CHADEMA kweli ni shwari au ni kauli za kisiasa tu ?

Jasusi,
Mtu wa Pwani,
Naona wewe una lako jambo na kijana Mbowe. Pia naona wewe si Chadema. Kwa hiyo ushauri wako ni kama vile simba anamwambia mbuzi akae akae karibu na kichuguu.
Umeniacha mbavu sina duh!
 
Mkandara... miye nakusikia na ninakuelewa lakini ninachosema ni kuwa inapojengwa hoja basi kuwe na msingi basi. Hoja ya ukabila imejibiwa mara nyingi lakini as long as ni wachagga baadhi ya watu hawatoridhika. Ingekuwa watu hao ni wangoni sidhani kamahoja ingekuwa kali hivi.

Sijui kama umesikia jibu la Tundu Lissu. Halafu kumbuka wanaozungumziwa ni wabunge wa viti maalumu siyo uongozi mzima wa Chadema. Mimi hoja ambayo kina wangwe wangetakiwa kuitoa ni jinsi gani wabunge wa viti maalumu wanapatikana. Angeonesha ni jinsi gani mfumo huo umesababisha kuonekana kwa hali ya watu wa eneo moja kupata nafasi za viti maalum. Kudai kuwa ni ukabila sidhani kama ni sahihi kwa sababu uongozi wa juu wa Chadema si wote wachagga! Itabidi watu wale njama kubwa kweli ya kutoa nafasi hizo kwa watu wa Kilimanjaro tu.

Hofu yangu ni kuwa tutaanza kuwabagua watu kwa kuogopa. Binafsi sipendi nitendewe kwa upendeleo kwa sababu ya rangi yangu au nionewe kwa sababu ya rangi yangu. Kama nimeomba kazi kwenye kampuni ya watu weupe na hakuna mweusi hata mmoja na nikakosa nafasi hiyo, ni matumaini yangu kuwa nimeikosa kwa haki. Endapo hata hivyo itaonekana kuwa aliyechaguliwa ni mweupe na hana qualification na experience kama za kwangu na kitu pekee walichompatia ni sababu ya hiyo rangi yake then, tutazungumza suala la urangi na kuhoji mfumo wa namna hiyo. Ni rahisi kulionesha hilo kwenye mahakama ya sheria na mtu atashinda.

Nitalieleza hili wakati mwingine kwani hivi majuzi nimeshinda kesi moja ya mambo haya haya ya civil rights...

Lakini ninachoogopa mimi ni huu uwezekano wa kuona walipo wachagga zaidi ya mmoja basi kuna tatizo, tuchunguze! Akija mtu kulalamika basi lazima tuchunguze as long as wachagga wako pale. Lakini tukiwakuta wamakua wengi eneo fulani tusifikiria ni ukabila, tukiwakuwa wakurya mahali fulani tusifikirie ni ukabila, isipokuwa wachagga. Mzee kuna anti-chagga sentiments kwa muda mrefu sasa na ninakumbuka kuna mtu mmoja aliapa kabisa kuwa kama angekuwa na uwezo angewamaliza! (hiyo ilikuwa ni mara ya mwisho niliopochangia mada ya ukabila TRA).

Believe me... yawezekana watu wakawa wanaonekana na nia nzuri lakini nyuma yake kuna mambo mazito sana. Nakumbuka Hitler alianza hivi hivi kwa kuona kuwa wayahudi wanamiliki biashara nyingi (which was true in a sense) na walikuwa as a community wamefanikiwa sana tangu karne na karne. Yeye akaona kuwa matatizo ya ujerumani yanatokana na hilo hasa na akaamua kutafuta kile alichokiita "Final Solution". Alitaka kuwapunguza kwa sababu aliona ule ukabila wao ulivyoenea na kufanikiwa kwao as a community. Akienda huku anakuta myahudi akienda kule anakuta myahudi..!

Linapokuja suala la ukabila na udini, kwa upande wangu I'm very strict and focused kwani hofu yangu ni kuruhusu kutengeneza chuki ya kikabila hata isiyo na msingi.

Pamoja na hayo nakubaliana na wewe kwa asilimia mia moja kuwa endapo kuna credible reason ya kususpect ukabila basi ifanyiwe uchunguzi na ioneshwe ni nini hasa. Usivumiliwe.

