukio hili inaonyesha siku hizi nchi haina watu wanaofikiri na kuona mbele..hivi mtu ambaye anakulalamikia juu ya kuamua kuongeza matumizi ya maji ya ziwa viktoria anaweza tena kuwa mjenzi wako wa bwawa la umeme na ukamwamini atajenga vzr??? sidhani!
 
Kampuni ya nchini Misri inayomilikiwa na serikali, Arab Contractors imeshinda tenda ya kubuni/kusanifu na kujenga bwawa la Stiegler's Gorge katika maporomoko ya mto Rufiji.

Baada ya Kampuni hiyo kushinda tenda, Rais wa Misri, Abdel-Fattah al-Sisi amempigia simu Rais Magufuli na kutoa shukrani huku akimwambia kama atamkaribisha atapenda kuhudhuria katika sherehe ya uwekaji wa jiwe la Msingi la ujenzi wa bwawa hilo kuonyesha mahusiano ya karibu ya kiuchumi kati ya nchi yake na Tanzania.

Rais Abdel-Fattah al-Sisi aliwahi kutembelea Tanzania mwaka 2017. Kabla ya Al Sisi, Rais wa mwisho kutoka Misri kuitembelea Tanzania ilikuwa mwaka 1968.

Kampuni ya Al Moqaweloon Al Arab iliyoshinda tenda inasifiwa kwa kazi mbali mbali za ujenzi ambazo inazifanya hasa katika nchi nyingi za Mashariki ya Kati na barani Afrika.

Hii ni kampuni ambayo imejenga bwawa linaloitwa Aswan high dam mwaka 1970 ambalo liko nchini Misri. Bwawa hili liligharimu zaidi ya US $1 bilioni.

Inakadiriwa bwawa la Stiegler's Gorge likimalizika kujengwa litatoa umeme wa zaidi ya 2,100 MW. Kwa sasa Tanzania ina uwezo wa kuzalisha umeme wa 1,540 MW nchi nzima.
Nimepitia website ya PPRA sijaona report yoyote ya mchakato wa manunuzi, hebu tusaidie maswali yafuatayo
1. Tender ilitangazwa link na wapi??
2. Tender ni ya aina gani/ local/ interational/
3. Consultant ni nani?? design and build??
4. Bidders wengine nikina nani?
6. Criteria za kumpata lowest evaluated bidder in zipi??
 
Sasaivi tunafanya kazi kizalendo zaidi.
Nimepitia website ya PPRA sijaona report yoyote ya mchakato wa manunuzi, hebu tusaidie maswali yafuatayo
1. Tender ilitangazwa link na wapi??
2. Tender ni ya aina gani/ local/ interational/
3. Consultant ni nani?? design and build??
4. Bidders wengine nikina nani?
6. Criteria za kumpata lowest evaluated bidder in zipi??
 
Ule mkopo wa ujenzi wa hilo bwawa umepatikana au umeandika kuwakoga wasiojitambua na kuua hii aibu ya sinema ya MO?
tindo bana!,akili yako hili lisiwezekane sio,siasa gani hizi?,wewe ni mtizedi kweli?,mmh!
 
Nimepitia website ya PPRA sijaona report yoyote ya mchakato wa manunuzi, hebu tusaidie maswali yafuatayo
1. Tender ilitangazwa link na wapi??
2. Tender ni ya aina gani/ local/ interational/
3. Consultant ni nani?? design and build??
4. Bidders wengine nikina nani?
6. Criteria za kumpata lowest evaluated bidder in zipi??
Habari mkuu, sipo katika mjadala lakini naomba nikukumbushe kuna kitu kinaitwa "selective tendering" yaan client anaandaa bajeti then anakupa contractor kujenga
 
Uhuru wa kuwachagua viongozi tuwapendao ni muhumu zaidi badala ya kusimikwa wale ccm inaowataka.
 
Habari mkuu, sipo katika mjadala lakini naomba nikukumbushe kuna kitu kinaitwa "selective tendering" yaan client anaandaa bajeti then anakupa contractor kujenga
Selective tendeering labda project yakupeleka shuttle kwenye space, kujenga dam ni simple engineering hata Skol au Delmonte akiwezeshwa anajenga
 
Kwa tukio hili inaonyesha siku hizi nchi haina watu wanaofikiri na kuona mbele..hivi mtu ambaye anakulalamikia juu ya kuamua kuongeza matumizi ya maji ya ziwa viktoria anaweza tena kuwa mjenzi wako wa bwawa la umeme na ukamwamini atajenga vzr??? sidhani!
Hawa ni wakandarasi, wanaangalia maslahi yao tu
Na suala la mto Nile ni suala la kitaifa na yalienda vizuri
 
Hakuna mfadhili wowote aliyeonyesha nia ya kutoa mkopo kwenye uo mradi na nchi za magharibi ndiyo kabisa hawawezi maana walitaka kuuzuia ila Rais kaukomalia na Mh alishasema tutfanya hata kwa fedha zetu za ndani! Ujenzi wa uo mradi ghalama zake sawa tu na Kipande cha Reli ya SGR toka Dar mpaka Morogoro ambacho tumeghalamia kwa fedha zetu za ndani.

Mradi wa SGR ni 7t, fedha za ndani imesemekana itakuwa 1t. Mkopo bado kutoka China, itategemea kama China watatoa. Ila wasipotoa hata kipande cha Dar-Moro itakuwa ngumu kukamilika.
 
tindo bana!,akili yako hili lisiwezekane sio,siasa gani hizi?,wewe ni mtizedi kweli?,mmh!

Kuwa mtizedi ni kutokuhoji ukweli? Tofauti yangu na yako, ww unapima utizedi wako kwa kukubali chochote cha serekali bila kuhoji, wakati mimi nahoji chochote cha serekali. Isitoshe hiyo miradi haujengwi kwa uzalendo zaidi bali kisiasa zaidi, hivyo kupelekea sisi wengine kuhoji.

Nasema hivi kwa sababu mwanzo ilisemekana hizo 3t za huo mradi zipo na nilisema toka mwanzo hizo pesa hakuna. Mnaosifia kila kitu mkaingia hadaa eti kwa kuwa tender ilishatangazwa. Baadae muda ulivyosonga ukweli ukawa peupe kwamba ni mkopo unatafutwa. Hivyo nimehoji pesa zipo sio wa bahati mbaya bali najua ni utapeli kama utapeli mwingine.
 
Back
Top Bottom