Pre GE2025 CCM wamchangia Lissu Milioni 5 atengeneze gari lake. Lissu azipokea
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel Nchimbi amewaongoza wajumbe wa NEC alioongoza nao ziarani mkoani Mwanza na wanachama wa chama hicho mkoani humo wamemchangia Shilingi Milioni Tano Makamu Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA, Tundu Lissu ili kufanyia matengenezo gari yake.

Pia soma: Lissu na CHADEMA wasikubali kejeli, dhihaka na dharau za kuchangiwa na CCM

Kada wa CCM, Mchungaji Peter Msigwa akiwa kwenye mkutano wa chama hicho kwenye uwanja wa Furahisha jijini Mwanza alimuomba Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Nchimbi kuhamasisha wanachama wa CCM kumchangia Lissu ili gari hilo limuwezeshe kufanya shughuli za siasa.

Kwa upande wake, Dkt Emmanuel Nchimbi amesema siasa si uadui hivyo ni vyema kushikana mkono pale panapobidi kwani wanasiasa wote wanaijenga Tanzania.


Alipotafutwa kuzungumzia kitendo hicho kilichofanywa na CCM, Lissu amewashukuru CCM kwa mchango na kwamba atazipokea fedha hizo kama ambayo amekuwa akipokea kutoka kwa makundi tofauti ya watu.

Pia soma: Tumechanga kiasi gani kwaajili ya gari ya Tundu Lissu? Mbona kimya kingi?

"Nawashukuru, kama nilivyosema...hatukusema tunachangiwa na wanaChadema peke yao, kama nilivyotibiwa, sikutibiwa na wanaChadema peke yao. Kwa hiyo, wakichangia nitazipokea, sina sababu ya kukataa," amesema Lissu.


Mwananchi
 
Hizo hela za Majini hazina nafasi kwa Lissu, Wapeni mnaowaita Wanyonge

Screenshot_2024-08-13-17-11-43-1.png
 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel Nchimbi amewaongoza wajumbe wa NEC alioongoza nao ziarani mkoani Mwanza na wanachama wa chama hicho mkoani humo wamemchangia Shilingi Milioni Tano Makamu Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA,...
Alikataa ile hongo ya Abdul sasa Msigwa kamtumia Nchimbi.

Kuna issue Ccm wana itega kwa Lissu. Soon ita kuwa wazi. Usishangae Lissu akaenda kupokelea huo mchango Lumumba
 
Kada wa CCM, Mchungaji Peter Msigwa akiwa kwenye mkutano wa chama hicho kwenye uwanja wa Furahisha jijini Mwanza alimuomba Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Nchimbi kuhamasisha wanachama wa CCM kumchangia Lissu ili gari hilo limuwezeshe kufanya shughuli za siasa
Limuwezeshe kufanya shughuli gani za kisiasa?

wakati yeye anasema kila siku cdm ni saccos ya mbowe.

Ndio kusema anataka saccoss iendelee kukua?

Msigwa is totally an I.D.I.O.T
 
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemchangia shilingi milioni tano Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu ili kufanya matengenezo ya gari yake na limuwezeshe katika shughuli za siasa.

Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema siasa si uadui hivyo ni vyema kushikana mkono panapobidi kwani wanasiasa wote wanaijenga Tanzania.

Gari hiyo aina ya Toyota Landcruiser V8, VXR alilokuwa amepanda Lissu lilishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana miaka saba iliyopita.
 
Back
Top Bottom