Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Binafsi sioni shida. Kuna mambo unaweza kukataa, lakini kuna mambo mengine ukubali au ukatae hayana effect yoyote. Ila yakikufanya ulainike, na kuanza kuimba mapambio labda. Otherwise, mchango kama mchango sioni shida. Ni kama sadaka za kanisani zinatoka kwa watu wa makundi mbalimbali, wema na wabaya. Na hapa sina maana kwamba CCM ni wabaya na mkundi mengine ni wema, ila kwamba hatuna njia ya kumpima mtu kwamba huyu atoe sadaka na huyu asitoe. Kwa mfano, hata hizo fedha zingine zilizochangwa, kama kuna wana-CCM waliochangia Tundu Lissu atawajuaje ili awarudishie? Unaona ilivyo ngumu? Anyway, ni maoni yangu.Kwa nini ukubali pesa ya laana?
View attachment 3071048
Naona doa hapa tayari, ilikuwa simple tu Lissu aseme ahsanteni kwa moyo wenu ila hizo pesa pelekeni kuweka madawati kwa watoto wanaokaa chini, hapa angekuwa amejibu vizuri sana na kupata wafuasi.Bado sana. Sioni "jiwe" la kumrushia Lissu hapa.
'Tehnically', hii pesa iliyo/itakayo changishwa siyo ya CCM, pamoja na kwamba itakuwa imeratibiwa na viongozi wa CCM, na inachangwa na watu binafsi, ambao wapo CCM.
Kwani hawa hawa wanaochanga ikifika wakati wa kupiga kura wakampigia kura Tundu Lissu, kuna mtu atakaye wahoji kutumia uhuru wao huo?
Hii nimeipenda,na hivi ndivyo siasa inatakiwa iwe🤣🤣🤣Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel Nchimbi amewaongoza wajumbe wa NEC alioongoza nao ziarani mkoani Mwanza na wanachama wa chama hicho mkoani humo wamemchangia Shilingi Milioni Tano Makamu Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA, Tundu Lissu ili kufanyia matengenezo gari yake.
Kada wa CCM, Mchungaji Peter Msigwa akiwa kwenye mkutano wa chama hicho kwenye uwanja wa Furahisha jijini Mwanza alimuomba Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Nchimbi kuhamasisha wanachama wa CCM kumchangia Lissu ili gari hilo limuwezeshe kufanya shughuli za siasa.
Kwa upande wake, Dkt Emmanuel Nchimbi amesema siasa si uadui hivyo ni vyema kushikana mkono pale panapobidi kwani wanasiasa wote wanaijenga Tanzania.
Alipotafutwa kuzungumzia kitendo hicho kilichofanywa na CCM, Lissu amewashukuru CCM kwa mchango na kwamba atazipokea fedha hizo kama ambayo amekuwa akipokea kutoka kwa makundi tofauti ya watu.
"Nawashukuru, kama nilivyosema...hatukusema tunachangiwa na wanaChadema peke yao, kama nilivyotibiwa, sikutibiwa na wanaChadema peke yao. Kwa hiyo, wakichangia nitazipokea, sina sababu ya kukataa," amesema Lissu.
Mwananchi
Vile virungu vya polisi juzi kule Mbeya kwa viongozi wa Chadema akiwemo Lissu mwenyewe ndio "urafiki" unaozungumzia hapa?!CCM haina uadui na Mwanachama wa Chama chochote cha siasa, hizi ndio siasa za kisasa…!!
Wafuasi wachache wa Chadema yalivyo primitive yatapinga, sbb hawajui maana ya siasa za kisasa
Juzi Katibu Mkuu wetu Dr. Nchimbi alihuzunishwa na viongozi wa Chadema kukamatwa, na akatoa amri waachiwe haraka na wakaachiwa, hizi ndio siasa za kisasa za Mama yetu Samia Suluhu ambaye aliruhusu mfanye siasa na mikutano ya hadhara kwa uwazi, ingawa Chadema bado mnamtusi na kumdharau sana Mh. Rais wetu
Ninakubaliana nawe sehemu kubwa.Naona doa hapa tayari, ilikuwa simple tu Lissu aseme ahsanteni kwa moyo wenu ila hizo pesa pelekeni kuweka madawati kwa watoto wanaokaa chini, hapa angekuwa amejibu vizuri sana na kupata wafuasi.