Mwaka 1968 Nyerere akihutubia siku ya Uhuru wa Tanganyika aliangalia kile alichokiita "Mambo tunayopaswa kusahihisha". Mojawapo ya alivyovigusia ni "ukabila". Naomba ninukuu sehemu ya hoja yake:

 

Hoja yangu Chadema wawe na system ya kuchagua wabunge wa viti maalum sio kuteuliwa na vigogo wa Chadema au atakayetoa mchango mkubwa wa pesa mtoto wake awe mbunge imetoka kwa LUCY mtoto wa Ndesamburo , hapo ndio kwenye tatizo nimetoa mfano mzuri wa CUF na CCM wanavyowapata wabunge wa viti maalum na hakuna anayelalamika kuwa kuna ubaguzi wa kidini wala kikanda.mtoto wa JK aligombea nafasi ya kuhudhuria mkutano mkuu wa CCM mwaka jana, hakuteuliwa wala kupendekezwa. just kuhudhuria mkutano mkuu lazima ugombee ni demokrasia ya hali juu,
 
msimtafute mchawi nani chadema kuweni wepesi wa kusoma nyakati


igeni mazuri yetu sisi tuko makini sana kujua wakati gani wa kulia na wakati gani wa kucheka


wakati gani wa kuvua nguo na wakati gani wa kuvaa nguo

na nnakwambieni kula fenesi hakutaki pesa kunataka nafasi
 


Ahaa nimekupata mkuu
Mimi naongelea "Mbowe Mkama" yani yule kaka yangu kwanini wewe unaongelea mbowe yupi?

Nimeshaelewa wakuu .
 
Mwanakijiji: Hoja zako kuhusu utetezi wa wagombea wa viti maalumu zina make sense sana kitaaluma lakini, naogopa kusema, hazi-make sense kabisa kisiasa. Pengine hoja zako zinaweza kukubali miongoni mwa wafuasi na wanachama wa CHADEMA lakini sio rahisi independents na wapinzani wa CHADEMA wakashawishika. To be honest, mimi binafsi nilishakiri siku nyingi kwamba uteuzi wetu wa wabunge wa viti maalumu ni kati ya makosa ya kutisha kisiasa ambayo CHADEMA tumewahi kuyafanya. Itakuchukia miaka mingi sana kuisambaratisha hoja ya wapinzani wetu kwamba kulikuwa na upendeleo wa aina fulani katika uteuzi wa wabunge wa viti maalumu.

Tatizo langu na Mhe Wangwe katika hili ni kwamba kwa nini analitumia hili kosa kujaribu kujijenga kisiasa yeye binafsi bila kujali madhara yake kwa chama? Ninaamini, I am not sure though, hili jambo litakuwa lilishajadiliwa katika vikao vikuu ndani ya CHADEMA ambavyo Chacha ni mjumbe muhimu, na lazima kutakuwa kulishatolewa maelezo na pengine makosa yakakiriwa. Sasa kwa nini yeye analirudiarudia kila mara huku akijua kabisa kwamba utatuzi wake hauwezi kupatikana leo hadi uchaguzi mwingine ufanyike 2010?
 

Kitila ni kweli kuwa Kamati Kuu ilishalifanyia maamuzi na ndio maana likaanzishwa Baraza la Wanawake ambalo kwa 2010 watakuwa na jukumu la kupendekeza wabunge viti maalum hivyo suluhisho lilishapatikana.

Ni taarifa tuu.
 

Jambo hili, pamoja na ubest na Amani Kaboul ndo vyanzo vya imani yangu kupungua kwa Mh, Wangwe. Asante Kitila.
 

