CCM, kwa mtaji wa ukakasi wa suala la Bandari, kaeni mguu sawa kung'olewa!

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
16,419
Reaction score
26,594
Suala la Bandari linajadiliwa kwa marefu na mapana kila kona ya nchi.

Maandamano ya vyama vya upinzani yameshaanza mikoani kupinga suala zima la ubinafsishaji/uuzwaji/ukodishaji, au hata kuigawa bure Bandari yetu na nyingine Tanzania.

Tukubali tusikubali, serikali ya CCM imeingia mkenge mkubwa kutowajulisha wenye nchi juu ya rasilimali kubwa na zinazotaka kubinafsishwa kwa kampuni ya kutoka Dubai, DP World.

Suala si kubinafsisha tu, suala ni mustakabali mzima wa kisiasa, na kushindwa kwa serikali kuelezea kwa maneno mepesi na yanayoeleweka juu ya ubinafsishaji huu wa Bandari zetu.

Kama CCM haikuliona hili kuwa suala zito basi sasa ifungue macho, 2025 siyo mbali.
Mimi ni kada wa chama, na kwa yote tunyoyaona mitandaoni na maelezo yasiyoeleweka kutoka Wizara husika ya Ujenzi, mikataba inayotuchanganya, bunge linaloitikia ndiyoooo.....!, bila uchambuzi wa kina, basi kwa CCM huu ni mtaji mbaya.

Yote haya hayaleti imani kwa CCM, na huku mitaani inanyooshewa kidole cha lawama.

Mtaji huu wa mikataba ambayo ni kama tumefumbwa macho na wananchi hawana elimu ya kutosha, CCM itavuna kama inavyostahili.
 
Nimefurahi kuona kwamba wapo walioamua kulipigania hili jambo kwa njia tofauti, wapo walioamua kupambana mitandaoni, wapo walioamua kwenda mahakamani, na wapo walioandamana.

Hizo zote zimekuwa ni njia za watanganyika kufikisha ujumbe wao, kwamba hawajaridhishwa na ubovu wa ule mkataba, ulioamua kuzitoa sadaka bandari zetu zote ndani ya Tanganyika.

Mwisho wa siku naamini jambo moja, kama Samia ataendelea kuziba masikio, asisikie hizi sauti zote zinazomtaka atuondoe kwenye ule mkataba, basi atambue, siku inakuja, makundi hayo matatu yataungana kwa pamoja, yaamue kufanya jambo moja, chini ya uratibu mmoja.

Ajiandae. Kuwa kiongozi wa watanganyika maana yake ni kusimamia mali zao, lakini sio kuzigawa kwa ndugu na marafiki zako.
 
Siyo kwa sanduku la kura na kumwachia DED atangaze matokeo. Labda wang'olewe na usalama wa taifa au wapigane fitna kwa kuvujisha Siri au mahakama ziwe huru ili wang'olewe kisheria au Mungu aamue ugomvi.
 
Kinachosikitisha ni taasisi kama Usalama wa Taifa, taasisi za kizalendo na zilizo ndani ya roho ya utaifa wa Tanzania, najiuliza kuwa huu ukakasi hawakuuona na kuuchukulia hatua?
 
Suala la Bandari linajadiliwa kwa marefu na mapana kila kona ya nchi.

Kama CCM haikuliona hili kuwa suala zito basi sasa ifungue macho, 2025 siyo mbali. Mimi ni kada wa chama, na kwa yote tunyoyaona mitandaoni na maelezo yasiyoeleweka kutoka Wizara husika ya Ujenzi, mikataba inayotuchanganya, bunge linaloitikia ndiyoooo, bila uchambuzi wa kina, basi kwa CCM huu ni mtaji mbaya.
Yote haya hayaleti imani kwa CCM, na huku mitaani inanyooshewa kidole cha lawama.

Mtaji huu wa mikataba ambayo ni kama tumefumbwa macho na wanannchi hawana elimu ya kutosha, CCM itavuna kama inavyostahili.
Mkuu Jidu, Jidu La Mabambasi , usiwe na shaka yoyote na Watanzania, Watanzania ni watu poa sana, hata uwafanyie nini, watapiga tuu kelele kujifanya wana hasira sana, lakini ukifika ule muda wa kuchagua, ni wanachagua kile kile chetu chama numberi uno!.
Zimwi likujualo...

P
 
Kuing'oa ccm madarakani ni ndoto za mchana ama ni kauli za kujipa moyo tu.

