Changamoto za kutokuwa na mtoto wa kiume kwenye familia

Changamoto za kutokuwa na mtoto wa kiume kwenye familia

Hizo facts, mimi sijazipinga na wala sio mjadala wa msingi.

Mjadala wa msingi ni kwamba mwanamke haendelezi kizazi cha asili alichotoka, ila anakiua mara baada ya yeye kuzaa. Mwanamke haendelezi familia/koo aliyotoka, anaendeleza familia ya yule anaemzalia. Mwanamke kibailojia ana yai na hana mbegu. Mwenye mbegu ni kiumbe kingine cha kiume. Ukisema tamaduni haizingatii sayansi ni kuidunisha tamaduni.

Nimekuuliza huko juu, wewe ukizaa na binti wa Dangote, mtoto wako atakuwa ni koo/familia ya Dangote? Atajiita Dangote? Hujanijibu.

Usichanganye mambo; Muhammad Ally alibadili majina yake kwa sababu alislimu kutoka ukristo kuja uislamu. Ally hakuikana koo/familia wala hakuikana jinsia yake ya kiume.
Hoja zako ni kama za mtu mwenye IQ chini ya 70.
 
Na problem ikawa na wa kike wakawa malaya tu utafungua danguro?
Wangu mmoja alipigwa Mimba mapema tu kamaliza chuo,
Mwingine nae akawa mwizi tu,tumemtoa selo nikamrudisha kwao huko magu.
Balaa lipo tu
Aseee umenitisha mana nina mtoto huko magu
 
Ipo hivi tajiri.
Mtoto wa kike sio wako. Ni wako tuu kumkuza, kumlea na kumpa maadili, kumlea kiroho na mwanzo wa maisha kumuandaa kuwa mke wa mtu mwingine, ambako atatawaliwa na kutumikishwa.

Kaa ukijua unawaandalia wajuba wake zao.

Akiolewa anaenda tengeneza mji mwingine, uwe umemsomesha au umempa mali. Anakwenda jenga mji wa wengine na watanufaika nae huko na yeye kuwa mwanaukoo wa huko.

Mtoto wa kike haendelezi ukoo/familia/jina la ukoo wako, hana jina, hilo jina lako la ukoo ulilompa mfano Shirima ni geresha tuu, akiolewa na Mushi, anabadiri kuanza kuitwa Mushi. 😁

Mtoto wa kike, atamjali mama yake hata akija kuwa na mji wake au kazi yake, mama yake ataangaliwa sana kuliko wewe, hasa nguvu zako zikiisha yaani uzeeni. Angalia familia nyingi mama akifa, watoto wa kiume ndio wanabaki na mshua wao.

Mtoto wa mtoto wa kike (Mjukuu) sio wako, huna haki nae atakapo kuwa mkubwa, huwezi kumrithisha wala kuwa na maamuzi nae, wala hatabsikiliza neno lako, utakuwa babu tuu wa yeye kuja kunufaika na mali zako na kutembea. Wala hawezi jenga mji wala kuendeleza uzao/jina lako. Mjukuu wa kiume mwenye akili atakuwa na uchungu na babu, maana ndie damu yake, patakuwa panamuuma.

Swai hawezi kuja kujenga kwa akina Laswai, ni watu tofauti hawa, hawa kwa mwanaume hawa kwa mwanamke. Huwezi kujenga ujombani jomba, uliona wapi hiyo bwashee, unajenga ubabani. Ubabani ndio kuna kuhusu bwashee. 😁

Utaishi maisha ya upweke sana uzeeni, hutakuwa na right-hand men wa kukusaidia, kuongea nao, kukulinda, kukushauri kiume, kuwapa siri zako na mbinu zako za kuishi ili kuendeleza mali na ukoo.

Hutakuwa na warithi kisheria. Mwisho wa siku mali hizo zitaenda kwa wengine kupitia "chupi" yaani mtoto wa kike anachukua mali kwao na kuwapa watoto wake ambao sio wanaukoo.

Hutakiwa na "succession plan" ya mali, kizazi na mipango yako. Ukifa watu wanagawana fito. Watoto wa kiume watakomaa kuendeleza legacy yako. Mali, kampuni, hisa n.k

Wajukuu wa mtoto wa kike, hawatakuheshimu na kukupa uzito uzeeni kama babu yao, achilia mbali kukutunza. Watamtunza babu hao mzaa baba ambae ni "maternal grandparents" wanaitwa jina lake na wanaweza kumrithi, kiafrika babu mzaa baba anarithisha mali kwa wajukuu zake wa kiume.

Hutaweza kuwapa jina watoto wa mtoto wa kike. Achilia mbali kupewa kitovu chake wala kumfisha akifa.

Mtoto wa kike akifa, wewe unaenda msibani kama jirani, atazikwa ukweni na jina lake litaandika la mumewe. Kam unakaa kijiji A, utalazimika kwenda kijiji B kuzika mwanao, ukifika hapo utapewa jina la baba wa mwanamke, mkwe, mkamwana. Na majina mengine ya kukutenga.

Nyumbani kwa mtoto wa kike, utaenda kama mgeni kusalimia na hutaruhusiwa kukaa hapo, hata mkweo akiwa mwema vipi. Hutajisikia amani na uhuru wewe kukaa hapo. Kwa mtoto wa kiume ni kwako, na unaweza kaa hapo kwa amani maana utakuwa upo kwa mwanao yaani kitovuni kwako.

We umezidi kumkata maini
 
Una mawazo ya kipindi cha Zama za mawe: Mtoto ni mtoto tu, hayo mambo ya kurithi sijui ujinga wa jina hayana maana yoyote ni mawazo ya ki ujima tu. Unaweza kuta unamilik labda nyumba tu, sasa jilinganishe na kina Barack Obama - 2 wa kike au Bill Clinton 1 wa kike ambao ni mabillionaire na wapo pouwa tu.
 
Una mawazo ya kipindi cha Zama za mawe: Mtoto ni mtoto tu, hayo mambo ya kurithi sijui ujinga wa jina hayana maana yoyote ni mawazo ya ki ujima tu. Unaweza kuta unamilik labda nyumba tu, sasa jilinganishe na kina Barack Obama - 2 wa kike au Bill Clinton 1 wa kike ambao ni mabillionaire na wapo pouwa tu.
Acha nyege. Njoo nikutie mimba basi unizalie dume.

Pumbavu.
 
Back
Top Bottom