Chinga ni mtu wetu. Alishaanza kufanya propaganda kuhusu hili. Lakini hebu vuteni kumbukumbu mfuatilie maandiko yangu. Nilisema hapa miezi mingi kabla kuwa Rostam Aziz kumtumia Chacha Wangwe kuibomoa CHADEMA kulipa kisasi cha kuitwa fisadi. Hapa watu mkasema naandika udaku na uwongo. Sasa si mnaona Mtanzania na Rai wanavyofanya kazi yao kwa uratibu wa Rostam? Sasa kama kuna watu mnapenda chama cha siasa cha upinzani. Si wakati wa kuwaonyooshea kidole wakina Mbowe, Slaa, Zitto- ni wakati wa kuwasaidia dhidi ya mafisadi kama milivyofanya wakati Mama Killango na Mwakyembe waliposhambuliwa. Nasikitika kwamba wote mmeingia mtego katika suala ambalo nilishawaonya hapa miezi mingi kabla. Kama suala ni ukilimanjaro, mbona vinara wa kambi ya Chacha Ni mjumbe wa Kamati kuu akiwakilisha pwani bwana Mziray na Mwenyekiti wa Mwanza Bwana Lyimo? Kama hoja ni ukabila kwanini Chacha Wangwe hakuanza kuwapinga hao wenzake? Badala yake anawapinga wakina Balozi Ngaiza, Profesa Baregu ndani ya kikao? Kwa kadiri ya taarifa ambazo chacha amezitoa kwa Ballile ni kuwa ndani ya kikao alimnyamazisha Profesa Baregu kwa kumwamba "Nyamaza, we muhaya tu!"na profesa wa watu akanyamaza

PM
 
Kitila ni kweli kuwa Kamati Kuu ilishalifanyia maamuzi na ndio maana likaanzishwa Baraza la Wanawake ambalo kwa 2010 watakuwa na jukumu la kupendekeza wabunge viti maalum hivyo suluhisho lilishapatikana.

Ni taarifa tuu.

Asha is back!

Nimepitwa na mengi.

Achaeni na huyo Chacha Wangwe. Suala la viti maalumu lilishatolewa maamuzi kwenye chama chetu. Tulitafakari faida na mapungufu yaliyokuwepo. Ilijadiliwa kamati kuu, baraza kuu na hatimaye mkutano mkuu tarehe 13 Agosti 2006. Mimi nilikuwepo nikitokea Zanzibar. Huyu mwanaume na misuli yake hakuchangia hoja yoyote wakati huo kuhusu hili ingawa alikuwa mjumbe kama mbunge na mwenyekiti wa Mkoa wa Mara. Chama kikafunga mjadala. Kikabadili Katiba ya chama na kuunda Baraza la Wanawake, ndani ya Katiba ya Baraza la Wanawake ikatajwa kwamba ni wanawake wenyewe ndio watakaopendekeza majina ya wabunge wa viti maalum. Sasa mwaka 2008 mwanaume anaibuka anasema kama vile ni hoja mpya, anakosa uwajibikaji wa pamoja, anajivua nguo mwenyewe. Anachafua chama chake. Huyu jamaaa inafaa mzee wa Maswali magumu amwanike kwa jinsi alivyo. Halafu anaibuka na kusema uwongo kuwa ruzuku haisambazwi. Mbona kule kwetu Zanzibar viongozi wa wilaya wameniambia kuwa tunapokea pamoja na kuwa tulipata kura chini ya 500 mwaka 2005? Huyu chacha ana nia gani?

Halafu nimeelezwa yote aliyoyafanya kikao ikiwemo kumtukuna tusi la nguoni Mama Chiku Abwao mbele ya kikao(siwezi hata kusema hapa alichokisema. mama wa watu akalia mbele ya Kamati Kuu.

Yani, wangenipa mimi ujumbe wa kamati kuu kwa kweli watu kama hawa ni wa kufukuza chama kabisa. Leo, tunawalaumu CCM kwa kulindana na kushindwa kuchukua hatua kwa mafisadi. Lakini tunawalaumu uongozi wa CHADEMA kwa kupiga kura ya kutokuwa na imani na kiongozi asiye na nidhamu. Sasa mlitaka walindani kama CCM?

Kwa kweli inakera jamani.
 
Kitila umesema kitu muhimu na Mpaka Kieleweke ameligusia.

a. Kama utaratibu au mfumo wa kuchagua wabunge wa viti maalumu haukuwa wazi na ulitokana na maelekezo au makubaliano tu ya hewani, Chadema walipaswa kukiri upungufu huo na kusema jambo hilo wameliangalia na wamegundua kosa lililofanyika, na wameamua kuanzia uchaguzi ujao hili na lile litafanyika. Unless kama wako tayari kuwataka wabunge hawa wa viti maalumu wajiuzulu ili wapate nafasi ya wabunge wapya.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
NA
WANANCHI WA TANZANIA

