Changamoto za kutokuwa na mtoto wa kiume kwenye familia

Tajiri, Aliko Dangote kaasili mtoto wa kiume baada ya kumkosa! Amemkosa mtoto wa kiume imebidi afanye "adoption" kwa lengo hilo hilo la "succession plan". Dangote anahofia kupoteza mali, au kuhamisha mali.
Juu hapo umesema kumpa mali mtoto wa kike ni kutupa mali kwenda kizazi kingine ambacho si chako kwa damu, umetumia neno bloodline.

Kwa hivyo unamaanisha kusema kuwa mtoto wa kike si damu yako?

Unaelewa bloodline maana yake nini?

Unaelewa kuwa bloodline haijali mtoto wa kike au kiume?

Unaelewa huyo mtoto wa Dangote wa kiume aliyeasiliwa hana bloodline? Amekuwa mtoto kwa kuasiliwa tu?

Unaelewa watoto wa kike wa Dangote wana bloodline ila wa kiume wa kuasiliwa hana bloodline?

Unaelewa ukimbagua mtoto wa kike kwa sababu ya bloodline (ambayo anayo) halafu uka support mtoto wa kiume aliyekuwa adopted ambaye hana bloodline, hapo unajionesha wewe huna shida ya bloodline, hapo shida yako ni kubagua watoto wa kike tu?
 
Matusi kwa mtu unayetofautiana mtazamo sio njia sahihi ya kujenga hoja.

Kila mtu ana mtazamo wake kutokana na jamii tulizopo. Kumbuka, hata kama dunia ni kama kijiji lakini jamii zetu haziwezi kuwa sawa.

Kwa jamii niliyopo watoto wa kike hawana msaada kwenye familia walizotoka zaidi ya kuwa wabinafsi na kuwapigania watoto wao. Tofauti na wanaume ambao naona wanasupport wenzao
Ujinga, Upumbavu na Ujima sio matusi.

Duniani kote katika jamii zote kuna baadhi ya mitazamo ya kijamii ni ya kijinga na kipumbavu, mfano Marekani ni lazima utoe tip kwa muhudumu ukila mghawani au bar, huo ni mtazamo wa kijinga na kipumbavu.

Tukirudi kwenye mada,
Samia hana msaada kwenye familia aliyotoka?
Ruth Zaipuna-NMB CEO hana msaada kwenye familia aliyotoka?
Fatma Abdallah- PUMA CEO hana msaada kwa familia aliyotoka?
Diamond ana msaada gani kwa baba yake?
 
Kama lengo la mali, utajiri na ufahari sio kuendelea kuwepo kwenye "Bloodline" basi leo kuna matajiri wakubwa Afrika usingewajua, akiwemo huyo Dangote, Mo Dewji, Yaseen and Yousef, Motsepe.
Kwemye 29 bora ya matajiri Afrika, seelf made billionaires Afrika hawazidi watano, ukimtoa Strive Masiyiwa.
Hao akina Dewji, Oppenheimer, Ruppert, Sawiris wa Egypt ni matokeo ya urithi unaotokana na Bloodline.

Watu mababu zao wamefika South Afrika 1880, leo ndio matajiri hapo South Afrika. Unawezaje kusema utajiri sio Bloodline??
Acha kuleta historia ndefu zisizo na mashiko, niambie nani alisema au aliweka sheria kwamba lengo la mali, utawala na ufahari ni kuendelea kuwepo kwenye bloodline.
 
Ujinga, Upumbavu na Ujima sio matusi.

Duniani kote katika jamii zote kuna baadhi ya mitazamo ya kijamii ni ya kijinga na kipumbavu, mfano Marekani ni lazima utoe tip kwa muhudumu ukila mghawani au bar, huo ni mtazamo wa kijinga na kipumbavu.

Tukirudi kwenye mada,
Samia hana msaada kwenye familia aliyotoka?
Ruth Zaipuna-NMB CEO hana msaada kwenye familia aliyotoka?
Fatma Abdallah- PUMA CEO hana msaada kwa familia aliyotoka?
Diamond ana msaada gani kwa baba yake?
Unaniuliza maswali kwa watu nisiowafahamu unataka nikujibu nini?

