CHADEMA yajiondoa kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Waziri Jafo awashangaa kususia uchaguzi


Sababu hasa ya ccm kuvuruga huu uchaguzi ni ccm kujua idadi ya watu waliojiandikisha ni wachache sana. Hivyo ili kuficha aibu ya watu wachache wameona bora wapitishe wanaccm karibia wote ili kuficha aibu ya watu kususia huo uchaguzi. Kumbuka wanajisifia kuwa wanakubalika, sasa kama wapiga kura watakuwa wachache watatambaje kukubalika?
 
OK good-luck kama unadhani ni jambo ambalo impact zake ni chanya.

Nikuhakikishie pamoja na kelele zote mabeberu nyuma ya pazia pia ni 80% supporters wa Magu mengi anayofanya ndio yale wanayotaka (ukitoa ukandamizaji wa demokrasia, JK alikuwa anachezea financial sanctions kushinda Magufuli; hiyo ni message tosha kama una akili timamu) na 20% iliyobaki ndio kama sehemu ya pressure tu.

Mtabaki hapo hapo kama sio kurudi kwa stahili ya “hewala sio utumwa”

Hata nikikuuliza mafanikio ya kisiasa CDM itakayopata kwa uamuzi huu na tunayapimaje huko mbele I doubt kama unaweza kujibu.
 
Inabidi tuzichape siku 1 afu mpira ukirudi mezani tuanze na sheria (katiba) mpyaaa. Japo tutapoteza ndugu na jamaa zetu, hao watakuwa chachu tu. Kila taifa linaloendelea kuna watu walishamwaga kidogo. Sisi hatujawahi
 
Nadhani viongozi wa chadema wameongeza chuki zaidi baina ya wananchi kuliko ccm,kwa sababu muda wa rufaa huu ungefaa sana kwa mazungumzo kuona kwanini wameenguliwa kuona uhalali na ubatiri na baadae ndo maamuzi yangefuata.
 
Hicho anachokiongea Jafo kinatoka moyoni au machozi ya mamba?
 
CCM ni chama cha siasa au serikali yenye polisi ndani yake?!!!
 

Ni hivi, acha tu kupata support ya hao mabeberu, apate hata ya malaika wa mbinguni who cares. Kama wagombea wako wote wametolewa kwa mizengwe unaendelea kushiriki ili umufurahishe nani? Mpaka sasa hata hicho chama hakiruhusiwi kufanya siasa na kila uchaguzi wanahujumiwa, je impact yao ni ipi? Nani aliyekuambia lazima tupate viongozi tunaowataka kwa box la kura linalohujumiwa wazi wazi? Ni nani aliyekuambia kuwa hicho chama kikorudi nyuma kwa ajili ya dhuluma, basi hao washabiki wa hicho chama automatically watahamia chama cha huyo mkandamizaji? Anzisha chama chako ushirika ili kisonge mbele.
 
Kwenye orodha yako wazee wa busara ni mzee warioba na butiku tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…