KUSIMAMISHWA KWA MHESHIMIWA CHACHA ZAKAYO WANGWE (MB.) KUWA KAIMU MAKAMU MWENYEKITI WA TAIFA (BARA) WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO

Ndugu wanahabari na wananchi wenzangu,

Tarehe 28 Juni 2008 Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo katika kikao chake cha kawaida kilimsimamisha Mheshimiwa Chacha Zakayo Wangwe kama Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Taifa (Bara) wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa kumpigia kura ya siri ya kutokuwa na imani naye. Huu ni uamuzi mzito na ambao haujawahi kufanywa katika historia ya miaka 16 ya CHADEMA. Tunapenda kuwafahamisha wananchi wetu kwamba uamuzi huu mzito ulichukuliwa baada ya mjadala na tafakuri ya muda mrefu. Kamati Kuu ya chama chetu ilifikia hatua hiyo dhidi ya baada ya kuridhika na ushahidi kwamba Mh. Chacha Wangwe amekiuka maadili ya uongozi na hivyo kupoteza sifa mahsusi za kuendelea kuwa kiongozi wa kitaifa wa CHADEMA kwa sababu zifuatazo:

1. Amekuwa akijihusisha na/au kushiriki katika vikundi na/au vitendo vya uchonganishi na/au kuzua migogoro ndani ya uongozi wa chama na/au wanachama wake.

Mheshimiwa Chacha Wangwe amejihusisha na/au kushirikiana na kikundi cha waliokuwa viongozi wa chama wa Mkoa wa Dar es Salaam ambao walifutwa uongozi na vikao halali vya chama na kwa kufuata Katiba na Kanuni za chama. Kujihusisha na/au kushiriki huko ni pamoja na kuandaa, kufadhili na kushiriki katika mikutano ya siri kwa lengo la kuendeleza migogoro na hujuma kwa chama. Mikutano hii ilifanyika Ndugumbi, Dar es Salaam na pia Mwanza na ilimshirikisha pia Dr. Amani Walid Kabourou aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Taifa (Bara) kabla hajahamia Chama cha Mapinduzi mara tu baada ya kushindwa kutetea kiti chake cha ubunge katika Jimbo la Kigoma Mjini. Kitendo cha kuandaa, kushiriki na/au kufadhili mikutano ya siri ya watu ambao wamechukuliwa hatua za kinidhamu na vikao halali vya chama na/au ambao wamekihama chama baada ya kupoteza ridhaa ya kuwaongoza wananchi kina tafisiri moja tu ya msingi: Kuendeleza migogoro na/au hujuma dhidi ya chama kwa lengo la kukidhoofisha na kukifanya kishindwe kuendeleza vita kubwa dhidi ya ufisadi uliojikita ndani ya Serikali na CCM ambayo imekipatia chama chetu sifa kubwa na uhalali kwa watanzania. Vitendo hivi vinapingana moja kwa moja na maadili ya viongozi wa chama kama yalivyoelezwa katika Sura ya Kumi ya Katiba, Kanuni, Maadili na Itifaki za CHADEMA.
2. Amekuwa akitoa tuhuma nzito lakini zisizokuwa na msingi dhidi ya viongozi wenzake wa kitaifa na watendaji wa chama pasipo kupitia vikao halali na wala kuzingatia taratibu za chama

