Bado hujatuonesha uhusiano wa kuanguka kwao na wao Kugombea uenyekiti TaifaNimeamini kweli kuwa yeyote atakaye jaribu na aliyejaribu kuchukua fomu ya kugombea uwenyekiti taifa kuna figisu lazima afanyiwe.
Na naamini yale maneno ya sumaye kuwa sababu ni kutangaza nia ya kugombea kiti ndio maana kura za hapana zilimiminika kama njugu.
Kwahiyo ndugu zangu yeyote atakayejaribu kusimama na mbowe ni pandikizi si ndio?
Aya bhana uwanja ni wenu pambaneni.
Mkuu kama kilishatoka basi, maana katiba za vyama zinapelekwa kwa msajili.msiishi kwa historia.hata katiba ya ccm haina ukomo Wa nafasi ya mwenyekiti Mkuu.Unajua ni kipi kilifanya hicho kifungu cha ukomo kisiwepo? Sikosei ninaposema muda wa Mbowe kukaa madarakani umepita. Uliza upate ukweli kwanini hicho kifungu cha ukomo hakipo. Kwa taarifa yako hicho kifungu kilitolewa kinyemela bila ridhaa ya vikao halali. Amka boss, usitoe nafasi ya siasa chafu kuendelea cdm.
Kama membe Leo anaandamwa Na bashiru kisa kutaka kumpinga magu hivi vyama basi tu.Tafsiri ya wasaliti kulingana na Kamusi ya Chadema;
Msaliti= " Mwanachama yeyote anayetaka kuchukua nafasi ya Mbowe kama mwenyekiti"
Saws nakubaliana Na mtazamo wako, lakini haki ya kutogombea ni ya MTU mwenyewe.kama katiba yao haina ukomo shida ni nin kwa mbowe akiamua kugombea? Jambo La msingi kila mwanachama aruhusiwe kuchukua fomu ili wanachadema waamue Siku ya kura.mbona lipumba hadi Leo ni mwenyekiti Wa cuf toka 1995, vipi mrema? VIP mbatiaMkuu hata wabunge kwenye katiba pendekezwa tuligoma wao kukaa zaidi ya miaka kumi, tena tulienda mbali zaidi kuwa iwapo mbunge atashindwa kutekeleza wajibu wake, apigwe chini hata kabla ya muda wake wa miaka mitano kuisha. Ila maoni yale yakachakachuliwa. Ni hivi kaka, kiongozi kukaa madarakani zaidi ya miaka kumi ni uhuni kama uhuni mwingine. Hapa haijalishi Utetezi wowote ule. Na mara nyingi kiongozi yoyote akikaa zaidi ya miaka kumi huanza kuchezea box la kura na figisu zisizo na aibu.
Hoja ya msingi sana hii.
Kushiriki uchaguzi ni haki ya kikatiba ya kila mwanachadema na kila mwanachama anapokuwa karibu na wanachama wa vyama vingine siyo pandikizi wala msaliti.
Tunaposhangilia ushindi tukumbuke kutokuwapaka mavi wagombea wengi kwa hoja za kitoto za pandikizi la chama fulani.
Kama wameshindwa kwa uhalali tuwatie moyo na kuwaunganisha ili wasilete migogoro ya ndani kwa ndani.
Ni muhimu sana kuwa na wanachama wanaoheshimiana na kuaminiana vinginevyo kinapoteza hadhi ya kuwa chama na kugeuka kuwa genge la wahuni tu.
Mwakani kijani tupu, wakurugenzi makada wataambiwa wakishatoa fomu kwa wagombea Wa ccm, wafunge ofisi wasafiri wiki nzima.Hamsusii uchaguzi Mkuu?
Kwanini isiwe UENYEKITI?
Unajua ni kipi kilifanya hicho kifungu cha ukomo kisiwepo? Sikosei ninaposema muda wa Mbowe kukaa madarakani umepita. Uliza upate ukweli kwanini hicho kifungu cha ukomo hakipo. Kwa taarifa yako hicho kifungu kilitolewa kinyemela bila ridhaa ya vikao halali. Amka boss, usitoe nafasi ya siasa chafu kuendelea cdm.
Huo utetezi wa kwamba cdm inamuhitaji sana Mbowe wakati huu hata hauniingii akilini, akifa kesho basi jumanne asubuhi chama kinakufa? Siko na ccm kabisa kuhusu nafasi ya Mbowe, huenda ccm wanataka Mbowe aondoke kwa sababu zao, na mimi nina sababu zangu hata kama wote tumetaka hilo sasa. Mbowe ajilaumu mwenyewe kushindwa kuandaa succesion plan, kwani alipaswa kujua hiyo ni taasisi. Chama kinachomtegemea mtu mmoja kuwaongoza na sio mifumo ya uongozi, hicho sio chama bali kundi la wajanja linalofanya siasa. Naamini kwenye cdm taasisi na sio kwa cdm mtu.
Alipaswa kuacha nafsi hiyo wazi kwa mwanacdm halisi. Nijuavyo mimi watu hushawishiwa kuchukua nafasi, na watu hao wapo ndani ya cdm. 2010 Slaa hakuwa amejiandaa kugombea urais, bali alishawishiwa. Hata sasa hilo lilipaswa kufanyika.
Ungesimamia hoja hii, hata mimi ningekuunga mkono bila kusita.
Hiyo ya miaka 15 ni 'dhana' tu na wala sio 'nadharia'.
Sasa tuwasisitizie CHADEMA wahakikishe uchaguzi uwe wa haki, kura zote zihesabiwe kwa utaratibu utakaohakikisha mizengwe haikufanyika.
Atakayeibuka mshindi apewe ushirikiano na visizuke tena visababu vingine pembeni.
..cdm mnatakiwa mvumiliane.
..ushindani ktk uchaguzi isichukuliwe kuwa ni uadui.
..siyo vibaya kushangilia ushindi, lakini pia mhakikishe wale wanaoshindwa mnawa-embrace na kuwatia moyo.
.....kwahiyo shida yako kubwa ni Mbowe kukaa madarakani miaka 15, na kumbe sio kazi imemshinda!, naamini CDM wanaangalia uchapakaji kazi, na sio kukaa madarakani miaka 15, na akiendelea hivi sitoshangaa akiendelea mpk miaka 20!Kama huyo Mwambe ameshindwa hiyo ni habari nzuri sana, sina imani na mtu yoyote toka ccm kupata nafasi yoyote ndani ya cdm. Bado Nyalandu, hao wanaccm 95%+ ndio waliorudi kuunga mkono juhudi, huu uchaguzi umenifurahisha sana. Ila doa langu kubwa ni kwa Mbowe kuendelea kulazimisha kuwa mwenyekiti wa cdm. Katika hilo simuelewi Mbowe wala siawaelewi kabisa cdm. Ifahamike cdm ni taasisi, iweje mtu mmoja akae madarakani zaidi ya miaka 15?
Mtu kufa ni mipango ya Mungu ukweli nikwamba Mimi naww tuko nyuma ya keyboard tunamwaga povu hata majina tunayotumia humu ni fake changamoto wanazokutana nazo wale jamaa Sisi nikubwa ambazo pengine Sisi hatujui kwa undani wanafunguliwa mikesi mingine yakipuuzi tu Mimi naww tunakula ugali na familia zetu! nisaidie kujua kwanini CUF...NCCR zimekufa! ni hivi mkuu Mbowe ataondoka atakuja Lisu maisha yataenda ikiwa unaSupport mageuzi tuwe pamoja hebu niambie ingekuwaje Waitara angekuwa mwenyekiti wa cdm kwenye vyama vya upinzani mamluki na watumikia tumbo ni wengi kuliko inavyofikiriwa angalia kila mahali wenyewe wanakwambia wanaunga juhudi na haya utayasikia vyema kuanzia January so kuwa kiongozi wa upinzani sio issue yakitoto kumbuka kwa sasa Nchi yetu haishindani na cccm inashindana na dola unaweza kuelewa namaanis sha nini
.....kwahiyo shida yako kubwa ni Mbowe kukaa madarakani miaka 15, na kumbe sio kazi imemshinda!, naamini CDM wanaangalia uchapakaji kazi, na sio kukaa madarakani miaka 15, na akiendelea hivi sitoshangaa akiendelea mpk miaka 20!
Tangu lini ccm wakawashauri viongozi wazuri wa kuwaongozeni,Makapi yadhibitiwe kwa ili nipo na chadema 100% sio kufanya uchaguzi leo mwakani mtu anaunga mkono juhudi ili halikubaliki hata kidogo makapi yachujwe yote.
Saws nakubaliana Na mtazamo wako, lakini haki ya kutogombea ni ya MTU mwenyewe.kama katiba yao haina ukomo shida ni nin kwa mbowe akiamua kugombea? Jambo La msingi kila mwanachama aruhusiwe kuchukua fomu ili wanachadema waamue Siku ya kura.mbona lipumba hadi Leo ni mwenyekiti Wa cuf toka 1995, vipi mrema? VIP mbatia
Hakuna kifungi cha katiba kinafutwa bila kikao halali na signatures za wenye dhamana
Mabadiliko yoyote ya sheria yanakua enacted na msajili baada ya kuhakikisha!
Pia,kama anapendwa,sanduku liongee!
Sanduku ndio ultimate!
Au Mbowe anaiba kura?
Katiba yao inasemaje kuhusu Kiongozi aliekaa mamlakani muda mrefu !