Pre GE2025 CCM yamchagua Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza katika Uchaguzi wa Oktoba 2025

Pre GE2025 CCM yamchagua Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza katika Uchaguzi wa Oktoba 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hahaha sasa nyie mambo ya ccm yanawahusu nini?

Mlitaka awe nani sasa Philip Mangula?
 
This time rough plays zitakuwa za kutosha, yale yale ya Gezaulole Kigambonini.
 
kwa nini siyo P.Mpango? haijawahi kutokea tanzagiza raisi akabadilisha mgombea mwenza ngwe ya pili, nafikiri kuna kitu kinaendelea na sii kidogo kwenye nchi yetu, mficha ugonjwa kifo kitamuumbua …
Kaomba kupumzika
 
kwa nini siyo P.Mpango? haijawahi kutokea tanzagiza raisi akabadilisha mgombea mwenza ngwe ya pili, nafikiri kuna kitu kinaendelea na sii kidogo kwenye nchi yetu, mficha ugonjwa kifo kitamuumbua …
Kikwete alibadili kwenye muhula wake wa pili baada ya Dk Shein kwenda kugombea Uraisi wa Zanzibar
 
Kwa hiyo kuanzia 2030 uwezekano ni mkubwa kuwa CHADEMA wakawa wanapambana na Nchimbi. Huu utakuwa wakati mzuri kwa CHADEMA kuweza kufurukuta, kuna uwezekano mkubwa. Kwa ujumla Nchimbi ni mwanademokrasia lakini pia ni mtu dhaifu. CHADEMA jipangeni vizuri.
Wanaweza kumkaribisha akawe mgombea mwenza
 
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni mgombea urais, Samia Suluhu Hassan amempendekeza Katibu Mkuu wa chama hicho, Dkt. Emmanuel Nchimbi kuwa mgombea mwenza katika uchaguzi utakaofanyika Oktoba 2025.
View attachment 3206628
Dkt. Nchimbi ambaye aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM Januari 15, 2024 katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya chama hicho kilichofanyikia Unguja, visiwani Zanzibar.

Pia, Soma: Wajumbe Mkutano Mkuu CCM wapitisha Rais Samia, Dkt. Mwinyi kugombea Urais 2025

View attachment 3206644
Dkt. Nchimbi alichukua nafasi iliyoachwa wazi na Daniel Chongolo aliyejiuzulu Novemba 29, 2023. Rais Samia amempendekeza Dkt. Nchimbi leo Jumapili, Januari 19, 2025 katika mkutano mkuu maalumu jijini Dodoma.
Mapichapicha tu....
🚮🚮🚮
 
Naskia January na Nape wamelia kwa uchungu sana
 
Kwahiyo yule aliyeogopa kukalia kiti mama aliposafiri ndiyo anatoswa mazima
 
View attachment 3206619

Hiyo ndio habari mpya toka mkutano Mkuu wa CCM Taifa kuwa Dkt Emmanuel Nchimbi ndio Mgombea mwezi wa CCM katika Uchaguzi Mkuu Ujao.

Mabadiliko haya yatakuwa na effect kuanzia mwezi July baada ya Bunge kuvunjwa hivyo Dkt Mpango na Dkt Emmanuel Nchimbi wataendelea katika nafasi zao hizo hizo.
===

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni mgombea urais, Samia Suluhu Hassan amempendekeza Katibu Mkuu wa chama hicho, Dkt. Emmanuel Nchimbi kuwa mgombea mwenza katika uchaguzi utakaofanyika Oktoba 2025.

Dkt. Nchimbi aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM Januari 15, 2024 katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya chama hicho kilichofanyikia Unguja, visiwani Zanzibar.

Dkt. Nchimbi alichukua nafasi iliyoachwa wazi na Daniel Chongolo aliyejiuzulu Novemba 29, 2023.

Rais Samia amempendekeza Dk Nchimbi leo Jumapili, Januari 19, 2025 katika mkutano mkuu maalumu jijini Dodoma.
 
Attachments

  • IMG_4035.JPG
    IMG_4035.JPG
    35.5 KB · Views: 2
Angempendekeza mzanzibar ili pale Ikulu wapitishe mswada kuwa Tanganyika iwe Zanzibar
 
Back
Top Bottom