Mheshimiwa Chacha Zakayo Wangwe aidha moja kwa moja ama kwa kuwatumia viongozi na/au wanachama walioadhibiwa na vikao halali vya chama amekuwa akiwatuhumu viongozi na watendaji wa chama kwa mambo ya uzushi na yasiyokuwa na ukweli na/au msingi wowote. Yeye mwenyewe amekuwa akisambaza uzushi kwamba kuna ufujaji na/au matumizi mabaya ya fedha za chama ambao amekuwa akidai unafanywa na viongozi wa kitaifa hususan Mwenyekiti wa chama Taifa na Katibu Mkuu na/au watendaji wa Makao Makuu ya chama. Aidha Mh. Chacha Wangwe amekuwa akisambaza uzushi kwamba viongozi wenzake wa kitaifa na watendaji Makao Makuu wamekuwa wakikataa ruzuku ya chama kupelekwa mikoani na wilayani nabadala yake wamekuwa wakiitumia ruzuku hiyo kwa shughuli za Makao Makuu na/au kwa manufaa yao binafsi. Uzushi huu umetolewa licha ya Kamati Kuu ya chama ambayo Mh. Chacha Wangwe alikuwa ni mjumbe kupokea na kupitisha taarifa zote zinazohusiana na mapato na matumizi ya fedha za chama na licha ya chama kutoa ruzuku ya vifaa na/au fedha taslimu tangu mwaka 2006 kabla hata ya yeye kuchaguliwa kuwa Kaimu Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA tarehe 17 Desemba mwaka 2007. Aidha Mh. Chacha Wangwe amesambaza uzushi huu licha ya kufahamu fika kwamba si yeye mwenyewe, wala si Makamu Mwenyekiti Taifa (Visiwani), wala si Mwenyekiti Taifa wala si Katibu Mkuu wala manaibu Makatibu Wakuu wote wa chama ambao wamepokea hata senti moja ya fedha za chama kama posho au mishahara. Tuhuma hizi za uzushi na uwongo juu ya kuwepo ufujaji na/au matumizi mabaya ya fedha za chama zina lengo moja tu: Kuwapaka matope viongozo wa chama wa kitaifa na watendaji wa ngazi za juu wa chama kwa lengo la kudhoofisha jitihada za chama kujijenga kwa wananchi na kuendeleza vita dhidi ya ufisadi ambayo imekipatia chama na viongozi wake umaarufu miongoni mwa wananchi wa Tanzania.

3. Amekuwa akikashifu chama, viongozi na watendaji wake bila kutofautisha kashfa na ukosoaji wa kisiasa na/au wa kiutendaji

Mheshimiwa Chacha Wangwe yeye mwenyewe na/au kwa kutumia wanachama na/au viongozi waliochukuliwa hatua za kinidhamu na vikao halali vya chama amekuwa akitoa kashfa dhidi ya chama, viongozi wake na/au watendaji wake. Bila ya kujali ushahidi uliopo hadharani wala maamuzi ya vikao vya chama ambavyo yeye mwenyewe alishiriki kuyafikia, Mh. Wangwe amekuwa akikituhumu chama, viongozi wenzake wa kitaifa na watendaji wake wa ngazi za juu kwa ukabila na/au udini. Licha ya ushahidi wa wazi kwamba viongozi wa ngazi za juu akiwemo yeye mwenyewe wametoka sehemu mbali mbali za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Chacha Wangwe ameendelea kutuhumu kwamba kuna upendeleo kwa Wachagga na/au watu wa kaskazini ya Tanzania. Kivuli pekee cha tuhuma hizi potofu ni madai ya uwongo kwamba Wabunge watano kati ya sita wa Viti Maalumu wa CHADEMA katika Bunge la Jamhuri ni Wachagga. Kama wananchi wanavyofahamu, Wabunge Wachagga ni watatu tu na wengine ni Mzanzibari mmoja, Mpare mmoja na Muha mmoja. Aidha Mh. Chacha Wangwe anafahamu kwamba kati ya wajumbe thelathini na sita wa Kamati Kuu ya Chama kuna Wachagga watano tu sawa na wajumbe wa Mkoa wa Kigoma! Aidha Mh. Wangwe anafahamu fika kwamba kati ya wakurugenzi na watendaji wa ngazi za juu wa Makao Makuu wapatao zaidi ya ishirini, Wachagga wako watatu tu. Kwa msingi huo, lengo la kashfa za ukabila ndani ya chama zina lengo moja tu: kuwapaka matope viongozi na watendaji wa ngazi za juu wa chama kwa nia ya kuwadhoofisha na kuwapunguzia nguvu ya kuendeleza mapambano dhidi ya ufisadi ndani ya serikali na CCM.