Mimi nakuelezea mtazamo wangu na jamii zetu zilivyo.

Ukienda kwa wahindi utakutana na jamii ya wanawake kulipia wanaume mali.

Hatuwezi kuwa sawa mitazamo. Na kutofautiana mitazamo sio ujinga wala upumbavu
 
Nina uhakika hata katika jamii yetu au yako inayokuzunguka unawajua watoto wengi tu wa kike walio na msaada kwa familia zao walizozaliwa kuliko watoto wa kiume kwenye hizo familia, pia unawajua watoto wengi wa kiume wasio na msaada wowote katika familia walizozaliwa.
Ninarudia tena kuna mitazamo ni ya kijinga na kipumbavu na inapswa kupuuzwa.
 
Kwenye jamii yangu watoto wa kike hawana msaada kwenye familia walizotoka zaidi ya kugombea mali na kuzipeleka walikoolewa.

Huenda hii imesababishwa na utamaduni wa kumpa haki zote mtoto wa kiume hivyo wanaogopa endapo wao hawatakuwepo, watoto wao hawatakua na haki kwenye mali za wazazi wao.

Kwa upande wa watoto wa kiume, ni kweli wapo ambao hawana msaada lakini kwa asilimia kubwa nimeona wanalea na kusupport mpaka watoto wa dada zao au kaka zao ambao wameshatangulia mbele za haki
 
Nani alisema lengo la mali, utawala na ufahari ni kuendelea kuwepo kwenye bloodline??

Kwa sababu huna uelewa wowote kuhusu elimu ya urithi na mirathi. Ungekuwa walau elimu kidogo tuu ya mambo hayo ungeekewa mantiki ya hao wanaotaka mtoto wa kiume kulingana na mfumo uliopo.

Family ni smallest unit ya Taifa au jamii Fulani.
Kama unavyoona mataifa yanapigania maslahi ya nchi zao kwa mustakabali wa vizazi vijavyo ndivyo mtoa mada anavyoeleza kuhusu yeye kutokuwa na mtoto wakiume inamaanisha yeye ukoo wake utakufa na jina lake litakufa.

Ni kama vile Iran hataki kutawaliwa na mmarekani alafu litokee lijinga kama wewe liseme kwani wakitawaliwa kuna tatizo gani

Kwenye familia na ukoo. Mwanaume ndiye anaongeza ukoo. Ukizaa watoto wakike unazalia ukoo mwingine.

Unaposikia mjerumani, muingereza, mmarekani, mchina Yote hayo chimbuko lake ni Familia yaani mke na mume.

Hao kina Obama na wengine uliowataja waliozaa watoto wakike. Habari Yao ndio imeishia hapo.
Mabinti zao wakiolewa na waarabu au waafrika watachukua majina na umiliki wa upande wa Baba zao.

Ni muhimu kuchanganya watoto na inafurahisha lakini haimaanishi kwamba ukikosa ndio ujiue
 
Acha kuleta historia ndefu zisizo na mashiko, niambie nani alisema au aliweka sheria kwamba lengo la mali, utawala na ufahari ni kuendelea kuwepo kwenye bloodline.

Hakuna mtu anatafuta mali ili iishe, kila mtu anatafuta mali ili iendelee kuwepo kwa vizazi na vizazi. Hakuna mtu kaweka sheria juu ya hilo. Ndio maana leo unaona kuna matajiri wanatokana na urithi na uendelezaji wa mali.
 
"Unaelewa watoto wa kike wa Dangote wana bloodline ila wa kiume wa kuasiliwa hana bloodline?"
Ndio naelewa.

"Kwa hivyo unamaanisha kusema kuwa mtoto wa kike si damu yako?"

Mimi, hoja yangu ni kwamba, hao mabinti w Dangote, hawatazaa watoto wakawa ni "Dangote's". Wewe Kiranga, ukienda kumuoa binti wa Dangote, watoto wako na binti huyo hawaiitwa Dangote's. Wataitwa Kiranga. Pamoja na privileges wanazoweza kuzipata kwa mama yao kuwa ni familia ya Dangote, bado wewe hao watoto wako watakuwa sio Dangote's.

