CHADEMA mna mikakati gani serious ya kushinda uchaguzi 2020?

CHADEMA mna mikakati gani serious ya kushinda uchaguzi 2020?

Chadema hawana mkakati wowote ni kama mkulima wa Dodoma anayesubiri mvua inyeshe msimu ukiisha na kazi inaishia hapo
 
Chadema wameacha yao yanayo wahudu wamebaki kushabikia migogoro ya ndan ya ccm tu
 
Huwezi kukiondoa madarakani chama kikongwe kama CCM kwa kulalamika kwenye vyombo vya habari, au kusubiri kigawanyike, unaweza kusubiri isiwe na kulalamika tu hakutoshi.

Hadi sasa hatuoni movement yeyote serious kuonyesha kweli mna nia ya kuingia ikulu, pamoja na operation Chadema ni msingi, kwa mfano, kuliko kuishia kufanya press conference pale Ufipa, mnaweza kuandaa makongamano ya kimataifa Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere, mkaita vyombo mbalimbali vya ndani na nje, investors, mabalozi, mkaalika known public speakers ikiwezekana kutoka nje, mkatumia fursa hiyo kueleza sera zenu na jinsi mtakavyozitekeleza mtakapochukua madaraka. Huo ni mkakati mmoja tu wa kujitangaza ndani na nje mkaaminika, kwa dunia ya leo huwezi kushinda urais bila support ya nje. Hatuoni mkifanya hivyo.

Sioni mkakati wa kuunganisha nguvu, nilisikia wapinzani wameanzisha Azimio la Zanzibar sijui limeishia wapi, nchini Kenya haikuwa kazi rahisi kuiondoa KANU, vyama vya upinzani viliungana baadhi ya viongozi wao wali sacrifice vyeo vyao.

Siyo lazima muweke wazi mikakati yote lkn angalau wapiga kura waanze kuona mwelekeo wa chama towards 2020, siyo mbali, ikiwezekana wamjue mshika kibendera siyo waje kushitukizwa dakika za mwisho kama mlivyofanya kwenye uchaguzi uliopita.

Kushinda uchaguzi ni zaidi ya sanduku la kura, ingekuwa sanduku leo Lowassa angekuwa rais kwa sababu naimani alipata kura nyingi na Self angekuwa rais wa Zanzibar, sanduku la kura ni kitendo cha kuhalalisha (legitimise) mikakati yako uliyofanya kabla, ya halali na isiyo halali.

If you don't plan you are planning to fail.
CHADEMA WAMEPOTEZA DIRA KABISA KIUFUPI
 
Yaani mabalozi, wawekezaji wa nje na ndani, na wengine kama hao waalikwe na CHADEMA ukumbi wa Nyerere wao kama wapigakura au vipi?
Huna hoja.
 
Nadhani kwa sasa wanamuacha bwana yule atambe na ajidanganye kuwa anakubalika ila wakati wa kampeni ukifika,wataanza kutema cheche na hapo bwana yule na chama chake ndio watajua wanakubalika kiasi gani.

Kwa sasa, wamebanwa, ila wanapata nafasi ya kukusanya madhaifu na kasoro za bwana yule na wakati ukifika wataanza kuyasema majukwaani.
Kibendera katika Ubora wake
 
Mkakati wa MaCCM ni kuzui mikutano ya CDM hata ya ndani.
Kama mnajiamini ruhusu mikutano na shughuli za kisiasa ili watu waambiwe ukweli.
Acha kujidai mnapendwa kumbe ni dhuluma na mauwaji!!
 
Yaani mabalozi, wawekezaji wa nje na ndani, na wengine kama hao waalikwe na CHADEMA ukumbi wa Nyerere wao kama wapigakura au vipi?
Huna hoja.
Hata nikikuelezea huwezi kuelewa inaonekana iko juu ya uwezo wako.
 
Quineni siasa ndiyo maisha, hata ukilima mahindi viazi nk bila siasa nzuri unakuwa fukara.
MaCCM wameleta ufukara kwa kuuwa soko la mazao kuanzia mbaazi mahindi kahawa hadi korosho.
Umejua ukweli sasa kawaambie Lumumba wajue dhuluma wanazofanya!!
 
Tatizo ubongo wako kwa sasa umegandishwa na Musiba maana kilicho changia na utumbo unao andika ni vitu viwili tofauti
Unachangia huku unamlaani mleta uzi kwa kuwavua nguo kwamba mpaka muda chama hakina muelekeo!
 
