GE2025 CHADEMA: Tumepata taarifa ya Tundu Lissu kutaka kupewa sumu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
TAARIFA KWA UMMA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinapenda kuujulisha umma kuwa kimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa zinazodai kuwa Mhe. Tundu Lissu, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, kuna mipango ya kuwekewa sumu akiwa kizuizini.

Taarifa hizi zimetolewa usiku huu wa leo, tarehe 02 Julai 2025, kutoka kwa vyanzo mbalimbali vya kuaminika. Miongoni mwa waliotoa kauli kuhusu suala hili ni Mhe. David McAllister, Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Ulaya (European Parliament), ambaye kupitia ukurasa wake wa X (zamani Twitter) ameandika:

"Nina wasiwasi mkubwa kuhusu ripoti za kutisha za jaribio la kumtilia sumu kiongozi wa upinzani wa Tanzania Tundu Lissu akiwa kizuizini."

Chadema inachukulia taarifa hizi kwa uzito wa hali ya juu. Hili si jambo la kupuuzia, hasa tukikumbuka kuwa si mara ya kwanza kwa viongozi wa Chadema kulengwa na vitisho, mashambulizi au uonevu wa aina mbalimbali, huku taarifa nyingi tulizowasilisha kwa mamlaka husika zikipuuzwa au kutochukuliwa hatua yoyote.

Tunazitaka mamlaka husika, likiwemo Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka na Mahakama kuchukua hatua za haraka, huru na za kina kuchunguza madai haya mazito. Tunaitaka Serikali kutoa kauli ya wazi na kuwajibika kuhakikisha usalama wa Mhe. Tundu Lissu akiwa kizuizini.

Pia, soma; IDU tunafatilia njama za kumuwekea Lissu sumu Gerezani

Tunatoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa, Mashirika ya Haki za Binadamu, Mabalozi na wahusika wengine wote wa kimataifa kufuatilia kwa ukaribu suala hili na kushinikiza uwajibikaji, ulinzi wa haki za binadamu, na kuheshimiwa kwa misingi ya demokrasia nchini Tanzania.

Imetolewa leo Jumatano, tarehe 02 Julai 2025

Brenda Rupia

Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi

View attachment 3391862
Kwa zile nondo walizopigwa na kamanda mahakamani lazma bi chura atafte njia mbadala,Ila Haki itashinda dhidi ya dhuluma Mungu yupo
 
Hizo taarifa ninazo kabla ndo maana nikaishauri serekali imuhudumie Lissu kila kitu magereza wasipokee chochote kutoka kwa watu wa Chadema kumpa Lissu wanaweza kumuua ili waichonganishe serekali na wananchi
kataa ujinga kubali maarifa uishi vizuri na watu
 
TAARIFA KWA UMMA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinapenda kuujulisha umma kuwa kimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa zinazodai kuwa Mhe. Tundu Lissu, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, kuna mipango ya kuwekewa sumu akiwa kizuizini.

Taarifa hizi zimetolewa usiku huu wa leo, tarehe 02 Julai 2025, kutoka kwa vyanzo mbalimbali vya kuaminika. Miongoni mwa waliotoa kauli kuhusu suala hili ni Mhe. David McAllister, Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Ulaya (European Parliament), ambaye kupitia ukurasa wake wa X (zamani Twitter) ameandika:

"Nina wasiwasi mkubwa kuhusu ripoti za kutisha za jaribio la kumtilia sumu kiongozi wa upinzani wa Tanzania Tundu Lissu akiwa kizuizini."

Chadema inachukulia taarifa hizi kwa uzito wa hali ya juu. Hili si jambo la kupuuzia, hasa tukikumbuka kuwa si mara ya kwanza kwa viongozi wa Chadema kulengwa na vitisho, mashambulizi au uonevu wa aina mbalimbali, huku taarifa nyingi tulizowasilisha kwa mamlaka husika zikipuuzwa au kutochukuliwa hatua yoyote.

Tunazitaka mamlaka husika, likiwemo Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka na Mahakama kuchukua hatua za haraka, huru na za kina kuchunguza madai haya mazito. Tunaitaka Serikali kutoa kauli ya wazi na kuwajibika kuhakikisha usalama wa Mhe. Tundu Lissu akiwa kizuizini.

