GE2025 CHADEMA: Tumepata taarifa ya Tundu Lissu kutaka kupewa sumu

GE2025 CHADEMA: Tumepata taarifa ya Tundu Lissu kutaka kupewa sumu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
TAARIFA KWA UMMA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinapenda kuujulisha umma kuwa kimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa zinazodai kuwa Mhe. Tundu Lissu, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, kuna mipango ya kuwekewa sumu akiwa kizuizini.

Taarifa hizi zimetolewa usiku huu wa leo, tarehe 02 Julai 2025, kutoka kwa vyanzo mbalimbali vya kuaminika. Miongoni mwa waliotoa kauli kuhusu suala hili ni Mhe. David McAllister, Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Ulaya (European Parliament), ambaye kupitia ukurasa wake wa X (zamani Twitter) ameandika:

"Nina wasiwasi mkubwa kuhusu ripoti za kutisha za jaribio la kumtilia sumu kiongozi wa upinzani wa Tanzania Tundu Lissu akiwa kizuizini."

Chadema inachukulia taarifa hizi kwa uzito wa hali ya juu. Hili si jambo la kupuuzia, hasa tukikumbuka kuwa si mara ya kwanza kwa viongozi wa Chadema kulengwa na vitisho, mashambulizi au uonevu wa aina mbalimbali, huku taarifa nyingi tulizowasilisha kwa mamlaka husika zikipuuzwa au kutochukuliwa hatua yoyote.

Tunazitaka mamlaka husika, likiwemo Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka na Mahakama kuchukua hatua za haraka, huru na za kina kuchunguza madai haya mazito. Tunaitaka Serikali kutoa kauli ya wazi na kuwajibika kuhakikisha usalama wa Mhe. Tundu Lissu akiwa kizuizini.

Pia, soma; IDU tunafatilia njama za kumuwekea Lissu sumu Gerezani

Tunatoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa, Mashirika ya Haki za Binadamu, Mabalozi na wahusika wengine wote wa kimataifa kufuatilia kwa ukaribu suala hili na kushinikiza uwajibikaji, ulinzi wa haki za binadamu, na kuheshimiwa kwa misingi ya demokrasia nchini Tanzania.

Imetolewa leo Jumatano, tarehe 02 Julai 2025

Brenda Rupia

Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi


View attachment 3391862
Huu ni upuuzi mwingine wenye lengo la kukusanya pesa kutoka kwa mabwana zenu. No Reporn No Errection.
 
Tafadhali aisee..lini nimekuwa mwanaCCM? Kwenye kesi yoyote inayohusu mauaji ambapo mtuhumiwa hajulikani swali la kwanza ni nani atanufaika na kifo cha mtu huyo. Tuchukulie kuwa hizi tetesini za kweli; unafikiri Samia ndiyo atanufaika zaidi itokee kweli Lissu afie jela? Sioni namna gani kama kwa kuendelea kuwa jela hairpiece faida yoyote Samia...
Utanisamehe, siku zote nilikuchukulia kuwa wewe ni mwana CCM asiyejali ni CCM ipi; maana kuna CCM nyingi tumeziitia Tanzania; zikitumia jina hilo hilo!

Huo mstari wako wa mwisho sikuelewi. Samia alitegemea kufaidika na matukio ya utekaji/upotevu/kuuawa kwa vijana kadhaa wa CHADEMA; akiwemo na mzee Kibao?
Kama unasema ha ana, hakuwa na uwezo wa kuyazuia?

Samia Suluhu Hassan, anachotaka ni kubaki madarakani; njia zitakazotumika azijue asizijue hilo ni swala jingine kabisa. Matokeo yake ni "kufaidika" kwake.
 
Hawa CCM waliwahi taka kumuua Mzee Mangula kwa Sumu, kuna yule jamaa mwenye Kibiongo hatari sana kwa haya mambo..
 
Mkuu funza wewe ni member mkongwe hapa JF ila ajabu sana unapotosha kuhusu Mbowe. Nani anafaidika na kunufaika na uzushi wako? Umekosa content? Mbona ulikuwa kimya kama ulijua hayo? Au wewe ndio wale wale?
Mbowe siyo mungu au mbowe ni malaika wako? Tambua kuwa mbowe ana chuki kubwa na Lisu kuliko hata ibirisi wa ccm, hakuna kinachopotoshwa hapo njama zote za kumpoteza Lisu ni Mbowe kwa kushirikiana na ibirisi wa ccm
 
Hawa CCM waliwahi taka kumuua Mzee Mangula kwa Sumu, kuna yule jamaa mwenye Kibiongo hatari sana kwa haya mambo..
ibirisi wa ccm wanahaha wanaweza kumwekea slow poison aje kufa huko baadae baada ya kuona wapenda haki wamewashitukia mapema
 
Kwenye duru za siasa hivi vitu huwa vipo. Hata ukimwangalia in deep hayuko sawa. Ana msongo mkubwa.

Kosa kubwa ni kuamua kujisimamia mwenyewe 100 kwa 100 kwenye kesi.
Mawakili wa Lisu wamenyimwa nafasi ya kuongea nae faragha ndipo akaona ajitetee mwenyewe lakini pia wapo nae sambamba kwa kila hali
 
Back
Top Bottom