Nyongeza: Mpaka Dangote kafanya "adoption" ya mtoto wa kiume, maana yake kashindwa kupata mtoto wa kiume kwa njia ya kibailojia. Kuna hitaji analo Dangote hapo. Na sio mbaguzi, wala mjinga.

Hizo surrogate, adoption ni njia za kupata watoto kisheria nje ya kibailojia. Huyo mtoto Dangote sio "biological father" wake.
Umejiweka katika utumwa wa dhana za kiutamaduni tu ambazo zinabadilika kwa wakati na pahala, dhana kama mtoto ni wa kiumeni, mtoto ni lazima aitwe jina la baba, na mambo mengine kama hayo ambayo ni arbitrary.

Kuna watoto wanaitwa majina ya upande wa mama. Wamakua hawa kina Mkapa wanaitwa majina ya uoande wa Mama zao kiasiki. Mkapa ndugu zake wamemuhoji mbona yeye kabadilisha tamaduni zao kajiita jina la baba yake, ni kwa sababu ya usomi tu uliobadikisha tamaduni zao matrilinear.

The Makuas and Yaos are matrilinear societies, zipo nyingi tu Affica.

Kuna tamaduni kabisa kama za Wahispania mtoto anapewa majina ya pande zote mbili.

Na umeacha kitu cha msingi ambacho hakibadilishwi na tamaduni hizi za kuungwaungwa na watu tu.

Umeacha kitu cha msingi kabisa, genetivs, hiyo bloodline. Mtoto wa kike kama wako ni wako tu, kibaiolojia ana genes zako.

Umeacha kitu cha msingi kama meritocracy.

Hivi ukiwa na mtotonwa kiume asiye na uwezo unajua kabisa huyubteja tu hawezi juendesha kampuni, na mtoto wa kike kasoma vi,uri anaweza kuendesha mambo vizuri, bado utampa kampuni mtoton wa kiume kwa sababu yeye ni wa kiume?

You are majoring in the minors.

Unafanya mambo ya kutungwa tungwa na watu tu yanayoweza kubadilishwa vyovyote unavyotaka wewe yawe kama kanuni za fizikia ambazo haziwezi kubadilishwa.

Dangote ni mfano kwamba Africa hata ukiwa bilionea ni vigumu sana kupita tamaduni za kumdogosha mwanamke.
 
Naheshimu mawazo yako, japo siyakubali. Naomba nibaki na mtazamo wangu, kwamba mwanamke haendelezi ukoo/familia. Anaendeleza kule anakoolewa, kwa mantiki hiyo, mwanamke kurithi mali ni kuipoteza/kuihamisha kwenda kwenye familia/koo zingine, huku koo yako ikiwa imeishia hapo.

Nje ya mada: Hata hivyo, nakupongeza kwa ustaarabu wako kwenye mijadala.
 
Na problem ikawa na wa kike wakawa malaya tu utafungua danguro?
Wangu mmoja alipigwa Mimba mapema tu kamaliza chuo,
Mwingine nae akawa mwizi tu,tumemtoa selo nikamrudisha kwao huko magu.
Balaa lipo tu
 
Naheshimu mawazo yako, japo siyakubali. Naomba nibaki na mtazamo wangu, kwamba mwanamke haendelezi ukoo/familia. Anaendeleza kule anakoolewa, kwa mantiki hiyo, mwanamke kurithi mali ni kuipoteza/kuihamisha kwenda kwenye familia/koo zingine, huku koo yako ikiwa imeishia hapo.

Nje ya mada: Hata hivyo, nakupongeza kwa ustaarabu wako kwenye mijadala.

Ustaarabu is overrated. Sometimes we need to be brutally honest. As long as we are truthful.

Kuhusu mada.

Haya si mawazo yangu tu. Ukisema kuwa ni mawazo yangu, unadogosha hoja kama ni mtazamo mmoja tu wakati mimi nakupa facts, logic na reason.

Hizi ni facts.

Kwamba hizi ni tamaduni ambazo watu wamejiwekea tu na zinaweza kubadilika ni fact.

Kwamba mtoto wa kike na wa kiume wote ni watoto wako is a fact.