Pia, soma; IDU tunafatilia njama za kumuwekea Lissu sumu Gerezani

Tunatoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa, Mashirika ya Haki za Binadamu, Mabalozi na wahusika wengine wote wa kimataifa kufuatilia kwa ukaribu suala hili na kushinikiza uwajibikaji, ulinzi wa haki za binadamu, na kuheshimiwa kwa misingi ya demokrasia nchini Tanzania.

Imetolewa leo Jumatano, tarehe 02 Julai 2025

Brenda Rupia

Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi

View attachment 3391862
Habari ya kustua sana hizi, wahenga walisema mpe mchawi mwana amlee. manake hata mdhulu. Sasa huyu mchawi dola hana haya wala aibu. Kama walimshusha mzee wa watu katika Bus na kwenda kumuuua hawashindwi kumuwekea sumu mwenyekiti.
 
TAARIFA KWA UMMA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinapenda kuujulisha umma kuwa kimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa zinazodai kuwa Mhe. Tundu Lissu, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, kuna mipango ya kuwekewa sumu akiwa kizuizini.

Taarifa hizi zimetolewa usiku huu wa leo, tarehe 02 Julai 2025, kutoka kwa vyanzo mbalimbali vya kuaminika. Miongoni mwa waliotoa kauli kuhusu suala hili ni Mhe. David McAllister, Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Ulaya (European Parliament), ambaye kupitia ukurasa wake wa X (zamani Twitter) ameandika:

"Nina wasiwasi mkubwa kuhusu ripoti za kutisha za jaribio la kumtilia sumu kiongozi wa upinzani wa Tanzania Tundu Lissu akiwa kizuizini."

Chadema inachukulia taarifa hizi kwa uzito wa hali ya juu. Hili si jambo la kupuuzia, hasa tukikumbuka kuwa si mara ya kwanza kwa viongozi wa Chadema kulengwa na vitisho, mashambulizi au uonevu wa aina mbalimbali, huku taarifa nyingi tulizowasilisha kwa mamlaka husika zikipuuzwa au kutochukuliwa hatua yoyote.

Tunazitaka mamlaka husika, likiwemo Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka na Mahakama kuchukua hatua za haraka, huru na za kina kuchunguza madai haya mazito. Tunaitaka Serikali kutoa kauli ya wazi na kuwajibika kuhakikisha usalama wa Mhe. Tundu Lissu akiwa kizuizini.

Pia, soma; IDU tunafatilia njama za kumuwekea Lissu sumu Gerezani

Tunatoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa, Mashirika ya Haki za Binadamu, Mabalozi na wahusika wengine wote wa kimataifa kufuatilia kwa ukaribu suala hili na kushinikiza uwajibikaji, ulinzi wa haki za binadamu, na kuheshimiwa kwa misingi ya demokrasia nchini Tanzania.

Imetolewa leo Jumatano, tarehe 02 Julai 2025

Brenda Rupia

Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi

View attachment 3391862
 
Attachments

  • Screenshot_20250703-081821.png
    Screenshot_20250703-081821.png
    491.9 KB · Views: 25
  • Screenshot_20250703-081802.png
    Screenshot_20250703-081802.png
    170 KB · Views: 25
Hizi ni tuhuma nzito sana , CCM mmefikia hatua hii kweli?? Kisa tu hamtaki Reforms.

Watanzania wameshawachoka they want changes - mtake msitake hamtaweza kulizima.wimbi hiki la mabadiliko hata kwa kushirikiana na hao machawa wenu.

# free Tundu Lissu#
 
Hii ni habari mbaya sana Serikali inafaa ichukue hatua stahiki katika hili mana mambo huanza hivi hivi kuharibu nchi.Hii haikubaliki mpinzani sio adui ni kutoftiana mawazo kuna shida gani uwaze upange kuua watu wanaotofautiana tu mawazo na mtazamo???
 
Serikari ipi Inayotakiwa kuchukua hatua??
 
Hakuna mtu wa kumpa sumu lissu akiwa mikononi mwa dola,hiyo italeta kelele na vurugu zaidi, hapo kuna watu wanaotaka mama avurugikiwe ndiyo huenda watafanya hilo,wangetaka kumuua wangefanya akiwa nje,isingeleta shaka
Naweza kukuunga mkono but serikali itakua wajinga kiasi gani? Japokua kuna sumu unapewa Leo unaenda Kukata kamba baada ya miezi hata Sita au mwaka
 
Back
Top Bottom