CHADEMA yajiondoa kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Waziri Jafo awashangaa kususia uchaguzi

CHADEMA yajiondoa kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Waziri Jafo awashangaa kususia uchaguzi

Ambao mnasema mnakubalika angalieni sasa idadi ya watu watakaokwenda kupiga kura! mkimaliza upinzani wa vyama mnaanza upinzani wa ndani ya chama! Then, wanaharakati watasonga mbele bila kujali chochote
 
Tatizo wapinzani wa Nchi hii ni wanafiki sana,utashangaa hao wengine wanaendelea na uchaguzi kama Kawaida.
Sasa vyama vingine ACT, NCCR nk vitangaze kujitoa ili hata upinzani CCM B kama CUF, TLP na UDP vikiungana na mume wao CCM hata wakiendelea shauri yao.
Chadema imefanya vizuri kusubiri hadi hatua hii ili ushahidi wa uzandiki wao uwe wazi
 
Chadema walisusia katiba mpya, hatimae leo wanapata walichokitaka
 
Wamechelewa sana. Tuliwaambia wahimize watu wasijiandikishe, wao wakahimiza waende kujiandikisha. Hawa jamaa sijui kwa nini ni wagumu sana kuona hali halisi.
Wangefanya unavyotaka, wangefutwa na msajili. Hivi walivyofanya ndio sawa, walionyesha nia lakini makando kando yamewaodoa.

Sasa utaona vichekesho, siku ya uchaguzi wasimamizi watawatangaza wagombea wa CHADEMA wameshinda baadhi ya mitaa, na hilo, ccm watalivalia njuga, na kusema kujitoa yalikuwa maamuzi ya Mbowe.
 
Ni vizuri sasa ACT,NCCR,CUF na TLP Nao watoe tamko kususia uchaguzi.
 
That's good decisions

Nothing to care katika huu wanaouita uchaguzi, hii sasa ni kama alert kwamba nin wanatakiwa wafanye against next general election

Jamaa huyu si wakumchekea, anaharibu nchi
Magufuli lazima apatiwe dawa mapema upinzani ulichelewa sana kufanya maamuzi dhidi ya huyu jamaa
Sasa hivi Magufuli ashaota mbawa, kiburi kimemjaa
 
Acha wafurahie walochokipanda maana hawahitaji ushindani wanataka kushinda kwa lazima.
 
Sasa vyama vingine ACT, NCCR nk vitangaze kujitoa ili hata upinzani CCM B kama CUF, TLP na UDP vikiungana na mume wao CCM hata wakiendelea shauri yao.
Chadema imefanya vizuri kusubiri hadi hatua hii ili ushahidi wa uzandiki wao uwe wazi
Well said kuna ushahidi wa kutosha na sababu za kutosha watu kujibu kisasi watakavyo ,kijani hakitavalika mtaani, sitarajii yeyote kushangilia ushindi feki.
 
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ametangaza chama chake kutoshiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 24, 2019 kwa madai wakishiriki wanahalalisha ubatili

Maamuzi hayo yanakuja ikiwa ni baada ya Wabunge wa CHADEMA kukutana leo alasiri Novemba 7, 2019 katika Kikao cha Kamati Kuu ya dharura ya chama kilichofanyika mkoani Dodoma

Jana, Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itikadi, Uenezi na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema alisema Kamati hiyo itakutana leo kutoa msimamo wao wa mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Pia soma

Naona kuna Faida chache na Hasara nyingi kwa CHADEMA Kujitoa katika hizi Chaguzi. Sauti zao za Malalmiko huenda zingesikika kwa uharaka na kupatiwa Ufumbuzi hata Kimataifa. Maamuzi yao haya ni ya Kimhemko, Kimkakati na Kipropaganda zaidi.
 
Back
Top Bottom