4. Kuvujisha siri za vikao halali vya chama kwa watu wanaotaka kuhujumu chama

Mheshimiwa Chacha Zakayo Wangwe amehusishwa moja kwa moja na kosa la kutoa siri za vikao vya vya ndani vya chama. Kwa mfano, Mh. Wangwe ametoa siri na/au nyaraka za vikao vya Kamati ya Wazee wa Chama vilivyokutana kujadili tuhuma, uzushi na kashfa zake dhidi ya Mwenyekiti wa Taifa, Katibu Mkuu na Sekretariat ya Kamati Kuu ya Chama kwa watu ambao nao wamechapisha kwa kuzipotosha siri na/au nyaraka hizo katika vyombo vya habari vinavyomilikiwa na watu wanaokabiliwa na tuhuma za kuhusika na ufisadi mkubwa wa Richmond na EPA. Vile vile Mh. Wangwe ametoa siri na/au nyaraka hizo kwa kikundi cha wanachama na/au viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam waliofukuzwa uongozi na vikao halali vya chama. Lengo la kuvujisha na/au kupotosha nyaraka na/au taarifa za vikao vya ndani vya chama ni kuendeleza migogoro yenye lengo la kukidhoofisha chama na kukifanya kiache mapambano dhidi ya ufisadi ndani ya serikali na CCM.

Ndugu wananchi na wanahabari,

Kamati Kuu ya CHADEMA haikufikia uamuzi huu mzito kwa haraka na/au bila kufikiria kwa kina madhara yake kwa chama na kwa taifa letu. Kamati Kuu imefikia uamuzi huu baada ya jitihada mbali mbali za kumsaidia Mh. Chacha Zakayo Wangwe kujisahihisha na kujirudi kushindikana kabisa. Jitihada hizi mbali mbali ni kama vile:

a. Vikao mbali mbali na vya muda kati yake mwenyewe, Mwenyekiti Taifa na Katibu Mkuu kujadili tofauti na/au migongano kati yao na/au ndani ya chama;

b. Kusuluhishwa na Kamati ya Wazee wa Chama ambapo Mh. Wangwe alitakiwa kuandika maandishi kwamba ataacha vitendo vyake dhidi ya chama, viongozi wa kitaifa na watendaji wa chama;

c. Kamati Kuu ya chama kumuonya kuacha vitendo vyake hivyo dhidi ya chama;

d. Baada ya jitihada zote hizi kushindikana, Kamati Kuu ilimsihi kujiuzulu kwa hiari yake yeye mwenyewe na hivyo kujiepusha na adha ya kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye na kusimamishwa na Kamati Kuu.

Kwa vitendo na matukio yote haya, Kamati Kuu ya CHADEMA imejikuta haina njia yoyote ile ya kuepuka mgogoro mkubwa zaidi na usio na maana au msingi zaidi ya kumchukulia hatua za kinidhamu Mh. Chacha Zakayo Wangwe. Kwa matendo haya ni wazi Mh. Chacha Zakayo Wangwe amepoteza sifa mahsusi za kuendelea kushikilia dhamana kubwa ya uongozi ambayo vikao halali vya chama vilimpatia. Kamati Kuu imelazimika kutumia mamlaka yake ya kikatiba ya kumsimamisha uongozi wa kitaifa Mh. Wangwe kwa kumpigia kura ya siri ya kutokuwa na imani naye. Azimio la kumsimamisha Mh. Wangwe kuwa Kaimu Makamu Mwenyekiti Taifa (Bara) liliungwa mkono na wajumbe ishirini na nne kati ya thelathini na moja waliohudhuria na kushiriki katika kikao cha Kamati Kuu. Idadi hii ni zaidi ya theluthi mbili ya kura za wajumbe wa Kamati Kuu inayohitajika kikatiba ili kumsimamisha uongozi kiongozi yeyote wa kitaifa kama alivyokuwa Mh. Chacha Zakayo Wangwe. Kamati Kuu imechukua hatua hii ngumu na nzito ili kukiokoa chama kutokana na migogoro ambayo imesambaratisha vyama vingine vya siasa hapa nchini.

Asanteni sana





-----------------------------------------------
Freeman A. Mbowe
MWENYEKITI
 

talk about utaratibu. ulikuwepo sana tu. Walichukua fomu wilayani. Wakawasilisha. Zikapitishwa mkoani. Kila mkoa ukaleta majina. Then kamati kuu ikatengeneza vigezo vya elimu, uzoefu katika chama, kugombea, mchango kabla ya uchaguzi etc. Then ikaundwwa kamati ya wazee kufanya mchujo wa fomu bila kuwahoji wagombea coz walikuwa all over the country. Then viongozi wakuu wa chama wakaachiwa. Sasa huo ni utaratibu wa wakati huo na kila mtu aliujua. Ulikuwa na ubora wake, thats y the party got good wabunge wa viti maalum, michango yao inaonekana bungeni. This was a good approach by then given that viti vilikuwa vichache.

