CHADEMA yatangaza Kupuuza Tamko la Jeshi la Polisi, Maandamano yako Pale pale

CHADEMA yatangaza Kupuuza Tamko la Jeshi la Polisi, Maandamano yako Pale pale

Tutakuja kuchekwa na wajuu wetu Kwa ushenzi huu tunao uangalia maliasili zetu zikiporwa bila huruma.
Siyo kuchekwa na wajukuu tu, historia ya nchi hii itawatatiza sana vizazi vijavyo na kushindwa kuelewa ilikuwa kuwaje kizazi hiki kilichopo sasa kiliingiwa na ujinga usio elezeka.
Ni kizazi hiki hiki kilitegemewa sana kuiinua Tanzania na kuwa nchi ya heshima kubwa kati ya mataifa mengine, lakini imekuwa kinyume kabisa na mategemeo hayo!

Tuzidi kuweka matumaini kwamba hii CCM chini ya uongozi wa Samia mwisho wake ni hapa 2025, vinginevyo taifa hili litaingia kwenye matatizo makubwa.
 
Masikini wengi wanawaza kula tu
Mtu kama huyo kumjibu ni kupoteza muda wako bure. Huyo ni mnufaika wa hali iliyopo, sasa unategemea aseme nini? Anasema hivyo akifikiria watu wataacha kudai haki zao ili yeye na wenzake waendelee kupata neema ya dhulma zinazofanyika.
 
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo mara baada ya Tamko Batili la Jeshi la Polisi la Kuzuia Maandamano Halali ya Chadema, Mkurugenzi wa Itifaki wa Chama hicho, John Mrema, amesema kwamba Wajibu Pekee wa Polisi kwenye mandamano yoyote ni kuimarisha Ulinzi tu, hawana Mamlaka yoyote ya kuyazuia.

Hii ni kwa Mujibu wa Sheria za Tanzania.

Mrema amedai kwamba, Maandalizi ya Maandamano hayo yanaendelea kama yalivyopangwa yakiwa na lengo la kupaza sauti Dunia nzima ili wote waliotekwa warejeshwe au kama wameuawa kama Ally Kibao basi mifupa yao ikabidhiwe kwa ndugu zao waizike kwa Heshima.

PIA SOMA
- Freeman Mbowe: Tutaandamana kudai watu waliopotea

- News Alert: - Polisi yapiga marufuku maandamano ya CHADEMA yasema ni haramu. Yasema chama hicho kimekuwa kikipanga mikakati ya kuchochea vurugu
Erythrocyte , how do we mitigate the death toll that is in the vicinity? Nina uhakika yale majitu yataua, yataua sana. Ansbert Ngrumo jana nimesoma clip yake inasema wanaotafutwa sasa ni Lema, Lisu Mbowe na Mnyika waondolewe. Watawaskamata na kuwaua/kuwapoteza/kuwaweka ndani na ukatili mwingine kama huo How do we mitigate that?
 
Mtu kama huyo kumjibu ni kupoteza muda wako bure. Huyo ni mnufaika wa hali iliyopo, sasa unategemea aseme nini? Anasema hivyo akifikiria watu wataacha kudai haki zao ili yeye na wenzake waendelee kupata neema ya dhulma zinazofanyika.
sawa mkuu ila nakwambia kwangu Ugali wa watoto ni bora. kwan mwisho wa siku nyie mnavodai si mule? mshibe na watoto wenu Au naongopa. ugali ni bora .kwanza tarehe zenu jau sana kwan 30 huko au 31 . ugali wa watoto ni bora akhaa
 
Hakuna mwana CHADEMA yeyote yule atakaye toa pua yake kuingia barabarani. maandamano yatakuwa Twitter na kuishia huko huko.
Wapuuzi kama nyie ndiyo mnaendelea kuwatia watu hasira, watu wana uchungu kwa watu wao kutekwa na kuuawa wewe unafanya mzaha ni akili hiyo au matope.
 
sawa mkuu ila nakwambia kwangu Ugali wa watoto ni bora. kwan mwisho wa siku nyie mnavodai si mule? mshibe na watoto wenu Au naongopa. ugali ni bora .kwanza tarehe zenu jau sana kwan 30 huko au 31 . ugali wa watoto ni bora akhaa
Wewe fikra zako fupi huko kwenye chakula ndiko zinako ishia. Usifikiri kila mmoja wetu anafikiri kama unavyo fikiri wewe.

Nchi hii ingekuwa na watu wengi wa akili kama yako, leo hii tungekuwa bado tunaye Mwingereza hapa. Sasa tunaye mkoloni mweusi chini ya CCM, kwako bado ni sawa tu.
Nchi hii itakombolewa, na hata nyinyi mtaendelea kuwepo; lakini msififishe jitihada za ukombozi huo. Hapo nanyi mtazolewa kama takataka.
 
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo mara baada ya Tamko Batili la Jeshi la Polisi la Kuzuia Maandamano Halali ya Chadema, Mkurugenzi wa Itifaki wa Chama hicho, John Mrema, amesema kwamba Wajibu Pekee wa Polisi kwenye mandamano yoyote ni kuimarisha Ulinzi tu, hawana Mamlaka yoyote ya kuyazuia.

Hii ni kwa Mujibu wa Sheria za Tanzania.

Mrema amedai kwamba, Maandalizi ya Maandamano hayo yanaendelea kama yalivyopangwa yakiwa na lengo la kupaza sauti Dunia nzima ili wote waliotekwa warejeshwe au kama wameuawa kama Ally Kibao basi mifupa yao ikabidhiwe kwa ndugu zao waizike kwa Heshima.

