GE2025 CHADEMA: Tumepata taarifa ya Tundu Lissu kutaka kupewa sumu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Write your reply...hakuna serikali itafanya upumbavu kama huu. Lengo kujengesha chuki mabeberu yanapambana kumuweka mtu wao kwa namna yeyote ile
Mabeberu ndo yanayotoka na kupoteza watanzania?, au mabeberu ndo wasiojulikana waliompiga risasi 30+?

Vinginevyo na wewe upuuzwe......
 
Kwenye duru za siasa hivi vitu huwa vipo. Hata ukimwangalia in deep hayuko sawa. Ana msongo mkubwa.

Kosa kubwa ni kuamua kujisimamia mwenyewe 100 kwa 100 kwenye kesi.
 
Huyu ndiyo dikteta sasa sio JPM. Kama unabisha muulize yule jamaa aliyenibatiza jina Ponjoro. Sasahivi ansishi kama digidigi. Maja nayeye katema bungo tayari. Huko kigoma bwana miplan nayeye ameshatema bungo kudadadeki walai.
🤔 🤔 🤔 💭
 
TAARIFA KWA UMMA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinapenda kuujulisha umma kuwa kimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa zinazodai kuwa Mhe. Tundu Lissu, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, kuna mipango ya kuwekewa sumu akiwa kizuizini.

Taarifa hizi zimetolewa usiku huu wa leo, tarehe 02 Julai 2025, kutoka kwa vyanzo mbalimbali vya kuaminika. Miongoni mwa waliotoa kauli kuhusu suala hili ni Mhe. David McAllister, Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Ulaya (European Parliament), ambaye kupitia ukurasa wake wa X (zamani Twitter) ameandika:

"Nina wasiwasi mkubwa kuhusu ripoti za kutisha za jaribio la kumtilia sumu kiongozi wa upinzani wa Tanzania Tundu Lissu akiwa kizuizini."

Chadema inachukulia taarifa hizi kwa uzito wa hali ya juu. Hili si jambo la kupuuzia, hasa tukikumbuka kuwa si mara ya kwanza kwa viongozi wa Chadema kulengwa na vitisho, mashambulizi au uonevu wa aina mbalimbali, huku taarifa nyingi tulizowasilisha kwa mamlaka husika zikipuuzwa au kutochukuliwa hatua yoyote.

Tunazitaka mamlaka husika, likiwemo Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka na Mahakama kuchukua hatua za haraka, huru na za kina kuchunguza madai haya mazito. Tunaitaka Serikali kutoa kauli ya wazi na kuwajibika kuhakikisha usalama wa Mhe. Tundu Lissu akiwa kizuizini.

Pia, soma; IDU tunafatilia njama za kumuwekea Lissu sumu Gerezani

Tunatoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa, Mashirika ya Haki za Binadamu, Mabalozi na wahusika wengine wote wa kimataifa kufuatilia kwa ukaribu suala hili na kushinikiza uwajibikaji, ulinzi wa haki za binadamu, na kuheshimiwa kwa misingi ya demokrasia nchini Tanzania.

Imetolewa leo Jumatano, tarehe 02 Julai 2025

Brenda Rupia

Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi

View attachment 3391862
Labda nyie mnaompelekea chakula huko gerezani ndo mumwekee sumu.
Nashauri Lissu aanze kupewa chakula wanachopewa mahabusu wote.
 
Huyu ndiyo dikteta sasa sio JPM. Kama unabisha muulize yule jamaa aliyenibatiza jina Ponjoro. Sasahivi ansishi kama digidigi. Maja nayeye katema bungo tayari. Huko kigoma bwana miplan nayeye ameshatema bungo kudadadeki walai.
Katelefoni nae katema bungo. Nduguyai yeye alitema zamani sana.
 