2010 CHADEMA itakuwa na viti vingi, inaweza kugawa kila mkoa wanawake wakaachiwa wenyewe washindane! Sasa huku ni kukua kwa chama na kubadilika kwa mifumo yake as a signal of growth. Sasa badala ya kuchambua, watu walia viti maalum viti maalum. Hebu mtu aniambie hapa. Katika ile orodha ya wabunge iliyopelewa tume 2005 ambayo ndiyo iliyotumika kutangaza hao ambao sita waliongoza wa kwanza. Nani ulitaka awepo kwa ubora wake ameachwa?

Au ni kelele za vyura tu, 'changu, changu, changu' ukisogea bwawani, Chura kimyaaa! Ukimuuliza chako nini, kipi, chura kimya!

Jiulize, haya yalifanyika 2005-2006; mjadala ukaisha, vipi leo Chacha ayafanye kama vile yameendelea leo. Ana ajenda gani baba huyu?

Asha
 

FDR Jr.

Umefikishwa nyumbani kwako. Haya endelea kurebuka kimdembwedo.

Nani kakudanganya kuwa Chacha alianikwa kwenye Mkutano wa Hadhara? Ilikuwa ni Press Conference. Baada ya hapo ilifanyika Public Rally, chacha hakutokea na jina lake halikutajwa kabisa nini kuanikwa.

Talk abou Tundu Lissu; that was mkurugenzi wa Sheria wa Chama, alizungumza mbowe mwenyekiti wa chama yeye akatoa tu ufafanuzi. Halafu unazungumzia makamu mwenyekiti kuanikwa, is he the makamu mwenyekiti wakati ameshang'olewa?

Yeye anazungumzzwa tu kama mwanachama mwingine yoyote.

Hebu kasome Sheria kuhusu Viti Maaluim huko, haiwezekani uteuzi ukafanyika kwa kufuata maeneo ambayo chama kimeshinda kwa kuwa uteuzi kisheria majina yanapaswa yawe tume siku 30 kabla ya tarehe ya upigwaji kura.

Asha
 

Hivi kwani CCM mlikosa wanawake mpaka wabunge wenu wengi wa viti maalum ni wachaga kuliko makabila mengine? Ama Kikwete alikosa mawaziri kwenye baraza lake lililopita mpaka akateua wengi wa Kilimanjaro kuliko makabila mengine?

Hivi CHADEMA ilikosa makabila mengine mpaka ikateua wasukuma wengi zaidi katika wakurugenzi na maofisa wake waandamizi katika makao makuu ya chama?

Hivi Mbowe alikosa makabila mengine mpaka akateua wahaya wawili Profesa Baregu na Balozi Ngaiza katika nafasi zake za kuteua wajumbe wa kamati kuu?

Ukabila, ukabila ukukabila. Hata mie Asha leo nikiolewa na Mmakonde mtanivua ungazija wangu kama mlivyomfanyia Maulidah Anna Komu- mlaniwe wanaume nyie.

This is male chauvisism of the highest order. Shame on you Mtanzania

Asha
 
The Citizen (Dar es Salaam)

3 July 2008
Posted to the web 3 July 2008

Joas Kaijage

Kagera Region members of the Chadema national governing council have challenged the recent suspension of party vice-chairman Chacha Wangwe which was approved by the party's national executive committee.

The members, who vowed to vote against the decision during the forthcoming meeting of the council, said the suspension of Mr Wangwe was a result of deep-rooted problems among the party's top brass which should first get cleared instead of "victimising the critics within the leadership".

A governing council member who requested for anonymity said the suspension of Mr Wangwe was a result of machinations of some individuals "who were not ready to see any of the party's national leadership positions held by members hailing from regions other northern part of the country".

He said such ideologies were the very reasons behind the defection of the party's former vice-chairman, Dr Walid Amani Kaborou, who shifted to CCM, paving the way for Mr Wangwe to replace him.

"Clear opposition by the party's top leadership to Mr Wangwe's election was a sign that they were not ready to work with other than individuals from the northern regions," the governing council member underlined. Without giving figures, he said that the nomination of women MPs for the special seats slots was conducted with bias whereby those elected originated from the northern regions.

