Hawa wote wameingia kwenye historia ya fedheha ambayo pengine haitatokea tena milele katika taifa hili.Tangu tupate Uhuru haijawahi kutokea Mkuu wa Majeshi (CDF) kulihutubia Taifa kwa njia yo yote ile. Jambo lililo wastaajabisha wengi ni pale CDF General Mkunda alipojitokeza mbele ya vyombo vya habari na kumuunga mkono IGP katika harakati za kuua wananchi kwa kisingizio cha kuzima maandamano ya wananchi kupinga uchaguzi mkuu haramu.
Tunafahamu kuwa JWTZ ndiyo chombo pekee chenye mamlaka ya kulinda nchi dhidi ya uvamizi kutoka nje na pia kuwalinda wananchi pamoja na rasilimali za nchi. Alipojitokeza mbele ya vyombo vya habari wananchi walitegemea angewakemea polisi kuacha mara moja operation yao ya kuua raia na kuwaamuru warudi katika vituo vyao. Kitendo cha General Mkunda kuungana na IGP Wambura kiliwahamasisha mapolisi waovu kuendelea kuua raia wasio na hatia hadi majumbani mwao.
Mauaji ya raia yangeweza kuzuilika kwa polisi kutumia mabomu ya machozi, risasi za mpira na maji ya kuwasha pale ambapo uvunjifu wa amani ungejitokeza na JWTZ kuwaongoza waandamanaji sehemu salama.
Kufuatia kadhia hii General Mkunda hastahili kuendelea kuwa CDF na anatakiwa ajiuzuru mara moja.
Napendekeza kila mmoja wao apewe kiasi chake stahiki cha fedheha ndani ya historia hiyo:
1. Emmanuel Nchimbi
2. Stephen Wasira
3. Jakaya Kikwete
3 Mkunda (sijui jina kamili ni nani)
4. Camillius Wambura
5. Jumanne Mulilo
6. Kundi la watu kama akina Mizengo Pinda, Adam Kimbisa, Kiongozi wa BAKWATA
7. Mchengerwa (kwa kazi yake ya serikali za mitaa)
8. Kailima na Mwenyekiti wake wa Tume ya Uchafuzi
9. Hamza Johari
Hawa wote, mbali ya kutambuliwa kwa historia yao ya mauaji ya waTanzania, wote ni muhimu wafikishwe mbele ya mahakama kujibu mashtaka juu ya maovu yao.
Samia Suluhu Hassan na wazanzibar aliowatumia kuua waTanzania, wao watakuwa na historia yao pekee mbali ya kundi hilo hapo juu