Kwamba mtoto wa kike anaweza kuwa na uwezo sawa na wa kiume, au hata kumpita, kwa kutegemea na maandalizi na jamii, that is a fact.

Kwamba mtoto wa kike anaweza kuwa na jina lolote analotaka, that is a fact.

Mwananke anaweza kuwa na jina lolote analolitaka. Hata mwanamme anaweza kuwa na jina lolote analolitaka.

Muhammad Ali hakuzaliwa Muhammad Ali. Alizakiwa Cassius Clay.

Akakua, akajitambua zaidi, akasema hili jina la Cassius Clay ni jina la kitumwa silitaki. Kuanzia leo nitaitwa Muhammad Ali.

Leo jina la Muhammad Ali ni maarufu kuliko Cassius Clay.

Sasa kwa nini watu wanafanya kama mtu hawezi kuamua kuwa na jina lolote analolitaka?

Hakuna sheria ya kiasili kama ya fizikia inayo zi support tamaduni hizi.

That is a fact.

Na kwenye logic kufanya kitu kwa sababu ni utamaduni tu ni logical fallacy.

Argument from tradition.

Your entire objection, entire position, entire logic, is based on a logical fallacy.

Argument from tradition logical fallacy.
 
Hizo facts, mimi sijazipinga na wala sio mjadala wa msingi.

Mjadala wa msingi ni kwamba mwanamke haendelezi kizazi cha asili alichotoka, ila anakiua mara baada ya yeye kuzaa. Mwanamke haendelezi familia/koo aliyotoka, anaendeleza familia ya yule anaemzalia. Mwanamke kibailojia ana yai na hana mbegu. Mwenye mbegu ni kiumbe kingine cha kiume. Ukisema tamaduni haizingatii sayansi ni kuidunisha tamaduni.

Nimekuuliza huko juu, wewe ukizaa na binti wa Dangote, mtoto wako atakuwa ni koo/familia ya Dangote? Atajiita Dangote? Hujanijibu.

Usichanganye mambo; Muhammad Ally alibadili majina yake kwa sababu alislimu kutoka ukristo kuja uislamu. Ally hakuikana koo/familia wala hakuikana jinsia yake ya kiume.
 
Au unataka kutuaminisha pia kwamba familia/koo na yenyewe ni mambo ya kitamaduni?

Usichanganye mambo; Muhammad Ally alibadili majina yake kwa sababu alislimu kutoka ukristo kuja uislamu. Ally hakuikana koo/familia wala hakuikana jinsia yake ya kiume.
Habari nzima ya mwanamke haendelezi kizazi chake cha asili alichokikuta ni utamaduni tu, ni arbitrary, ni ujinga tu.

Mwanamke ndiye anayebeba mimba kwa miezi tisa takriban, utasemaje haendelezi kizazi chake cha asili?

Kwanza kabisa, namna nzuri kabisa ya kumjua nani ni mtoto wa nani ni kuangalia mama gani kazaa mtoto gani.

Hizi habari za baba kusema huyu ni mwanangu wa kiume, kama hajapima DNA, which is the case for more than 99% of the cases, baba hana uhakika hata huyo mtoto wa kiume anayesema ni wake ni wake kweli.

Lakini mama tunamuona ana mimba, tunamuona anazaa, tunamuona mtoto kazaliwa na mama.

Sasa hapo unajimwambafy sana vipi kuwa mtoto ni wa mwanamme wakati 99% ya watu hata kupima DNA hampimi na wengi wa hao mnaowaita watoto wenu wa kiume kibaiolojia hata si wenu?

Mwalimu Julius Nyerere alikuwa anaelezea mila za Wazanaki, akasema Wazanaki mtoto harithi mali za baba, anarithi mali za mjomba, kaka wa mama. Kwa sababu wameelewa kuwa uhakiki wa nani ni mtoto wa nani kwa upande wa baba ni mgumu sana, hususan miaka hiyo ya kabla ya DNA. Na uhakiki wa nani ni mtoto wa nani kupitia mama ni rahisi zaidi, kwa sababu tunamuona mama anazaa na tunaweza kuhakiki mtoto huyu ni wa mama huyu mpaka anakua.

