Uchaguzi 2020 CHADEMA, kazeni buti zenu, you are almost there. Adui yuko hoi, ushindi uko wazi mno!

Uchaguzi 2020 CHADEMA, kazeni buti zenu, you are almost there. Adui yuko hoi, ushindi uko wazi mno!

Unasema?
20201005_140926.jpg
 

Attachments

  • 20201005_140736.jpg
    20201005_140736.jpg
    63.7 KB · Views: 1
Huyo kibaraka wa mabeberu akishinda mi nahama nchi
Akili zako zimeshahama,zimeshatoka nje ya mwili wako,bado wewe tu kuhama,mtahama hata na huyo bwana wenu kwa aliyoyafanya hawezi stahimili kubaki nchini
 
huo mda ulikua 2015, nadhan kama watu ni kuichoka ccm waliichoka kweli, lile vibe la kujiandikisha sio poa, upinzani ni muhimu sana ila mnachofanya kwa watanzania sio poa kabisa! yaani mlivoanza tu kusema sjui tule izo barabara, sjui tule ndege! wacha ninyamaze tu, kwanza nmefurahi sana hii flyover imekuja apa ubungo, sio kwa kusubiri kule aisee alafu mnakuja kusema kweli hazina kazi, mnachofanyia watanzania sio poa kabisa, bora mngekazia ajira, nyongeza ya mshahara na mengine mengi ambayo yalikua kero alafu muongee kwa kushawishi watu sasa sio mnapsha watu, watu wana shida nyingi kwenye haya maisha vita za mtu binafsi na mtu mwingine kiukweli tunampa pole lakini hata mm nna matatizo yangu binafsi pia sipo tayar kuskiliza matatizo mengine, but npo tayar kuskiliza utatuzi
Amini nakwambia CCM imechokwa kwelikweli. Hata unaowaona wako humo ni wale kwa maslahi binafsi ila sio kwa mapenzi ya itikadi kweli.
Nafikiri hujajua Kwa nini watanzania wamefikia hatua hata ya kusema hizo barabara si lolote si chochote!! Sababu kuu mnafanya hayo yote huku mkiumiza wengine tena wengi vibaya sana. Mbaya zaidi mnaumiza na kutesa wengi alafu ikitokea kitu kama fly-over mnakitangaza Kama mmefika mbinguni vile na hapo ndo watu wanafanya comparison na nchi nyingine ambapo Kuna nzuri na za kisasa zaidi ya hizi zenu na kuishia kuwakejeli.

Mbaya zaidi tena mnaharibu kwingine kama kwenye kilimo, biashara alafu mnataka bado msifiwe
 
ukihisi baridi KALI basi kunakaribia kucha!!
 
Laiti ungeomba CHADEMA ikiingia madarakani ishughilikie mageuzi ya kiuchumi ili kutokomeza maadui watatu (umaskini, maradhi na ujinga) maombi yako yangesikilizwa.

Kwakuwa hamjui hao ndio maadui wakubwa wa Watanzania, usingeomba uhuru wakati ni uhuru na haki waliyo nayo wataenda kupiga kura. Uhuru na haki waliyo nayo wagombea ndio wanatumia kufanya kampeni. Uhuru na haki uliyo nayo ndio umetumia kuleta bandiko hilo.

Unajitambua kweli kushabikia CHADEMA chenye viongozi wenye kila sifa ya uovu, ili wakabidhiwe nchi?
"Kila.sifa ya uovu..."!!!
Unahitaji kuombewa wewe. Hata Shetani hana kila sifa ya uovu. Hapa na pale anatenda mema hata kama ni kwa lengo la hatimaye uanguke.

Hakuna kiumbe anayeweza kuwa na kila sifa ya uovu.
 
Muda wote unamrejelea Mungu wa Israel, je sisi Watanzania hatuna Mungu? Je Mungu wa Israel ni tofauti na wa Kwako wewe Mmakonde?

Mungu ni mmoja TU, Muumba Mbingu na ardhi wanadamu, mimeo na vyote ulimwenguni. Ndiye aliyemuumba Adam, Yesu, Muhammad, mimi na wewe. So, huna haja ya Kumtaja Mungu wa wapi.

Nimeona, nikupe hili kwa upande huo; ingawa kwa upande wa hoja kisiasa upo sawa
Mungu wa Israeli amesikia kilio cha Watanzania cha miaka mingi.

Mungu wa Israel ameona mateso ya watu wake na sasa ameshuka mwenyewe kuja kutukomboa.

Mungu kampiga upofu wa fikra na ufahamu adui. Nguvu na manlaka yao siyo kitu tena. Havina msaada kwao. Haviwezi kuwaokoa na anguko kuu la kushindwa.

CHADEMA na Tundu Lissu ni zana tu za ukombozi wa nchi hii anazotumia Mungu. Lakini ukweli ni kuwa yeye mwenyewe Kristo simba wa Yuda yuko kazini anaokoa!

Adui ameshaona na amenusa kushindwa kwake. Yuko so desparate.

