CHADEMA yajiondoa kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Waziri Jafo awashangaa kususia uchaguzi

CHADEMA yajiondoa kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Waziri Jafo awashangaa kususia uchaguzi

Mhe. Mbowe anasema kuwa Mkoa wa Dar es Salaam wote wameenguliwa isipokuwa 24 tu, Jiji la Mbeya na Arusha wote wameenguliwa. Kweli?. Kama ni kweli siku ya kura jumla ya watu watakopiga kura hawatafika hata 10% kwa wale watu 19 Millioni waliojiandikisha. Ilikuwa busara wote waingie uwanjaniwote na CCM ingepata 96% kwenye uchaguzi huu. Viongozi mnaosimamia uchaguzi MMEKOSEA SANA. Mtakuja kujuta.

Sababu hasa ya ccm kuvuruga huu uchaguzi ni ccm kujua idadi ya watu waliojiandikisha ni wachache sana. Hivyo ili kuficha aibu ya watu wachache wameona bora wapitishe wanaccm karibia wote ili kuficha aibu ya watu kususia huo uchaguzi. Kumbuka wanajisifia kuwa wanakubalika, sasa kama wapiga kura watakuwa wachache watatambaje kukubalika?
 
Unaongea nini, timu yako zaidi ya 80% ya wachezaji wametolewa tena kwa mizengwe na ww lengo lako ni kushinda, unaendelea kushiriki huo mchezo ili nani afurahi kwa mfano? Ukiona mwanaume anashiriki kwenye mchezo wenye uhayawani wa wazi hivyo ujue huyo ni mpuuzi kama mpuuzi mwingine. Acha huyo anayehujumu uchaguzi aendelee na huo uchaguzi ili heshima yake ipande.
OK good-luck kama unadhani ni jambo ambalo impact zake ni chanya.

Nikuhakikishie pamoja na kelele zote mabeberu nyuma ya pazia pia ni 80% supporters wa Magu mengi anayofanya ndio yale wanayotaka (ukitoa ukandamizaji wa demokrasia, JK alikuwa anachezea financial sanctions kushinda Magufuli; hiyo ni message tosha kama una akili timamu) na 20% iliyobaki ndio kama sehemu ya pressure tu.

Mtabaki hapo hapo kama sio kurudi kwa stahili ya “hewala sio utumwa”

Hata nikikuuliza mafanikio ya kisiasa CDM itakayopata kwa uamuzi huu na tunayapimaje huko mbele I doubt kama unaweza kujibu.
 
Inabidi tuzichape siku 1 afu mpira ukirudi mezani tuanze na sheria (katiba) mpyaaa. Japo tutapoteza ndugu na jamaa zetu, hao watakuwa chachu tu. Kila taifa linaloendelea kuna watu walishamwaga kidogo. Sisi hatujawahi
 
Mbona hujaongelea swala la uadui ambao CCM imepandikiza baina ya raia kwa raia, kwa hili walilofanya safari hii la kujipitisha bila kupingwa tanzania nzima?

Naamini hili halitapotea katika roho za raia wa tanzania milele, na uadui hautakwisha hata baada ya uchaguzi.
Nadhani viongozi wa chadema wameongeza chuki zaidi baina ya wananchi kuliko ccm,kwa sababu muda wa rufaa huu ungefaa sana kwa mazungumzo kuona kwanini wameenguliwa kuona uhalali na ubatiri na baadae ndo maamuzi yangefuata.
 
Hicho anachokiongea Jafo kinatoka moyoni au machozi ya mamba?
 
Kosa kubwa mtakuwa mnajitoa mpaka lini fuateni utaratibu kama mlikosea form kubalini lakini jiandaeni mwaka mwingine.
Huyu alikosea wapi ,je ACT SIO CHAMA KILICHOSAJILIWA NA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA ?
Screenshot_20191107-194045_Twitter.jpg
Screenshot_20191107-194045_Twitter.jpg
 
CCM ni chama cha siasa au serikali yenye polisi ndani yake?!!!
 
OK good-luck kama unadhani ni jambo ambalo impact zake ni chanya.

Nikuhakikishie pamoja na kelele zote mabeberu nyuma ya pazia pia ni 80% supporters wa Magu mengi anayofanya ndio yale wanayotaka (ukitoa ukandamizaji wa demokrasia) na ndio 20% iliyobaki kama sehemu ya pressure tu.

Mtabaki hapo hapo kama sio kurudi kwa stahili ya “hewala sio utumwa”

Hata nikikuuliza mafanikio ya kisiasa CDM itakayopata kwa uamuzi huu na tunayapimaje huko mbele I doubt kama unaweza kujibu.

Ni hivi, acha tu kupata support ya hao mabeberu, apate hata ya malaika wa mbinguni who cares. Kama wagombea wako wote wametolewa kwa mizengwe unaendelea kushiriki ili umufurahishe nani? Mpaka sasa hata hicho chama hakiruhusiwi kufanya siasa na kila uchaguzi wanahujumiwa, je impact yao ni ipi? Nani aliyekuambia lazima tupate viongozi tunaowataka kwa box la kura linalohujumiwa wazi wazi? Ni nani aliyekuambia kuwa hicho chama kikorudi nyuma kwa ajili ya dhuluma, basi hao washabiki wa hicho chama automatically watahamia chama cha huyo mkandamizaji? Anzisha chama chako ushirika ili kisonge mbele.
 
Kwenye orodha yako wazee wa busara ni mzee warioba na butiku tu
Kwanza nieaoongeze sana chadema kwa maamuzi hayo magumu lakini pili jambo hili ni picha ya hatari sana kwa amani na muono wa democracia msichezee .
Nionavyo mimi watu wamechoka na kwasababu wamechoka watakavyoamua hata kama wachache wakafa kaaajili ya kutetea Amani na democracy yanchi tayari watakuwa wameshaichafua nchi.

Itoshe wazee wa busara
Mzee mkapa
Mzee mwinyi
Mzee kikwete
Mzee mangula
Mzee msekwa
Mzee butiku
Mzee warioba
Na wengine wengi watoke mafichoni waseme jambo hili.
Kumbuka wengi wanatamani amani ivunjike na hata miradi ijayo hataweza kutekelezeka.

Viongoz msikubali kamwe kuingizwa katika mtego ambao mnaweza kuuzuia.

Vyama vifuatavyo vyaweza kujiondoa
Ili kufuata chama kilichotangulia
Chadema
Act wazalendo
Cuf

Mwisho sio kila jambo linahitajika ubabe mengine ni diplomasia tu
 
Back
Top Bottom