CHADEMA kukataa mualiko wa NEC wakati wanasubiri mualiko wa Rais Samia ni kichekesho

CHADEMA kukataa mualiko wa NEC wakati wanasubiri mualiko wa Rais Samia ni kichekesho

Na hilo la kujiona wao ni bora na muhimu kuliko vyama vingine vyote vya upinzani litaendelea kuwakwamisha miaka nenda rudi, kwasababu vyama vingine vitaendelea kutowapa ushirikiano katika madai yao yote. Hiki ni chama ambacho hakina political strategists kabisa; kimejaa watu wa mitulinga tu. Utadhani Jeshi la Sungusungu!
Cdm hawajioni bora, bali kila chama ni tofauti na chama kingine. Hata kutaka kuonana na rais cdm waliomba kivyao wala hawakuomba kwa niaba ya vyama vingine. Vyama vingine vikitaka vitaomba kwa muda wao. Kila mmoja ana matatizo yake na mitazamo yake.
 
Ni kwa mwenye ufinyu wa akili tu ndiyo anaweza kuandika hivi. Mpaka hapo nchi itakapoingia kwenye machafuko ya kutisha kwa UCHAFUZI wa uchaguzi ndiyo mtatia akili kichwani.
Hayo machafuko hayatatokea iwe mchana au usiku
 
NEC ni office ya CCM ,hawana la maana zaidi ya unyang'anyi wa haki za raia
 
Iko wazi Chadema na vyama vingine vilivyokataa kuhudhuria Mualiko wa NEC kwenye kutoa ripoti ya Uchaguzi wa 2020 sababu ilikuwa ni malalamiko yao juu ya wanachokiita dhuluma kwenye uchaguzi huo. WAMEKWENDA mbali zaidi hata wengine kugomea ruzuku, kugoma kupeleka majina ya wabunge wa viti maalum na kugomea chaguzi za marudio.

Kwa uwazi kabisa mtazamo wa CDM ni kuwa chaguzi za S/M 2019 na MKUU 2020 zilikuwa ni batili na walioshinda hawawatambui. Ajabu ya CHADEMA ktk hili ni uleule undumilakuwili wa "Sizitaki mbichi hizi" kwani inaonekana wako tayari kukutana na Rais Samia kwa ajili ya kufanya mjadala wa kisiasa sijui maridhiano ya kitaifa, they know much.

SWALI hapa wanataka kukutana na Rais aliyetokana na uchaguzi waliouita batili, What does that mean?. Maana yake hawatambui ushindi wa JPM/SSH mwaka 2020. Je wanataka kukutana na SAMIA yeye kama nani?. Kama ni Rais ameupata kutokana na uchaguzi upi?, je kama wanamambua hivyo kuna haja kutoutambua huo uchaguzi? It is just a logical fact!

CHADEMA katika kususia jambo bado wamefeli na wanafeli, mwaka 2015 walisusa na kutotambua Urais wa JPM na walifika mbali wakamuita Lowassa kuwa "Rais wa Mioyo ya Watanzania" (Sitaki kuongelea tena huu upuuzi wao maana huyu Rais amerudi kwao kumenoga). In the end bado walikuwa wanajipendekeza kutaka maridhiano mara kutaka kuonana na JPM ili kusikilizwa kilio chao wakati hawakumtambua kama Rais. Funny indeed

Kuna mawili ambayo CDM yanawashinda na wataendelea kuwa Ndumilakuwili mpaka kesho baada ya kuamua moja:-
1. Kama unasusa basi susa mazima ijulikane UMESUSA KIUME NA UNA MSIMAMO kisha dai tume huru KWA NGUVU ZOTE.
2.Show some respect kisha omba kukutana na RAIS ufikishe kilio chako awasikilize shida zenu.

Zaidi ya hapo ni Undumilakuwili na kuendelea kuonekana hawana msimamo . UNAMSUSIA KUKU WAKATI MAYAI YAKE YANAKUTOA MATE.

NEC ni boya tu na hawana meno unakutana nao kuongelea kitu gani, hawana uwezo wa kubadili au hata kuhoji chochote popote bali hupokea directives kutoka kwa watawala hivyo ni bora kuongea na watawala direct hata kama hao watawala wameukwaa utawala kwa njia haramu.
 
kwani mwaliko wa NEC ndio mwaliko wa Samia???

Halafu wakiambiwa Tume ya Uchaguzi sio huru wanapiga kelele tena. Hapa mleta mada anaonesha wazi kuwa Taasis ya Rais ndio ile ile ya NEC au Rais na NEC lao moja!!

Kuna kipindi najiuliza uwezo wetu wa kufikiri una walakini gani? Mleta mada hashangai hata Rais anashauri mambo kadhaa yaangaliwe. Anashindwa kujiuliza kwanini Rais (kama Rais - sio mwenyekiti wa CCM) anatoa ushauri namna mambo kadhaa yafanywe!! Kwanini Rais anaalikwa kama Rais badala ya mwenyekiti wa CCM! Je, wahudhuriaji wa hii event nao wangepata nafasi ya kuzungumza? Tuna shida sana na mamlaka ya uRais!

Mkuu, muache huyo - uelewa wake mdogo sana!!
 
Ni kwa mwenye ufinyu wa akili tu ndiyo anaweza kuandika hivi. Mpaka hapo nchi itakapoingia kwenye machafuko ya kutisha kwa UCHAFUZI wa uchaguzi ndiyo mtatia akili kichwani.
Hayo machafuko ni Chadema utopia. Tanzania ni imara na yenye amani chini ya Serikali ya CCM.
 
Unawaita Chadema wajinga wakati wewe hata watu wawili tu imeshindwa kuwaongoza,sijui kama una familia,kama unayo basi hata familia yako tu imekushinda kuiorganize.
Bwashee, hata huko kwa rais wameshaghairi asipokutana nao peke yao. Akiwaweka kwenye kundi la vyama vyote basi hawaendi!
Ujinga uliomo chadema sasa hivi hata kwa fimbo hatuwezi kuutoa.
 
Bwashee, hata huko kwa rais wameshaghairi asipokutana nao peke yao. Akiwaweka kwenye kundi la vyama vyote basi hawaendi!
Ujinga uliomo chadema sasa hivi hata kwa fimbo hatuwezi kuutoa.
Sasa nfo umeandika nini!
 
Back
Top Bottom