Uchaguzi 2020 CHADEMA: Tunamuunga mkono Maalim Seif kwa Urais Zanzibar. Lissu hataendelea na kampeni, atapangiwa majukumu mengine

Uchaguzi 2020 CHADEMA: Tunamuunga mkono Maalim Seif kwa Urais Zanzibar. Lissu hataendelea na kampeni, atapangiwa majukumu mengine

Binafsi naona watapoteza kura nyingi sana za wale wanaohofia kura kuibiwa. Wengi waliamini ktk msimamo usiyo yumba wa Lisu na chama. Sasa kwa maamuzi haya stori zitakuwa zile zile za miaka yote
Wee fara kweli! Hiyo hukumu ni lazima itumikiwe, ingawa siyo ya haki, lakini ni ya halali. Hapa wewe, unafahamu fika wasipoitii, ni makosa, na hapo watakuwa wametengeneza kosa lingine. Na hilo ndio ombi lako litokee. Usifikirie hao jamaa ni wajinga kwa kuweza kufanya kama hayo MATAMANIO yako wewe TAGA!
 
Hili la watanzania kuwa waoga linajulikana Sana. Na ndiyo maana wananchi tumeweka matumaini yetu makubwa kwa mtu jasiri asuyeogopa kitu...Tundu lisu.
Kwani Lisu sio mtanzania? ni mbelgiji?
 
Wee fara kweli! Hiyo hukumu ni lazima itumikiwe, ingawa siyo ya haki, lakini ni ya halali. Hapa wewe, unafahamu fika wasipoitii, ni makosa, na hapo watakuwa wametengeneza kosa lingine. Na hilo ndio ombi lako litokee. Usifikirie hao jamaa ni wajinga kwa kuweza kufanya kama hayo MATAMANIO yako wewe TAGA!
Sasa kama ubatili huu unaheshimiwa. Badi na ubatili mwingine mkubwa wa mawakala kukataliwa na kura kuibiwa vitakuwa halali pia.
 
Kuna harufu ya uwoga hapa.

Sasa mgombea ataanza saa ngapi kampeni za leo? Hapa tushapata majibu tayari. Kamati kuu imeufyata kwa tume.
Be reasonable.
Hasira za mkizi hizi hazina nafasi wakati huu.

Huwezi kushinda vita kwa papara, ni lazima utumie mbinu, na CHADEMA wakati huu wanahitaji sana mbinu.

Tuliza hicho kichwa chako, najua unaweza kubuni mbinu bora zaidi ya kuinyonga CCM badala ya kuwapa ahueni unayowatafutia hapa.
 
Ukichunguza kwa makini Lisu huyu wa leo siye yule wa zamani kabla hajapelekwa ubelgiji.
We chunguza tu utagundua.
Intelligence yake imeshuka saaana!
I am sure kuna kitu wazungu wamemfanyia kudestroy some of his brain cells.
Sipo uko mkuu.
Twende na mada, unadhani uanzishwaji wa mfumo wa vyama vingi na utolewaji wa nyadhifa kwa wale waliorudi 'nyumbani' unaendana na hapa tulipo?
 
Ni busara hii hii ndiyo ilifanya 2015 tukaambiwa ooh Edo kashinda lkn muwe watulivu tutaenda ICJ. .....mpk leo kimya.

Sasa na uchaguzi huu chadema itapigwa (itaibiwa) mchana kweupee kisa busara.

Nafikiri viongozi wa Chadema Kuna kitu Cha ziada zaidi ya ukombozi wanachopigania. Wameniudhi sana, kwenda kinyume na Lisu.
Mkuu nadhani tuwe watulivu tusubiri maamuzi maana kamati kuu ina wajumbe zaidi ya 20 so lazima wame debate na kuweka options zote mezani wakaona ipi ina faida kubwa zaidi.

Maana huu ni mtego wa CCM kuona reaction kwa hiyo kutakachoamuliwa leo ndio kitaamua hatma ya upinzani hapo October 28.
 
Kuna barua ya maamuzi tushaiona mkuu.
Maamuzi ni kwamba kamati kuu imeridhia adhabu ya tume kwa mgombea urais hivyo ataitumikia mok tarehe 9/10.
 
baada ya hapo siwezi tena muamini Lisu.
ama kweli akili za kuambiwa changanya na za kwako...
 
Lisu amemtega Mbowe. Ni ama aheshikike ama adhauraulike. Maamuzi ya mgombea tunayajua, maamuzi ya kamati yakiwa kinyume na yale ya mgombea Mbowe utapwaya sana
Mara hii umekwishasahau busara kubwa alizotumia Mbowe hadi CHADEMA ikafikia hapa?
Wewe umesahau kwamba CHADEMA haikutakiwa iwepo wakati huu?
 
