DesertStorm
JF-Expert Member
- Nov 22, 2015
- 3,131
- 2,537
Narudia tena, pumzi inakupa kibri, wala hujui ni nani anaekufanya upumue.Kwenye Nini labda, au hiyo pumzi inatolewa na hayo mavitabu ya watu weupe? Mmelishwa hofu za kijinga kwa mambo msiyo na ushahidi nayo. Hizo hofu ndio mnataka Kila mtu aziamini. Fanya hivi, tunza hiki nilichoandika hapa, siku ukifika huko unakoaminishwa utaenda ww unayeamini hayo mavitabu, unishitakie kuwa nilikufuru.
إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا سَوَاءٌ عَلَيْهِمْ أَأَنْذَرْتَهُمْ أَمْ لَمْ تُنْذِرْهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ
2:6 Al-Baqarah
Hakika wale walio kufuru ni sawa kwao ukiwaonya au usiwaonye, hawaamini.
خَتَمَ اللَّهُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ وَعَلَىٰ سَمْعِهِمْ ۖ وَعَلَىٰ أَبْصَارِهِمْ غِشَاوَةٌ ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ
2:7 Al-Baqarah
Mwenyezi Mungu amepiga muhuri juu ya nyoyo zao na juu ya masikio yao, na juu ya macho yao pana kifuniko. Basi watapata adhabu kubwa.
وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ اتَّبِعُوا مَا أَنْزَلَ اللَّهُ قَالُوا بَلْ نَتَّبِعُ مَا أَلْفَيْنَا عَلَيْهِ آبَاءَنَا ۗ أَوَلَوْ كَانَ آبَاؤُهُمْ لَا يَعْقِلُونَ شَيْئًا وَلَا يَهْتَدُونَ
Al-Baqarah 2:170
Na wanapo ambiwa: Fuateni aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu; wao husema: Bali tutafuata tuliyo wakuta nayo baba zetu. Je, hata ikiwa baba zao walikuwa hawaelewi kitu, wala hawakuongoka?