Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 16,419
- 26,594
Suala la Bandari linajadiliwa kwa marefu na mapana kila kona ya nchi.
Maandamano ya vyama vya upinzani yameshaanza mikoani kupinga suala zima la ubinafsishaji/uuzwaji/ukodishaji, au hata kuigawa bure Bandari yetu na nyingine Tanzania.
Tukubali tusikubali, serikali ya CCM imeingia mkenge mkubwa kutowajulisha wenye nchi juu ya rasilimali kubwa na zinazotaka kubinafsishwa kwa kampuni ya kutoka Dubai, DP World.
Suala si kubinafsisha tu, suala ni mustakabali mzima wa kisiasa, na kushindwa kwa serikali kuelezea kwa maneno mepesi na yanayoeleweka juu ya ubinafsishaji huu wa Bandari zetu.
Kama CCM haikuliona hili kuwa suala zito basi sasa ifungue macho, 2025 siyo mbali.
Mimi ni kada wa chama, na kwa yote tunyoyaona mitandaoni na maelezo yasiyoeleweka kutoka Wizara husika ya Ujenzi, mikataba inayotuchanganya, bunge linaloitikia ndiyoooo.....!, bila uchambuzi wa kina, basi kwa CCM huu ni mtaji mbaya.
Yote haya hayaleti imani kwa CCM, na huku mitaani inanyooshewa kidole cha lawama.
Mtaji huu wa mikataba ambayo ni kama tumefumbwa macho na wananchi hawana elimu ya kutosha, CCM itavuna kama inavyostahili.