Chalamila: Namuonya Dkt. Slaa aache kupotosha taifa, Bandari haijauzwa

Chalamila: Namuonya Dkt. Slaa aache kupotosha taifa, Bandari haijauzwa

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
1687239434618.png

"Nimeona kwenye mtandao, ndugu yangu balozi Dkt. Wilbroad Slaa na yeye akieleza mambo yake kwenye mtandao, moja ya watu ambao kwa miaka mingi nimewaheshimu, kwa umri wao, kwa nafasi zao, kwa usomi wao ni pamoja na Dkt Wilbroad Slaa.

Sasa na yeye pia nimuonye kwamba kwa umri wake, kwa hadhi yake, sio muda sahihi kutumika kulipotosha Taifa.

Ninamjua kabisa hata yeye anafahamu vizuri kuhusiana na mambo yote ambayo nayaeleza, Tanzania ya dkt Samia Suluhu Hassan anayokusudia kuijenga na aliyoanza kuijenga ni Tanzania yenye umoja.

Na ni Tanzania ambayo kwa mtu yoyote ana azma ya kutaka kufahamu, Serikali imekuwa very polite kwa mtu yeyote anayetaka kuja jambo kwa ufasaha."

Pia soma >
Bandari na DP World: Dkt. Slaa asema ni uuzaji wa Nchi. Adai Serikali iliyopo ina uhalali wa wasiwasi
 
Anamuonya huyo Dr Slaa, akiwa kama nani!! Maana imefikia wakati kila mtu ndani ya ccm anajiona ana mamlaka ya kuwakaripia/kuwafokea/kuwakoromea/kuwatishia nyau watu wengine. Hivi huu ujasiri wanautoa wapi!

Au wanajiona hii nchi ni mali yao, hivyo watu wengine hawana haki ya kuhoji, au kutoa maoni yao?
 
"Nimeona kwenye mtandao Ndugu yangu Balozi Dkt. Wilbroud Slaa akieleza mambo yake katika mtandao. Moja ya watu kwa miaka mingi nimewaheshimu kwa umri wao ,kwa nafasi zao, kwa usomi wao ni pamoja na Dkt. Slaa, Sasa na yeye pia nimuonye kwamba kwa umri wake kwa hadhi yake sio muda sahihi kutumika kulipotosha Taifa, namjua kabisa hata yeye anafahamu vizuri kuhusiana na mambo yote ambayo anayaeleza"
Kapotosha nini? Au kusema ukweli kuwa sio tu bandari zimeuzwa lakini hata reli ya SGR na barabara za kupitisha mizigo ya bandari nazo zimeuzwa
 
nakazia
Anamuonya huyo Dr Slaa, akiwa kama nani!! Maana imefikia wakati kila mtu ndani ya ccm anajiona ana mamlaka ya kuwakaripia/kuwafokea/kuwakoromea/kuwatishia nyau watu wengine. Hivi huu ujasiri wanautoa wapi!

Au wanajiona hii nchi ni mali yao, hivyo watu wengine hawana haki ya kuhoji, au kutoa maoni yao
 
Anamuonya huyo Dr Slaa, akiwa kama nani!! Maana imefikia wakati kila mtu ndani ya ccm anajiona ana mamlaka ya kuwakaripia/kuwafokea/kuwakoromea/kuwatishia nyau watu wengine. Hivi huu ujasiri wanautoa wapi!
Mkuu wa Mkoa ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama Mkoa.

Hili hulijui au unajilazimisha kulisahau kwa ushabiki?
 
Kiki kikini hakuna haja ya kutishiana Slaa amejenga hoja kwamba bandari umeuzwa wewe Lete hoja yako kwamba bandari haijauzwa wananchi tuzipime ndio demokrasia inataka hivyo.
 
"Nimeona kwenye mtandao Ndugu yangu Balozi Dkt. Wilbroud Slaa akieleza mambo yake katika mtandao. Moja ya watu kwa miaka mingi nimewaheshimu kwa umri wao,kwa nafasi zao, kwa usomi wao ni pamoja na Dkt. Slaa, Sasa na yeye pia nimuonye kwamba kwa umri wake kwa hadhi yake sio muda sahihi kutumika kulipotosha Taifa, namjua kabisa hata yeye anafahamu vizuri kuhusiana na mambo yote ambayo anayaeleza"
Ni vzr wana CCM wajifunze kupangua hoja za watanzania kwa hoja, vitisho havisaidii wala sio majibu kwa Slaa!! NB; CCM jikiteni kweny kujibu hoja kwa kauli hiz mnaonyesha udhaif wa kujenga hoja!!
 
Anamuonya huyo Dr Slaa, akiwa kama nani!! Maana imefikia wakati kila mtu ndani ya ccm anajiona ana mamlaka ya kuwakaripia/kuwafokea/kuwakoromea/kuwatishia nyau watu wengine. Hivi huu ujasiri wanautoa wapi!

Au wanajiona hii nchi ni mali yao, hivyo watu wengine hawana haki ya kuhoji, au kutoa maoni yao?

Kama RC wa Bandari Salama😎
 
Mkuu wa Mkoa ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama Mkoa.

Hili hulijui au unajilazimisha kulisahau kwa ushabiki?
Usianike ujinga kweny public!! Slaa kaleta uvunjifu wa amani? Jifunzeni kujibu hoja kwa hoja vitisho sio jibu la mtoa hoja!!!
 
Back
Top Bottom