Hata mseme nini hizi drama za kutunga wengine tumeishazizoea😂
Mkuu ukiwa na utimamu wa akili sio kila jambi ni la kupuuza. Ukikutana njiani na kichaa na akakuambia unakoelekea huko kuna nyuki usipuuzze kwa sababu ya ukichaa wake. Chukua tahadhari.
Mashirika makubwa ya upelelezi kama FIB nk kwao kila taarifa inachikuliwa kwa uzito mkubwa.
Chadema hawapaswi kukaa kimya.
 
Mungu amlinde dhidi ya waovu
Mhe Tundu Lissu
Akawaaibishe wanaoitafuta nafsi yake, maana yeye Mungu amesema mwenyewe kuwa ataagiza Malaika zake toka Mbinguni wakulinde mguu wako usijikwae.
 
Mtu anatiria shaka, watu mmeamin bila ushahidi.
Mda utasema...

Wakitaka kumpa sumu ni suala simple tu, anakwenda na maji.
Ila saiv hawawezi kwan watahojiwa...

Labda apigwe sumu ya mda mrefu.. Aje afe baadae
 
Aisee
 
Attachments

  • FB_IMG_1751515057912.jpg
    FB_IMG_1751515057912.jpg
    136.5 KB · Views: 14
Kwenye duru za siasa hivi vitu huwa vipo. Hata ukimwangalia in deep hayuko sawa. Ana msongo mkubwa.

Kosa kubwa ni kuamua kujisimamia mwenyewe 100 kwa 100 kwenye kesi.
Huyui kusoma body language ya mtu. Lissu yupo vizuri kiakili na kiafya. Hana shida yoyote.
 
TAARIFA KWA UMMA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinapenda kuujulisha umma kuwa kimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa zinazodai kuwa Mhe. Tundu Lissu, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, kuna mipango ya kuwekewa sumu akiwa kizuizini.

Taarifa hizi zimetolewa usiku huu wa leo, tarehe 02 Julai 2025, kutoka kwa vyanzo mbalimbali vya kuaminika. Miongoni mwa waliotoa kauli kuhusu suala hili ni Mhe. David McAllister, Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Ulaya (European Parliament), ambaye kupitia ukurasa wake wa X (zamani Twitter) ameandika:

"Nina wasiwasi mkubwa kuhusu ripoti za kutisha za jaribio la kumtilia sumu kiongozi wa upinzani wa Tanzania Tundu Lissu akiwa kizuizini."

Chadema inachukulia taarifa hizi kwa uzito wa hali ya juu. Hili si jambo la kupuuzia, hasa tukikumbuka kuwa si mara ya kwanza kwa viongozi wa Chadema kulengwa na vitisho, mashambulizi au uonevu wa aina mbalimbali, huku taarifa nyingi tulizowasilisha kwa mamlaka husika zikipuuzwa au kutochukuliwa hatua yoyote.

Tunazitaka mamlaka husika, likiwemo Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka na Mahakama kuchukua hatua za haraka, huru na za kina kuchunguza madai haya mazito. Tunaitaka Serikali kutoa kauli ya wazi na kuwajibika kuhakikisha usalama wa Mhe. Tundu Lissu akiwa kizuizini.

Pia, soma; IDU tunafatilia njama za kumuwekea Lissu sumu Gerezani

Tunatoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa, Mashirika ya Haki za Binadamu, Mabalozi na wahusika wengine wote wa kimataifa kufuatilia kwa ukaribu suala hili na kushinikiza uwajibikaji, ulinzi wa haki za binadamu, na kuheshimiwa kwa misingi ya demokrasia nchini Tanzania.

Imetolewa leo Jumatano, tarehe 02 Julai 2025

Brenda Rupia

Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi

View attachment 3391862
Hivi nchi hizi imekosa watu wenye busara wa kumwambia Samia na genge làke kuwa inatosha atuache salama?
 
^anataka kuwekewa sumu^?????

-Mkuu, hicho Kiswahili kimekaa kiponjoro sana.
 
Back
Top Bottom