Lakini hawa CCM, ambao juzi tu wametoka kuwacharaza virungu viongozi wa Chadema kupitia polisi wao, virungu vilivyomhusisha Lissu mwenyewe, leo kutoa mchango kwa Lissu na kupokewa, hii kwangu automatically wameshajinasua kwenye ule ujinga wao waliofanya juzi kule Mbeya.
Now wakiulizwa simply watajibu Chadema ni marafiki zetu kwenye siasa, ndio maana juzi tumemchangia Lissu apate gari mpya!.
Waongo, wanalazimisha 4R kwa Lissu wakati Samia mwanzilishi ameshazipiga teke, huu mtego Lissu na Chadema wamenasa!.
Hapa ndipo na mimi nishindwa kuacha kumshangaa mtoa mada.Watu wamejichangisha huko wenyewe, hata pesa haijapelekwa umeanza kumlaumu Lissu. Umeingia kwenye mtego mapema Sana.
Endeleaaaaa na chama chakoo wenzio wanakula hela mnaishia kupiga keleleeKwa nini ukubali pesa ya laana?
View attachment 3071048
Mtoa mada kakurupuka!!Hapa ndipo na mimi nishindwa kuacha kumshangaa mtoa mada.
Pesa hizo hazikutoka CCM zimetoka kwa watanzania ambao hawskufurahishwa na kitendo cha serikali ya Magufuli.Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel Nchimbi amewaongoza wajumbe wa NEC alioongoza nao ziarani mkoani Mwanza na wanachama wa chama hicho mkoani humo wamemchangia Shilingi Milioni Tano Makamu Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA, Tundu Lissu ili kufanyia matengenezo gari yake.
Kada wa CCM, Mchungaji Peter Msigwa akiwa kwenye mkutano wa chama hicho kwenye uwanja wa Furahisha jijini Mwanza alimuomba Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Nchimbi kuhamasisha wanachama wa CCM kumchangia Lissu ili gari hilo limuwezeshe kufanya shughuli za siasa.
Kwa upande wake, Dkt Emmanuel Nchimbi amesema siasa si uadui hivyo ni vyema kushikana mkono pale panapobidi kwani wanasiasa wote wanaijenga Tanzania.
Alipotafutwa kuzungumzia kitendo hicho kilichofanywa na CCM, Lissu amewashukuru CCM kwa mchango na kwamba atazipokea fedha hizo kama ambayo amekuwa akipokea kutoka kwa makundi tofauti ya watu.
"Nawashukuru, kama nilivyosema...hatukusema tunachangiwa na wanaChadema peke yao, kama nilivyotibiwa, sikutibiwa na wanaChadema peke yao. Kwa hiyo, wakichangia nitazipokea, sina sababu ya kukataa," amesema Lissu.
Mwananchi
Kuachana nayo si sahihi, hiyo pesa haijatoka kwenye mfuko wa CCM, kwani Lissu hana ndugu wanachama wa CCM, nao awakatae! Hapana.Ninakubaliana nawe sehemu kubwa.
Lakini hapo hapo elewa kwamba huko CCM siyo wote ni akina .... eeerrr-eerrr-eh, nani yule polisi anaitwa yule?
Huko ndani ya CCM sasa hivi kuna mashetani kweli kweli, wasioona kitu kingine zaidi ya kumpambania 'Chura Kiziwi'; lakini pia kuna watu wanaoweza kuaminika na kuheshimika; kama huyo Nchimbi.
Hivi kwa maoni yako, hii pesa iliyo changwa ni sawa na ile ya Abdul, ambayo Lissu amekuwa akiipigia kelele? Mimi naona tofauti kubwa.
Kiukweli, milioni tano si pesa ya kudhalilishwa nayo; kama lengo ni kufanya hivyo, Tundu Lissu aachane nayo.