Madhara yatakayoletwa baada ya uchaguzi huu hayatakwisha na yataleta vikundi vingi sana vya ajabu tz. Hatuombei ila Hekima inahitajika sana kwa viongozi wetu.
Hekima ya kwanza ni hao walioshindwa kuheshimu katiba ya nchi;
hekima yao ya pili ni kutii sheria za nchi bila shuruti,
tatu wawaombe msamaha watanzania kwa makosa waliyoyafanya wakati wa kampeni kwa kuwadhalilisha watanzani na hasa wafuasi wao kwa hao washindwaji kushindwa kunadi sera za chama chao kupitia ilani yao badala yake wakawa wanatukana viongozi wa serikali wakati wanajua serikali si chama cha siasa;
ya nne ni kuviomba msamaha NEC na vyombo vyetu vya usalama kwa kuvidhalilisha na kuvidharau leo;
tano wakubali matokeo na waache wafuasi wao waliopewe raidhaa na wananchi kuwawakilisha watekeleze wajibu huo.
Sita, watamke wazi na kwa kuapa kuwa hawatajihusisha na wale wote wanaodhaniwa hawaitakii mema TANZANIA.
Saba wawe tayari kushiriki kwa uaminifu Tanzania kuwa imara katika nyanja zote za kimaendeleo bila hila.
Nane, watoe mrejesho wa mapato na matumizi ya ela zote walizowahi kuchangiwa katika mikusanyiko yao ya kichama na hasa wakati wa kampeni. Ili warudishe imani kwa wafuadi wao
Tisa, Waahidi rasmi na kwa uwazi tena kwa maandishi kumuunga mkona rais aliyechaguliwa na wananchi, ndugu yetu rais mteule Dr. JPJ Magufuli.
Kumi, waahidi kumrejesha shahidi namba moja dereva wa Antipasu wakati anashambuliwa ili asaidie kutoa taarifa rasmi zinazoweza kusaidia washukiwa wa uhalifu huo kutiwa mbaroni.
====
Waweza kuongeza hekima zingine kuwasaidia ndugu zetu hawa ambao wako " depressed "!