Ulitaka kiongozi wa kitaifa yupi aje kwenye sherehe wakati Mkt wao Taifa mmemshikilia gerezani? Ulitaka Lissu asafiri toka Ubelgiji kwa ajili tu ya kuja kwenye sherehe za uhuru? Ulitaka Mnyika aache kuhangaika na kesi ya Mbowe aje kugongesha glass na watu waliomkamata?
Kwanza Uhuru tunaosherekea sasa si uhuru wa wapinzani bali ni Uhuru wa ccm na wanachama wake lakini lakini wapinzani bado wako chini ya mkoloni mweusi!
Siku ya Uhuru mwaka 1961, ilishushwa bendera ya mkoloni ikapandishwa bendera ya taifa, Siku zote CCM imekuwa ikiamuru kushushwa kwa bendera za CHADEMA na kupandishwa zile za ccm hayo matendo yanaashiria wazi kuwa wapinzani uhuru bado hawajaupata, Hivyo hata kushiriki sherehe za uhuru ni sawa na unafiki dhidi ya nafsi zao wenyewe hivyo walichofanya nkutoshiriki sherehe hizo ni sahihi kabisa kwakuwa uhuru wa nchi yetu ccm ilishajimilikisha!