He said that is why during Mr Wangwe's election, members from other regions opted to use the popular slogan "people's power" to fight the stereotyped northern party dominance entertained by the top brass. However, he said together with members from the rest of the regions, Kagera council members were prepared to fight tooth and nail to ensure democracy within the party was nurtured, adding that leadership cannot be imposed on Chadema members.

"You know this is costing our party a lot because the defection of Dr Kaborou for instance led our party to lose many councillors to CCM," the concerned activist noted. Dr Kaborou was Kigoma Urban MP for years before crossing over to CCM. The party won a majority of councillors in the town council, holding the Kigoma urban mayorship for two five-year terms.

If the party calls governing council members for a meeting to endorse the suspension of Mr Wangwe, the Kagera group vows to ensure that the meeting was attended by eligible members "so that democracy and people's power take their right course," he further stated. "If Mr Edwin Mtei and other founder members believe that the party's top leadership should be dominated by people from their tribe they were no different from what Robert Mugabe was doing," they said.

It was high time this group was reminded that democracy starts from bottom to the top and not otherwise, they quipped. The members charged that the leadership's failure to support party activities at regional levels owes to lack of transparency as financial affairs were handled by a small group of people.

"Party members knew nothing about what friends from inside and outside the country had donated to support their party," the Chadema stalwart observed. Kagera is represented by three members in the national governing council, two of whom stay in the region and one resides in Dar es Salaam.
 

Uzuri wa JF watu wana macho na masikio. Kama ulichoandika kina make sense wana JF watakuwa wamekuelewa, vinginevyo mawazo kama hayo ni kama junks na yanaishia kwenye jalala la takataka.
 

Mkamap,

Kwa sababu inawezekana hawana daftari la hela hawa.

Lingekuwepo kusingekuwa na hearsay za nimekupa hujanipa.

Wakati wanaanza tu kubishana kuhusu hela wangeombana daftari la hesabu huko huko kwenye vikao, na wala haya yasingekuwa makubwa hivi.

Au waweka hazina ni wezi, wana doctor daftari. Au ma auditors na accountants wao ni mafisadi.

Halafu ume raise pointi ya nguvu, kuhusu kwa nini Tundu Lissu hakusema habari ya lake 4, laki 2, laki 1 kutegemeana na viti. Kasema laki moja tu. Kwa nini statement zake zitofautiane na za Zitto (Mh.)

Halafu kingine cha kushangaza, siku wanahojiwa na Mwanakijiji, Lissu kasema wanapata ruzuku ya milioni 59, Wangwe kasema wanapata milioni 66.

Huoni hawa watu inawezekana hawana daftari hawa?

Na hiki ninachokisema kwamba inawezekana hawana daftari la wazi hii ni miaka miwili iliyopita ndio kuna utata. Kabla ya 2006 hakuna utata: Lissu kasema wameanza 2006 kuanika daftari.

Kabla ya 2006 hesabu zilikuwa zinatunzwa wapi, nyumbani kwa Mwenyekiti?
 

Zitto,


  1. Kabla ya uchaguzi kwani CHADEMA ilikuwa inaendeshwaje?
  2. Matatizo ya pesa hayakuanzia hapa maana kama ukiangalia kwenye uchaguzi 2005, Mbowe alitumia zaidi ya 60% ya pesa za chama kwa ajili ya helikopta, wakati wagombea ubunge sijui walipewa nini, je hii sio moja ya sababu za Dr. Kaborou kuondoka CHADEMA?
  3. Suala la kopta limepingwa sana na Wangwe, je hamuoni kuwa ana point hapa?
  4. Hizo pesa za rusuku zinazogawiwa kutokana na wingi wa wanachama, je hiki sio kigezo dhahiri cha kupendelea maeneo husika yenye wanachama wengi (i.e. Kigoma, Kilimanjaro, & Dar), kama vile CCM walivyoweka kigezo cha idadi ya wabunge ili kujinufaisha?
Kuna haja ya kuangalia kwa undani madai ya Bw. Wangwe, ingawa inaelekea CHADEMA-Mbowe, mnamdharau either kwa sababu ya elimu yake ndogo au uwezo weke mdogo wa kuweka mada kitaalamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…