CCM na Magufuli ni kama simba aungurumae kumtafuta yeyote aliyekaa kihasara na mwenye hofu ili amle.

Lakini kiukweli ni kuwa, CCM na Magufuli wala siyo simba bali wanaigiza usimba.

Kama hujagundua kuwa unachosikia sio sauti ya simba, bali ni ya kumuigiza simba, basi unaweza kuanza kutimua mbio kumkimbia simba - mbuzi.

Sisi tuko serikalini. Ni wazalendo katika kambi ya adui. Tunawahakikishia kuwa adui kwa ndani ameshakwisha habari yake. Mnavyomwona kwa nje ni fabrication tu, MSIOGOPE. Songeni mbele!

Mungu yuko pamoja nanyi. Sisi huku tunawapa habari zote kwa kadiri tunavyozipata na zilivyo. Tu wadogo sana, lakini tunajua kila kitu.

Mna siku zisizozidi 23 kuanzia leo ku - revisit mikakati yenu ya ushindi. Nawahakikishia tena robo tatu (3/4) ya machinery za kidola zinawaunga mkono tukiwemo 99% ya watumishi wa umma.

Tuko upande wenu. Nasi tunahitaji kuwa huru. Tuko tayari kusaidia kumwangusha Farao wa Misri iwe kwa kutaka ama bila kutàka.

Mpango mzima uko kwenye vituo vya kupigia kura. Angazieni uko. Mikakati na nguvu zote zielekezwe huko. Ishu haiko kwenye kampeni na nyomi.

Tundu Lissu hata asipofanya kampeni, anashinda unless mshindwe kuweka mikakati thabiti kwenye vituo vya kupigia kura.

Njooni na mkakati wa kudhibiti kura za kila kituo cha kupigia kura ili kuhakikisha kuwa kura zinakuwa halisi zilezile zilizopigwa.

Hakikisheni mnaweka mawakala kila kituo, wanaapishwa kwa wakati, wanaingia vituoni na wanapata nakala ya matokeo kwa kila kituo cha kupigia kura.

Msifikiri sana kuhusu fedha kwa sababu fedha haiwezi na haijawahi kufanya kila kitu kwa mwanadamu.

Tazameni, wao wana fedha nyingi kuliko maelezo. Lakini mbona haziwapatii upendo na kila kitu wanachokihitaji? Fedha kwao imeleta uhasama na mgawanyiko kuliko kufikia lengo lao.

Wekezeni kwenye kile watu wanachohitaji. Watu wako tayari kwenda kwenye vituo kuwa mawakala wenu hata bila malipo ili mradi waufikie ukombozi wao.

Watu wamechoka. Watu hawako huru. Watu wamefungwa na wako gerezani. Watu wanahitaji kufunguliwa.

Mungu mwenyewe yuko kazini kujibu kilio cha watu.

Pokeeni heshima hii ya pekee aliyowapa Mungu kupitia mja wake Tundu Lissu ili kuwatoa watu wake kwenye utumwa wa Misri wa zaidi ya miaka 57.

Hili ndilo jukumu alilopewa Tundu Lissu.
 
kwahio ukaona lissu akiwa raisi, mbowe waziri mkuu, lema waziri wa fedha, halima mdee waziri wa afya nchi itaenda swwa?

Kwani wewe ndiye mpanga nani awe waziri mkuu, wa fedha au wa afya?

Pia wewe ndiyo mwenye vipimio kuona kama nchi inaenda sawa?

Mbona vichwa vyenu mnavitumia kwa kazi zisizo?

Ni matumizi mabovu kutumia kichwa kufugia nywele.
 
Rais Mteule Tundu Lissu akishatangazwa kuwa ndiye mshindi, ndipo wana CCM nao watakapo tambua ubaya na maudhi ya matangazo ya mgombea wao yaliyotapakaa nchi nzima. Yaani ni kama yamchoresha tu.
 
Mbinu za kutisha zinazotumika ni ishara kubwa sana kuwa wapo hohe hahe, matumizi ya wasanii wakubwa, sasa hivi watu hawaangalii ahadi kedekede za hicho chama bali mabadiliko peke yake.

Tumechoka kuahidiwa maji Safi na salama, tumechoka kuahidiwa afya bora, tumechoka kuahidiwa elimu bora, tumechoka kuahidiwa umeme kila kijiji badala ya kila kaya, tumechoka na stori za njaa.

Tanzania ilipaswa kuwa tumeachana na hayo mambo kitambo kama miaka thelasini iliyopita. Tulipaswa sasa kuangazia mambo makubwa kama VIWANDA na vinginevyo lakini kuahidiana afya, maji, elimu, chakula na umeme n dharau sana kwa WATANZANIA.

Miaka karibu 60 ya UHURU tunaahidia mambo msingi kabisa ambayo yalipaswa yameshatekelezwa miaka mingi iliyopita.

Watanzania lazima tujitafakari kwanza Ni muda wa kuachana na ushabiki.

Let's go with LISSU akifeli tupige tu spana na kwake mpaka tufike tunakotaka kwenda.
 
Back
Top Bottom