huyo hapendwi hata na mkewe na familia yake nadhani. enzi za kikwete tulikuwa tunawajuwa wanae kina Ridhiwani na Miraji huyu mwambafai hata haeleweki kama ana watoto na familia.
Tangu kuondoka kwa Dr Slaa ,Chadema haina ubunifu wala mvuto kwa wananchi tena. Hela walizokuwa wanapata kutoka kwa wafadhili zimekatika, chama kina njaa kali lakini ukweli huu hausemwi!!.
Mathalani wakati wa kuandikisha wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa chadema mkoa wa Kilimanjaro hawakuweka mawakala na alipoulizwa mwenyekiti wa chadema mkoa wa Kilimanjaro kwa nini chama hakiweki mawakala? Alisema Chadema hakina pesa ya kuwalipa mawakala shs 5000 kwa kila siku kwa siku 30 za uandikishaji!
Freeman Mbowe baada ya kuona maji ya shingo, sasa amekuja na mbinu mpya kugomea kushiriki kila uchaguzi ulio mbele yake na akiulizwa anasema ,sababu ni ubinywaji wa democrasia wakati si kweli. Ukweli ni kwamba chama hakina pesa..
Hata mchakato wa ndani wa chama kutafuta wagombea kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa chadema haikufanya.!!View attachment 1256773
Waswahili husema kufa kufaana baada ya chama kikuu cha upinzani nchini kujitoa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa kimetoa fursa kwa chama cha ACT wazalendo kuimarika zaidi.
Maana yake ni kwamba kwa sasa Chadema itakosa uwakilishi katika serikali za mitaa jambo ambalo ni hatari sana kwa ustawi wake.
Nina imani Zitto na maalimu Seif hawatasusia uchaguzi ila watapanga mbinu muafaka za kumkabili mwenzao waziri Jafo kwenye uwanja wa uchaguzi kwani waswahili wanasema.......Waarabu wa Pemba hujuana kwa vilemba.
Leo nimemsikiliza ndg.Polepole akizungumza na waandishi wa habari kwa kweli vyama vya upinzani havina sababu ya msingi kususia uchaguzi kwani makosa yamefanywa kwa uzembe wa wagombea wao wenyewe, na hilo ni fundisho kwa vyama vya upinzani, kuwa wanahitaji elimu ya kutosha. uchaguzi sio lelemama!
Nyasaka hapa jijini Mwanza, mgombea mmoja kwenye fomu zake aliandika kazi yake ni dereva, akaambiwa aweke nakala ya leseni yake ya udereva kumbe hana, ila pia anaishi kwenye nyumba ya kupanga(si mkazi wa eneo hili) nasikia naye ameshindwa kuwa na vigezo jina lake limeondolewa, nauliza kama kaonewa ili nami nijiunge naye tususe kuitambua serikali ya mtaa itakayochaguliwa.
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ametangaza chama chake kutoshiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 24, 2019 kwa madai wakishiriki wanahalalisha ubatili
Maamuzi hayo yanakuja ikiwa ni baada ya Wabunge wa CHADEMA kukutana leo alasiri Novemba 7, 2019 katika Kikao cha Kamati Kuu ya dharura ya chama kilichofanyika mkoani Dodoma
Jana, Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itikadi, Uenezi na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema alisema Kamati hiyo itakutana leo kutoa msimamo wao wa mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
---- WAZIRI JAFO AWASHANGAA
Baada ya Chadema kutangaza kutoshiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa, Waziri wa Tamisemi, Seleman Jafo amesema uamuzi huo unawanyima fursa wagombea wa chama hicho waliopitishwa, waliokata rufaa kupinga kuenguliwa.
Mleta mada na wewe ni kenge mlemavu,badala umshauli mchumia tumbo mwenzio Zitto,ili aonekane ni mpinzani wa kweli,wewe unasema ameokota dodo,hata chama chenu na kiongozi wako Mkuu msipo jitoa,ni wajinga wachache sana mliobaki kama wewe mtaenda kupiga kura.
Waswahili husema kufa kufaana baada ya chama kikuu cha upinzani nchini kujitoa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa kimetoa fursa kwa chama cha ACT wazalendo kuimarika zaidi.
Maana yake ni kwamba kwa sasa Chadema itakosa uwakilishi katika serikali za mitaa jambo ambalo ni hatari sana kwa ustawi wake.
Nina imani Zitto na maalimu Seif hawatasusia uchaguzi ila watapanga mbinu muafaka za kumkabili mwenzao waziri Jafo kwenye uwanja wa uchaguzi kwani waswahili wanasema.......Waarabu wa Pemba hujuana kwa vilemba.
Sasa ndio nimepàta majibu ni kwa nini jimbo LA Chato kuna mtu alikuwa anapita ubunge bila kupingwa kwa miaka 10 mfululizo kumbe mbinu zenyewe ni za kishamba sana.
Hamuwezi siasa za ushindani, na huo upuuzi kupandikiza jiwe ndani vya ccm. Na kwakuwa ccm ilikuwa imechoka kushindana imeona ni sawa huu uhayawani uendelee.
Afadhali, INAKUBALIKA KAMA HUJAJIPANGA, UNA-RETREAT KISHA UNA-REGROUP.....
Hapa nimewapongeza chadema. Sasa mjipange vizuri, mkija hovyo 2020 WATANZANIA watawafyekelea mbali kwenye boks la kura.
Hamuwezi siasa za ushindani, na huo upuuzi kupandikiza jiwe ndani vya ccm. Na kwakuwa ccm ilikuwa imechoka kushindana imeona ni sawa huu uhayawani uendelee.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.