Pre GE2025 CCM wamchangia Lissu Milioni 5 atengeneze gari lake. Lissu azipokea
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Akili ndogo hizo fedha pelekeni kwenye Matundu ya vyoo hapo Buzuruga shule ya msingi...
 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel Nchimbi amewaongoza wajumbe wa NEC alioongoza nao ziarani mkoani Mwanza na wanachama wa chama hicho mkoani...
wasiishie tu kumchangia, tunataka kumjua aliye mpiga risasi kijana wa watu na kumpa kilema cha maisha ni nani? uchunguzi umeishia wapi?

hizi cheap politics ndio tatizo lenyewe humo ccm. Leteni mambo ya maana , tujue kwamba muko serious na sisi munaotuongoza.... Uchunguzi na mashtaka ya walio mshambulia umefikia wapi? Jibuni hilo swali kabla ya kuchanga...mchango uje na majibu ya watesi wake ni nani?
 
Nakuonea huruma umechelewa kuwafahamu hawa wanasiasa wa nchi hii.
 
Hizi ni dalili muhimu sana toka CCM kuonyesha hofu yao kwa Tundu Lissu. Fikra zao zote wamezielekeza kwenye njia za kumbana Tundu Lissu sasa hivi;kwa sababu ni tishio kubwa kwao.

..lakini Mch.Msigwa kushiriki mizaha kama hii dhidi ya Lissu ni jambo ambalo linasikitisha sana. Hata kama ameamua kujitoa ufahamu sio kwa kiwango hiki anachofanya kumdhihaki Lissu.
 
Mimi nimejaaliwa kuzira ,yaani juzi umeniking'uta viboko eti Leo unipe tuhela kunipoza ? Ningesema nashukuru hata Kama Sina
 
..lakini Mch.Msigwa kushiriki mizaha kama hii dhidi ya Lissu ni jambo ambalo linasikitisha sana. Hata kama ameamua kujitoa ufahamu sio kwa kiwango hiki anachofanya kumdhihaki Lissu.
Huyo Msigwa ni mtu 'desperate' sana wakati huu; hawezi kuwa na kikomo cha "kusikitisha".

Lakini ngoja nikurudishe nyuma kidogo kabla ya huyo Msigwa kuondoka CHADEMA na alivyo jaribu kumhusisha Tundu Lissu wakati huo na hujuma alizokuwa anazifanya mara tu kabla hajatangazwa kuwa kaenda CCM.

Ukielewa hujuma iliyokuwa ikilengwa wakati huo, pengine itasaidia kuelewa mwendelezo wa juhudi hizi wakati huu.
 
Upumbavu mkubwa sana
Kwa hiyo mtu ana shida, na pesa imekuja mkononi hasipokee?

Jamaa alioomba pesa za gari siku nyingi lakin bado hazijatimia, na nyie mpo mumeshindwa kumsaidia, kazi kutumia keyboard kupiga kelele tu bila msaada.,na pesa imeletwa, lazima achukue:

Mwenyekiti wa, kudumu mpaka leo hajamchangia wala kumpa gari!!
 
CCM haina uadui na Mwanachama wa Chama chochote cha siasa, hizi ndio siasa za kisasa…!!

Wafuasi wachache wa Chadema yalivyo primitive yatapinga, sbb hawajui maana ya siasa za kisasa

Juzi Katibu Mkuu wetu Dr. Nchimbi alihuzunishwa na viongozi wa Chadema kukamatwa, na akatoa amri waachiwe haraka na wakaachiwa, hizi ndio siasa za kisasa za Mama yetu Samia Suluhu ambaye aliruhusu mfanye siasa na mikutano ya hadhara kwa uwazi, ingawa Chadema bado mnamtusi na kumdharau sana Mh. Rais wetu
 
Msigwa alikuwa anahangaika na Mbowe kila siku kwasababu hakuwa na jiwe la kumpigia Lissu, sasa naona ameshalipata hilo jiwe.

Tusubiri.
Bado sana. Sioni "jiwe" la kumrushia Lissu hapa.

'Tehnically', hii pesa iliyo/itakayo changishwa siyo ya CCM, pamoja na kwamba itakuwa imeratibiwa na viongozi wa CCM, na inachangwa na watu binafsi, ambao wapo CCM.
Kwani hawa hawa wanaochanga ikifika wakati wa kupiga kura wakampigia kura Tundu Lissu, kuna mtu atakaye wahoji kutumia uhuru wao huo?
 
Back
Top Bottom