Kama kweli suala la DP World limewagusa njia sahihi ya kupambana na Hilo ni kutunga katiba mpya. Vinginevyo ccm itaendelea kuwepo.
 
Kuhusu uchaguzi kutolewa CCM madarakani ni mazingaombwee, wakati Tume ya uchaguzi ishateuliwa juzi, na wamejaa wa kulee jambiani. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Kazii ipooo.
Kwa hiyo unamaanisha kwamba labda mungu aingilie hili bifu [emoji1787] kati yetu na hao
 
Kwa nchii hii, mabifu na migogoro ina amuliwa na muweza wa yotee, maana yeye hapangiwi, haangalii una kinga dhidi ya wenzio au huna, anaku adhibu tyuuh chwaaah. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Suala la Bandari linajadiliwa kwa marefu na mapana kila kona ya nchi.

Maandamano ya vyama vya upinzani yameshaanza mikoani kupinga suala zima la ubinafsishaji/uuzwaji/ukodishaji, au hata kuigawa bure Bandari yetu na nyingine Tanzania.

Tukubali tusikubali, serikali ya CCM imeingia mkenge mkubwa kutwajulisha wenye nchi juu ya rasilimali kubwa na zinazotaka kubinafsihwa kwa kampuni ya kutoka Dubai DP World.

Suala si kubinafsisha tu, suala ni mustakabali mzima wa kisiasa, na kushindwa kwa serikali kuelezea kwa maneno mepesi na yanayoeleweka juu ya ubinafsishaji huu wa Bandari zetu.

Kama CCM haikuliona hili kuwa suala zito basi sasa ifungue macho, 2025 siyo mbali. Mimi ni kada wa chama, na kwa yote tunyoyaona mitandaoni na maelezo yasiyoeleweka kutoka Wizara husika ya Ujenzi, mikataba inayotuchanganya, bunge linaloitikia ndiyoooo, bila uchambuzi wa kina, basi kwa CCM huu ni mtaji mbaya.

Yote haya hayaleti imani kwa CCM, na huku mitaani inanyooshewa kidole cha lawama.

Mtaji huu wa mikataba ambayo ni kama tumefumbwa macho na wanannchi hawana elimu ya kutosha, CCM itavuna kama inavyostahili.
Ni kweli kuna msemo kuwa ukubwa na nguvu za tembo pia ndiyo udhaifu wake ulipo. Shuhudia tembo akizama kwenye matope. Kila akitumia nguvu zake kujikwamua ndivyo anavyodidimia. CCM ichukue hadhari.
 
Suala la Bandari linajadiliwa kwa marefu na mapana kila kona ya nchi.

Maandamano ya vyama vya upinzani yameshaanza mikoani kupinga suala zima la ubinafsishaji/uuzwaji/ukodishaji, au hata kuigawa bure Bandari yetu na nyingine Tanzania.

Tukubali tusikubali, serikali ya CCM imeingia mkenge mkubwa kutwajulisha wenye nchi juu ya rasilimali kubwa na zinazotaka kubinafsihwa kwa kampuni ya kutoka Dubai DP World.

Suala si kubinafsisha tu, suala ni mustakabali mzima wa kisiasa, na kushindwa kwa serikali kuelezea kwa maneno mepesi na yanayoeleweka juu ya ubinafsishaji huu wa Bandari zetu.

Kama CCM haikuliona hili kuwa suala zito basi sasa ifungue macho, 2025 siyo mbali. Mimi ni kada wa chama, na kwa yote tunyoyaona mitandaoni na maelezo yasiyoeleweka kutoka Wizara husika ya Ujenzi, mikataba inayotuchanganya, bunge linaloitikia ndiyoooo, bila uchambuzi wa kina, basi kwa CCM huu ni mtaji mbaya.

Yote haya hayaleti imani kwa CCM, na huku mitaani inanyooshewa kidole cha lawama.

Mtaji huu wa mikataba ambayo ni kama tumefumbwa macho na wanannchi hawana elimu ya kutosha, CCM itavuna kama inavyostahili.
Ccm hatong'oki ng'oo. Kwani we ndo Huwa unatuweka madarakani au tunajiweka wenyewe. We piga kura timiza wajibu wako lakini kutangaza ni kazi yetu
 
Kwa nchii hii, mabifu na migogoro ina amuliwa na muweza wa yotee, maana yeye hapangiwi, haangalii una kinga dhidi ya wenzio au huna, anaku adhibu tyuuh chwaaah. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Nimekuelewa sana binafsi [emoji119][emoji119][emoji119][emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom