#COVID19 CHADEMA: Chanjo ya COVID-19 iwe ya lazima

#COVID19 CHADEMA: Chanjo ya COVID-19 iwe ya lazima

Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, iweke utaratibu mzuri wa chanjo kuwa ya lazima kwa Watanzania,” amesema Mbowe.
Mheshimiwa, wewe si umeishachanja? kwanini unataka na sisi sote tuchanjwe? Au siku hizi uzima ni wa kulazimishana, kama wewe umeishajiponya kwanini ulazimishe na sisi tujikinge?

Sasa naanza kuwaelewa akina halima,Inaonekana ulitaka kwa kuwa umekosa ubunge wote mkose.

Na kama umejiridhisha kwamba chanjo ina madhara,nakuomba ukubali yakupate wewe na wenzio mliokwishachanja peke yenu.
 
Mbowe huenda ana nia nzuri lakini bahati mbaya sio watu wote wana mtazamo sawa juu ya Covid-19 achia tu hizo chanjo zake...
Nia nzuri imehamia huku badala ya kudai katiba mpya anashinikiza chanjo?
 
Ngoja nikuulize,hata ile ya polio ni hiari sio,achilia mbali pepopunda,kifaduro,kutajakwa uchache.
Zote hizo ni ipi unajaza fomu ya endapo ukipatwa na madhara hutaishtaki serikali?
 
Hivi CHADEMA wanaelewa kwamba kabla ya chanjo kuna fomu ya kusaini kukubali kuchanjwa?

Wanaelewa kwamba kuna issue nzima ya consent katika maadili ya kitabibu?

Wanaelewa kwamba kulazimisha watu wasiotaka chanjo wachanjwe ni kuvunja haki zao za kibinadamu?

 
Mbowe huenda ana nia nzuri lakini bahati mbaya sio watu wote wana mtazamo sawa juu ya Covid-19 achia tu hizo chanjo zake...

Nia nzuri ipi. Msimfanye mkubwa wenu kuwa hakosei. Taja Nchi gani chanjo hizi Ni lazima. Hakuna chanjo iliyochukua miaka 2. it’s a risky. Mimi nilichomwa toka mwezi wa nne kwa hiari. Na wengi tu ulaya huku hawataki. Afu Sijaona huku ulaya mwana upinzani anatoa hotuba za namna Hii. Mama mwema sana.
 
Zote hizo ni ipi unajaza fomu ya endapo ukipatwa na madhara hutaishtaki serikali?
Kwakuwa kwako ni kakorona hakata kutisha,ukizingatia mwili nyumba,nyungu kwa Sana,pamoja na juisi lishe.utishike tena.
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeomba huduma ya utoaji chanjo ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu, inayosababishwa na Virusi vya Corona (COVID-19), iwe ya lazima badala ya hiari kama ilivyotangazwa na Serikali...
Hapo siungi mkono hoja
 
Kwakuwa kwako ni kakorona hakata kutisha,ukizingatia mwili nyumba,nyungu kwa Sana,pamoja na juisi lishe.utishike tena.
Na ndo maana tunataka chanjo iwe hiari,mnaotishika mchanjwe.tusiotishika tuendelee na maisha.
 
Hata mimi kwa hilo Mbowe siungani nae maana hata huko ulaya ambako wameathirika chanjo siyo lazima na kuna baadhi ya wafanyakazi wa hospital wamediriki kutishia hata kuacha kazi kama watalazimishwa
 
Back
Top Bottom