PIA SOMA
- Freeman Mbowe: Tutaandamana kudai watu waliopotea

- News Alert: - Polisi yapiga marufuku maandamano ya CHADEMA yasema ni haramu. Yasema chama hicho kimekuwa kikipanga mikakati ya kuchochea vurugu
Kikubwa ni kwamba Maandamano ni kwa mujibu wa sheria ya Tanzania, Polisi itabidi wakubali kutoa ulinzi tu, hakuna namna!......Kuwazuia Chadema maandamano halali ni sawa na kurusha jiwe kwenye mzinga wa nyuki.
 
Mchango wa Amani na Utulivu Tanzania

Tanzania imejulikana kama kisiwa cha amani kwa muda mrefu, na kama raia wa taifa hili, tuna jukumu la kudumisha sifa hii. Hivi karibuni, baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakihamasisha maandamano ambayo hayana baraka za Jeshi la Polisi, jambo ambalo linaweza kuhatarisha usalama wa nchi na raia wake.

Kwa mfano, kiongozi wa Chadema, Mr. Godbless Lema, ameonekana kuipeleka familia yake nje ya nchi, akijaribu kuwalinda dhidi ya madhara yanayoweza kusababishwa na maandamano hayo. Huku yeye akibaki kuhamasisha maandamano bila kujali hatari zinazoweza kujitokeza, inatoa picha ya kiongozi ambaye hafikirii madhara kwa raia wengine wa kawaida na familia zao.

Maandamano yasiyo ya amani hayawezi kuleta suluhu yoyote ya kero za kijamii au kisiasa, bali hupelekea vurugu, mali kuharibiwa, na hata kupoteza maisha ya watu wasio na hatia. Tuna wajibu wa kuhakikisha tunazingatia sheria na kuheshimu mamlaka zinazohusika, kama vile Jeshi la Polisi, ambalo lipo kwa ajili ya kulinda amani na usalama wa wananchi.

Tunaweza kushiriki katika mijadala yenye lengo la kuleta maendeleo bila kutumia vurugu. Hivyo, ni muhimu kulaani maandamano yoyote yasiyo halali na kujiepusha nayo. Tuwafundishe watoto wetu thamani ya amani na kuwa mfano wa raia wema kwa kizazi kijacho. Tanzania ni yetu sote, na sote tunalo jukumu la kuihifadhi.
lema famila.jpeg
 
Ukikaa kimya wewe ukasema hayanihusu siku wewe ama mtoto wako ama kaka yako, dada yako, Mama yako, baba yako, bibi yako, babu yako, Shangazi yako, mjomba wako, binamu yako, mjukuu wako, kitukuu chako au hata kilembwe chako siku wakitekwa na kupotezwa nani atawasemea ?

Jirani anapofiwa msiba hauishii tu mlangoni pake bali mtaa mzima ama kijiji kizima tuna shiriki nae kumpa pole.

Utekaji hautaishia kwa wengine tu hata milangoni kwetu utafika ndipo tutakumbuka sauti za watu kututetea na kututia moyo.

Karibu mwezi, miezi inasonga watu kama wakina soka mpaka leo hawajulikani walipo iwe ni wazima ama wameuawa.

Tujitokeze tarehe 23 kesho kupaza sauti zetu Tanzania sio kisiwa cha amani tena ni kisiwa cha utekaji na kunyamazisha watu wenye akili.
 
Friends and Our Enemies,

Nimemskia mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe akihamasisha wafuasi wake eti kesho wajitokeze kwa wingi kushiriki maandamano ya amani na maombolezo.

Kinachostaajabisha zaidi yeye anasema ni amani na maomboleze kisha hapo hapo anatembea na kauli mbiu ya kusema Samia must go..!

Umeshasema must go,amani itokee wapi hapo?

Na wale ambao ni walinda amani ya nchi hii na mali za watanzania wengine ambao siyo wafuasi wa CHADEMA na ambao siyo wafuasi wa wanasiasa wowote unataka wakae kimya wakuangalie?

Hamasisha wafuasi wako ingieni Road kisha tuone mwisho wake.

Shame on you CHADEMA, before hamjafikia hatua ya kusema.Samia must go,mlipaswa kwanza kuanza slogan hiyo na Freeman Mbowe.

Soma Pia:

Mnataka kuonyesha sharubu kisa Samia mwanamke siyo?yule mwanaume mwenzenu mlifyata mikia mkakimbia nchi .
 
Ukikaa kimya wewe ukasema hayanihusu siku wewe ama mtoto wako ama kaka yako, dada yako, Mama yako, baba yako, bibi yako, babu yako, Shangazi yako, mjomba wako, binamu yako, mjukuu wako, kitukuu chako au hata kilembwe chako siku wakitekwa na kupotezwa nani atawasemea ?

Jirani anapofiwa msiba hauishii tu mlangoni pake bali mtaa mzima ama kijiji kizima tuna shiriki nae kumpa pole.

Utekaji hautaishia kwa wengine tu hata milangoni kwetu utafika ndipo tutakumbuka sauti za watu kututetea na kututia moyo.

Karibu mwezi, miezi inasonga watu kama wakina soka mpaka leo hawajulikani walipo iwe ni wazima ama wameuawa.

Tujitokeze tarehe 23 kesho kupaza sauti zetu Tanzania sio kisiwa cha amani tena ni kisiwa cha utekaji na kunyamazisha watu wenye akili.
Umeyaona yanatembea mitaani? Kesho mjipange ndugu zangu
 
Back
Top Bottom