Shukrani sana mkuu kwa uchambuzi mzuri
Upinzani umefungwa mikono na miguu, huku watawala wakiwa huru kufanya wanachokitaka, popote pale na escort ya polisi wanapata, media attention wanapewa...

Ni ngumu kutoboa, hata wanachama wako kukutana nao huna uhuru huo..

Mbinu zilizosalia ni kutumia nguvu ya uma, ila chadema hawako tayari ku_risk usalama wa raia wake kwa sasa...

So, maybe kuna mipango smart zaidi wanayo..ila kila physical mean wamebanwa...
 
Sasa wewe punga LA Lumumba wakwambie mikakati yao ikusaidie nin wewe endelea kuliwa hapo Lumumba.
Punga ni wewe unayejibu hoja ya msingi kwa matusi. Kwani ungewasilisha hoja yako bila kutukana isingeeleweka?
 
Mwanzoni tulijua kuwa swala la susasusa lilikuwa la muda kupima upepo kumbe hii ni sera mbadala ya chama hicho. Wachambuzi wa mabo ya kisiasa wanasema chama cha democrasia na maendereo na ni chama kikuu cha upinzani Tanzania kinapita katika kipindi kigumu sana kwana tangia kuondoka kwa Dr Slaa kimeonyesha pengo kubwa kwa kutumia kichwa kimoja cha Freeman Mboe ambae yeye anaona njia pekee ni kususia uchaguzi zote.

Katabia haka kalianzishwaga zamani kidogo na Freeman Mboe mwenyewe kule bungeni lakini Dr. Slaa alikuwa anakapinga sana na baada ya kuondoka sasa imekuwa ndiyo sera kuu ya chama hicho. Wafuwasi wa chama hicho wanamwamini kiongozi huyo kuwa hawezi kukosea hata kidogo kitu ambacho ni kizuri pia.

Taarifa zinasema kuwa hari ya kisiasa katika chama hicho sio siri tena kwani nikama chama kimekutana na kisiki cha mpingo. Chama hiki ambacho kimewahi kuruka vihunzi vingi sana vigumu lakini kwasasa kimeshindwa kuruka hiki kihunzi cha awamu ya 5 na njia pekee kwa chama hicho kwa sasa ni kususatu.

Baadhi ya wabunge wa chama hicho ambao waliomba majina yao yasitajwe wamesema hata wao wamepoteza matumaini kwani kamanda mkuu aliyekuwa akijulikana kama mfalme wa anga wakati huo hawauoni ufalme ule tena.
Mmoja aliendaa mbali zaidi huku akisisitiza jina lake wala picha kuchukuliwa na kusema anajuta kuikataa ile ofa iliyotolewa na JPM kipindikile.

Wadadavuaji wanasema kilichowakatisha tamaa zaidi hadi mtaa anaotokea Freemani Mboe pia hauna mwakilishi na kibaya zaidi chama kinazidi kudorora siku hadi siku lakini Mwenyekiti huyo wa taifa wa chama hicho yeye anasisitiza kutuchangisha wabunge kwa kukatwa katika mishahara na posho zao. Hata hivyo mmoja wa wabunge hao ambaye amekuwa mtihifu sana kwa mwenyekiti huyo anakili kuwa hari hii inachangia kwani chama chao kina hisia za humiliki wa mtu.
Mbunge mwingine akiongea huku akijipa moyo mwenyewe yeye alisema kuwa maisha bado yapo ataendelea na shughuli zake za zamani na hatoiacha Chadema kwani hata mtaji ameupatia katika chama hicho.

