Siafikiani na sera za chadema kutokana na baadhi ya sera zenyewe kutokuwa na uhalisia (huo ni mtazamo wangu kila mtu wake) ila kuna baadhi ya vipengele kama hiki najiuliza tatizo liko wapi ndipo napokuja kugundua kuna baadhi ya akili ndogo ambazo nazo zinaparamia kila mada na hata kuvuruga wenzao ambao wapo kwenye dini yao
Ni akili ndogo tu ndio itaongea pumba na kuendelea kulalamika kuhusu DP World awe mwislamu au mkristo wakati kila mmoja aliona jinsi lilivyokuwa limkataba libovu (kuna miwatu mijinga kweli)
Sasa Kupinga ule mkataba kuna Islamophobia gani, kueleza mtu atazame sera na asiangalie dini ya mtu kuna ubaya gani?, mara ngapi tunasisitizana kuwa tusizingatie dini, kabila au kanda kwenye kufanya jambo fulani je huwa tuna hiyo phobia??
Sijaona mahali alipozua taharuki au kuchochea ugomvi baina ya waislamu na wasio ni mtu mwenye upungufu wa fikra tu ndio atang'ang'ania hiyo issue na huu ujinga ndio uliokikwamisha chama cha CUF baada ya porojo za watu kukishikamanisha na dini fulani ilhali sio
Tuache pumba tuongee facts