CHADEMA yajiondoa kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Waziri Jafo awashangaa kususia uchaguzi

CHADEMA yajiondoa kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Waziri Jafo awashangaa kususia uchaguzi

Mbowe alichelewa sana kufanya haya maamuzi yeye na kamati kuu

Ila pamoja na hayo wamefanya vyema kutokushiriki huo ujambazi unaoitwa uchaguzi wa serikali za mitaa
 
Salama wana bodi.

Tangu kuondoka kwa Dr Slaa ,Chadema haina ubunifu wala mvuto kwa wananchi tena. Hela walizokuwa wanapata kutoka kwa wafadhili zimekatika, chama kina njaa kali lakini ukweli huu hausemwi!!.

Mathalani wakati wa kuandikisha wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa chadema mkoa wa Kilimanjaro hawakuweka mawakala na alipoulizwa mwenyekiti wa chadema mkoa wa Kilimanjaro kwa nini chama hakiweki mawakala? Alisema Chadema hakina pesa ya kuwalipa mawakala shs 5000 kwa kila siku kwa siku 30 za uandikishaji!

Freeman Mbowe baada ya kuona maji ya shingo, sasa amekuja na mbinu mpya kugomea kushiriki kila uchaguzi ulio mbele yake na akiulizwa anasema ,sababu ni ubinywaji wa democrasia wakati si kweli. Ukweli ni kwamba chama hakina pesa..
Hata mchakato wa ndani wa chama kutafuta wagombea kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa chadema haikufanya.!!View attachment 1256773

Unajifunza propaganda lakini huzipatii, kwa hiyo uchaguzi huu uandikishaji ulikuwa siku 30?
 
Waswahili husema kufa kufaana baada ya chama kikuu cha upinzani nchini kujitoa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa kimetoa fursa kwa chama cha ACT wazalendo kuimarika zaidi.

Maana yake ni kwamba kwa sasa Chadema itakosa uwakilishi katika serikali za mitaa jambo ambalo ni hatari sana kwa ustawi wake.

Nina imani Zitto na maalimu Seif hawatasusia uchaguzi ila watapanga mbinu muafaka za kumkabili mwenzao waziri Jafo kwenye uwanja wa uchaguzi kwani waswahili wanasema.......Waarabu wa Pemba hujuana kwa vilemba.

Poleni sana Chadema

Maendeleo hayana vyama!

Mlenta mada nawe ni ng’ombe tu. ACT itang’aaje wakati wagombea wote wameenguliwa?
 
Leo nimemsikiliza ndg.Polepole akizungumza na waandishi wa habari kwa kweli vyama vya upinzani havina sababu ya msingi kususia uchaguzi kwani makosa yamefanywa kwa uzembe wa wagombea wao wenyewe, na hilo ni fundisho kwa vyama vya upinzani, kuwa wanahitaji elimu ya kutosha. uchaguzi sio lelemama!
Nyasaka hapa jijini Mwanza, mgombea mmoja kwenye fomu zake aliandika kazi yake ni dereva, akaambiwa aweke nakala ya leseni yake ya udereva kumbe hana, ila pia anaishi kwenye nyumba ya kupanga(si mkazi wa eneo hili) nasikia naye ameshindwa kuwa na vigezo jina lake limeondolewa, nauliza kama kaonewa ili nami nijiunge naye tususe kuitambua serikali ya mtaa itakayochaguliwa.
 
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ametangaza chama chake kutoshiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 24, 2019 kwa madai wakishiriki wanahalalisha ubatili

Maamuzi hayo yanakuja ikiwa ni baada ya Wabunge wa CHADEMA kukutana leo alasiri Novemba 7, 2019 katika Kikao cha Kamati Kuu ya dharura ya chama kilichofanyika mkoani Dodoma

Jana, Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itikadi, Uenezi na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema alisema Kamati hiyo itakutana leo kutoa msimamo wao wa mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

----
WAZIRI JAFO AWASHANGAA
Baada ya Chadema kutangaza kutoshiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa, Waziri wa Tamisemi, Seleman Jafo amesema uamuzi huo unawanyima fursa wagombea wa chama hicho waliopitishwa, waliokata rufaa kupinga kuenguliwa.


Pia soma
Jafoooo,baa.Hivi somo kweli utasimama leo na kusali sala ya isha?
 
Mleta mada na wewe ni kenge mlemavu,badala umshauli mchumia tumbo mwenzio Zitto,ili aonekane ni mpinzani wa kweli,wewe unasema ameokota dodo,hata chama chenu na kiongozi wako Mkuu msipo jitoa,ni wajinga wachache sana mliobaki kama wewe mtaenda kupiga kura.
 
Waswahili husema kufa kufaana baada ya chama kikuu cha upinzani nchini kujitoa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa kimetoa fursa kwa chama cha ACT wazalendo kuimarika zaidi.

Maana yake ni kwamba kwa sasa Chadema itakosa uwakilishi katika serikali za mitaa jambo ambalo ni hatari sana kwa ustawi wake.

Nina imani Zitto na maalimu Seif hawatasusia uchaguzi ila watapanga mbinu muafaka za kumkabili mwenzao waziri Jafo kwenye uwanja wa uchaguzi kwani waswahili wanasema.......Waarabu wa Pemba hujuana kwa vilemba.

Poleni sana Chadema

Maendeleo hayana vyama!
Mimi nilifikiri masisie leo yangeonekana barabara kushangilia Chadema kujitoa badala yake inaumia sasa yameanza kushawishi ACT ishiriki. Pumbavu piteni bila kupingwa muanze kuchekana wenyewe
 
Sasa ndio nimepàta majibu ni kwa nini jimbo LA Chato kuna mtu alikuwa anapita ubunge bila kupingwa kwa miaka 10 mfululizo kumbe mbinu zenyewe ni za kishamba sana.

Huyo ndio zilikuwa zake, hiyo tabia yake binafsi ndio kaipandikiza katika nchi nzima.
 
ndipo tulipofikia na safari bado inaendelea, Tanzania ya vibanda
 
Kawaida yao walikuwa wanatafuta mlango tu!

Hamuwezi siasa za ushindani, na huo upuuzi kupandikiza jiwe ndani vya ccm. Na kwakuwa ccm ilikuwa imechoka kushindana imeona ni sawa huu uhayawani uendelee.
 
Afadhali, INAKUBALIKA KAMA HUJAJIPANGA, UNA-RETREAT KISHA UNA-REGROUP.....
Hapa nimewapongeza chadema. Sasa mjipange vizuri, mkija hovyo 2020 WATANZANIA watawafyekelea mbali kwenye boks la kura.
 
Hamuwezi siasa za ushindani, na huo upuuzi kupandikiza jiwe ndani vya ccm. Na kwakuwa ccm ilikuwa imechoka kushindana imeona ni sawa huu uhayawani uendelee.
Mnalia lia toka 1995....
Watanzania tumewakataa upinzani huu wa kinafiki...
 
Back
Top Bottom