Kwanini sera mbadala ya kususia uchaguzi mkuu itadumu na kutumika 2020:
  1. Mosi chama kimepoteza mshikamano au ummoja kwani chama ni vikao kwa hivi sasa hakuna vikao enderevu kuanzia juu wala chini na tumeshuhudia baadhi ya ofisi zikirudishwa kwa kusa kodi na zilizopo zina vumbi yaani azijafunguliwa kwa muda.
  2. Vingozi karibu wote wakuu wa chama au wajuu kabisa bara na visiwani wanakesi mahakamani hivyo watoto wanakosa mwongozo na baba akiulizwa kitu kwakuwa amefikwa na mazito jibu lake ni jepesi tu, suseni kwani haoni njia nyingine tena.
  3. kuondoka kwa Dr. Slaa na lowasa. hili bado limeacha maumivu na maswalimengi ya ndani kwa wanachama na wapenzi wa chama hicho ambapo kwa sasa wanaanza kujua kuwa kunamaamuzi mepesi yalifanywa na viongozi wao aidha kujipatia pesa au kukosa mikakati imara na makini ambapo imewamega nusu kuwaamini na nusu nyingine kukosa imani na chama hicho na hii imekuja kwa kuwa mpaka leo hawajaambiwa kwanini waliamua kumkataa Dr. Slaa na kumpokea waliyemwita mwizi na fisadi kwa mika 8. Hivyo uchaguzi ujao njia pekee ni kususa.
  4. Kutokuaminiana katika vikao vya ndani, hili limekuja kwao kama jinamizi kwani wanashindwa wa kumwamini kwasababu leo wanaongea nae kesho anaamia Ccm. Katika vikao kama hivyo ambavyo mkopamoja lakini si wamoja ni ngumu kuweka mikakati thabiti ya kikazi kwani kilammoja amamwogopa mwenzie na muda wote wa kikao mwenyekiti anatumia muda mwingi kutishia wasaliti.
  5. Kuachana na sera ya kupambana na ufisadi na kuja na sera ya kususa hili pia ni mwendelezo wa kususa tu.
  6. Walisemaga huko nyuma na kuwafundisha wananchi kwa nguvu zao zote nchi zima kuwa nchi hii tunataka Raisi atakayekuwa hasafiri safiri. Nchi hii inataka Raisi mkali, Nchi hii inatakiwa Raisi anaye chukia rushwa, Nchi hii ianatakiwa raisi atakayekuwa anakusanya kodi (huku wakisaahau kuwa Freemani halikuwa halipi kodi) na walienda mbali zaidi na kusema nchi hii inahitaji Raisi dikteta na mengine mengi. Sasa haya yote watu waliyashika na wameshindwa kutoa majibu, badala yake wakaja na sara ya kupinga kila kitu hata walivyovitabiri wenyewe pia walisahau, hivyo njia pekee ya kuepuka aibu yoyote ni kususa uchaguzi tu.
  7. kuzuiwa kwa maandamano nchi nzima na kuelekeza nguvu hizo katika kufanyakazi pia hili liliipunguzia Chadema kiki sana katika medani za kisiasa kwani wakati ule jambo dogo tu likitokea wanatangaza maandamano nchi nzima kwa sasa No. Njia pekee kwa chama hicho ni kususa kwani hakuna tena M4C, Operasheni Sangara na UKUTA.
  8. Siasa za kutukana watu katika awamu hii imesema matusi basi, kitu ambacho ni ngumu kwa kiongozi wa Chadema kupanda jukwaani bila kutoa mitusi kwani hata Mtumishi wa Mungu Mchungaji Msigwa pia alikuwa anashusha mineno hisiyo poozwa yaani kila aliyesimama jukwaani aliachilia mitusi na tuliamini siasa za vyama vingi ni mitusi kipindi kile. Hivyo hapa njia pekee ni kususa kwani Chadema bila mitusi haiwezekani. Maana kipindi cha nyuma uliweza kutukana kuanzia Raisi hadi mtendaji wa kijiji na usifanywe kitu chochote lakini katika awamu hii unapotoa neno chafu watu wa usalama wanakushusha pale pale na wanaondoka na wewe na mkutano unaendelea bila matata.
  9. Siasa za kiki hizi nazo zimekuwa ngumu sana kuzifanya katika kipindi hiki. kwamfano zamani kama kumetoke ajali kubwa imeua watu wengi au mafuriko au tetemeko basi wapinzani waliinuka kisiasa lakini kwa awamu hii hakuna kitukama hicho. Hivyo hakuna njia nyingine ya kujihararisha isipokuwa ni kususa tu.
  10. Wafuasi na wanachama wa chama hiki wa wingi wao wengi wanaamini kuwa mtu pekee chini ya jua anayeweza kuwatoa hapo ni Freemani mboe pekee, si jambo baya. Lakini yeye Mboe mwisho wake wa kufikiri na kupambana kwake kwa sasa anaona njia pekee ni kususa tu ndiyo maana alianzisha bungeni, hata kikao cha kumpokea JPM bungeni yeye ndiyo aliongoza kususa na leo serikali za mitaa 2020 uchaguzi mkuu.
Asanteni.
 
Back
Top Bottom