Kama ameyasema hayo, basi Chalamila atakuwa na upunguani.
Yeye Chalamila amuonye Dr Slaa kama nani, na kwa mamlaka gani? Angekuwa na busara japo kidogo asingetumia neno kuonya, angetumia neno, 'namshauri'.
Rais Samia watakaomganya achukiwe na hawa wasaidizi waje waliokosa busara. Kwenye hili suala la mkataba wa DP, Rais Samia asipowapata wenye busara, litamharibia sana. Na akiharibikiwa, hawa ndumila kuwili alio nao, watamgeuka na kuanza kumshambulia.
Mpaka sasa Rais Samia, namwona ameamua kufuata busara kwa kukaa kimya bila shaka akitafakari na kupima upepo unavyoenda. Sasa kushindwa kwake au kufaulu ni siku atakapolitolea ufafanuzi jambo hili. Itayegemea ameamua kufuata ushauri wa watu gani, waropokaji au wenye hekima.
Kwa upande wa viongozi, mpaka sasa kiongpzi pekee aliyetoa kaulo yenye busara ni Majaliwa pekee yake.