Nahisi hivyo wanachama wanamkubali sana TL lakini uongozi haumkubali chini ya MBW
Lisu toka ateuliwa ana hasira ana dharau kubwa mno kwa wajumbe wa kamati kuu
Hashauriki ,hasikilizi chochote.Ndio maana hata barua ya kumwita tume ya maadili katibu mkuu wa Chadema mnyika aliikataa akasema mpeklekeeni mwenyewe sisi kama chama hatuhusiki na matamshi yake abebe zigo lake mwenyewe

Lisualipopelekewa alikataa kabisa wito wa tume ya maadili akasema yeye anaendelea na kampeni kamati kuu ya Chadema ndio ikamlazimisha kuwa lazima atii afike Dar es salaam ajieleze mbele ya tume yeye Kama yeye na matamshi yake.

Kwa jeuri Lisu alipofika Dar akagoma kwenda tume akawaambia Kamati kuu sitaki siendi waamue lolote

Kamati kuu ya CHADEMA wakaona Kuna hatari huyu asipoenda italeta shida kubwa kwa chama ndipo wakatuma mawakili wawili waende Kamati ya maadili kwa niaba ya Lisu aliegoma kwenda akikoroma nyumbani kwake usingizi ili kunusuru chama

Maamuzi ya tume ya maadili yalipotoka kuwa Lisu asifanye kampeni siku Saba akaenda vyombo vya habari kusema hatambui bila kuwasiliana na kamati kuu ambao ndio walituma mawakili kwenda kikaoni kupewa mrejesho wa kichama kuhusu kile kikao ambacho chama kilituma wajumbe

Ikabidi Tena kamati kuu imwambie wewe Sasa inatakiwa tukujadili kamati kuu usiendelee na kampeni mpaka sisi kamati kuu tutoe tamko letu ambalo ndilo hilo mwenyekiti atakutana na waandishi wa habari leo

Lisu aliitwa kikaoni kikao Cha kamati kuu ya CHADEMA akajieleze akakataa akawaambia amueni lolote I don't care ndio maana kamati ilichelewa kutoa tamko ku sort out na kuweka mambo fulani sawa kati ya chama na mgombea mwenyewe aelewe maana ya party supremacy kama mgombea aliyeteuliwa na chama chake na ili asirudie tena kudharau kamati kuu na chama na wajumbe wa kamati kuu

Tamko la kamati kuu litakuwa na upande wa kumuonyesha kuwa sisi ndio kamati kuu wewe huko juu ya kamati kuu .Na ni vizuri kila mgombea uraisi wa chama kujua hilo kuwa ukiteuliwa na chama huko juu ya chama kipindi hiki cha uchaguzi ni lazima kuheshimu mamlaka za chama zilizo juu yako
 
Kuna barua ya maamuzi tushaiona mkuu.
Maamuzi ni kwamba kamati kuu imeridhia adhabu ya tume kwa mgombea urais hivyo ataitumikia mok tarehe 9/10.
Ungetoa mchango wa maana sana kama ungetumia wakati kubuni nini akifanye Lissu katika muda huo wa siku saba alizopewa ili kampeni zake zizidi kuimarika zaidi.

Huo sio muda uliopotea, ni muda unaoweza kutumika kuleta mafanikio chanya zaidi kwa mgombea mwenyewe.
 
Mkuu nadhani tuwe watulivu tusubiri maamuzi maana kamati kuu ina wajumbe zaidi ya 20 so lazima wame debate na kuweka options zote mezani wakaona ipi ina faida kubwa zaidi.

Maana huu ni mtego wa CCM kuona reaction kwa hiyo kutakachoamuliwa leo ndio kitaamua hatma ya upinzani hapo October 28.
Kinachotakiwa ni wafuasi walioanza kujenga ujasiri wafahamu kwamba mgombea na chama wana utiifu kwa mamlaka. Ni hilo tu tukielekea oct 28.

Nadhani unaelewa mamlaka iliyopo ni ya nani.
 
Kuna barua ya maamuzi tushaiona mkuu.
Maamuzi ni kwamba kamati kuu imeridhia adhabu ya tume kwa mgombea urais hivyo ataitumikia mok tarehe 9/10.
Then wame weigh options maana pale mwenye maamuzi sio Mbowe ila ni kura na walio wengi ndio wanasikilizwa. Kwahiyo wanajua zaidi kuliko sisi tuliopo huku nje kuhusu situation.
 
Back
Top Bottom