Kwa hivyo hata hao watoto mnaosema wenu wanaume, bila kupima DNA, mnajuaje ni watoto wenu kweli?

Nimekueleza hapo juu mtu yeyote ana uhuru wa kuamua ataitwa vipi, na mtu atakayeamua kuzaa na binti wa Dangote anaweza kuamua kuwa mtoto awe wa ukoo wa Dangote. Huo ni uamuzi wao. Hakuna sheria ya kifizikia inayosema mtoto lazima awe wa ukoo wa mwanamme.

Nimekuambia wa Spanish mtoto anabeba majina yote ya baba na mama, wewe huijui dunia tu.

Sasa kama Muhammad Ali kabadilisha jina kwa ajili ya dini, akachukua jina ambalo hata halipo katika ukoo wake, mtu atakayezaa na binti wa Dangote utamkatalia vipi kuamua kuchujua jina la upande wa mama yake, Dangote?

Mbona kama huelewi kuwa hizi ni tamaduni zlkizowekwa na watu tu na tunaweza kuzikataa kama tunaona zimepitwa na wakati?

Mbona unakumbatia sana logical fallacy ya "argument from tradition"?

Unaelewa logical fallacy ni nini?

Unaelewa "argument from ttadition" ni nini?

Unaelewa "argument from tradition" ni logical fallacy?
 
Habari nzima ya mwanamke haendelezi kizazi chake cha asili alichokikuta ni utamaduni tu, ni arbitrary, ni ujinga tu.

Mwanamke ndiye anayebeba mimba kwa miezi tisa takriban, utasemaje haendelezi kizazi chake cha asili?

Kwanza kabisa, namna nzuri kabisa ya kumjua nani ni mtoto wa nani ni kuangalia mama gani kazaa mtoto gani.

Hizi habari za baba kusema huyu ni mwanangu wa kiume, kama hajapima DNA, which is the case for more than 99% of the cases, baba hana uhakika hata huyo mtoto wa kiume anayesema ni wake ni wake kweli.

Lakini mama tunamuona ana mimba, tunamuona anazaa, tunamuona mtoto kazaliwa na mama.

Sasa hapo unajimwambafy sana vipi kuwa mtoto ni wa mwanamme wakati 99% ya watu hata kupima DNA hampimi na wengi wa hao mnaowaita watoto wenu wa kiume kibaiolojia hata si wenu?

Mwalimu Julius Nyerere alikiwa anaelezea mila za Wazanaki, akasema Wazanaki mtoto harithi malinza baba, anarithi mali za mjomba, kaka wa mama. Kwa sababu wameelewa kuwa uhakiki wa nani ni mtoto wa nani kwa upande wa baba ni mgumu sana, hususan miaka hiyo ya kabla ya DNA. Na uhakiki wa nani ni mtoto wa nani kupitia mama ni rahisi zaidi, kwa sababu tunamuona mama anazaa na tunaweza kuhakiki mtoto huyu ni wa mama huyu mpaka anakua.

Kwa hivho hata hao watoto mnaozema wenu wanaume, bila kupima DNA, mnajuaje ni watoto wenu kweli?

Nimekueleza hapo juu mtu yeyote ana uhuru wa kuamua ataitwa vipi, na mtu atakayeamua kuzaa na binti wa Dangote anaweza kuamua kuwa mtoto awe wa ukoo wa Dangote. Huo ni uamuzi wao. Hakuna sheria ya kifizikia inayosema mtoto lazima awe wa ukoo wa mwanamme.

Nimekuambia wa Spanish mtoto anabeba majina yote ya baba na mama, wewe huijui dunia tu.

Sasa kama Muhammad Ali kabadilisha jina kwa ajili ya dini, akachukua jina ambalo hata halipo katika ukoo wake, mtu atakayezaa na binti wa Dangote utamkatalia vipi kuamua kuchujua jina la upande wa mama yake, Dangote?

Mbona kama huelewi kuwa hizi ni tamaduni zlkizowekwa na watu tu na tunaweza kuzikataa kama tunaona zimepitwa na wakati?

Mbona unakumbatia sana logical fallacy ya "argument from tradition"?

Unaelewa logical fallacy ni nini?

Unaelewa "argument from ttadition" ni nini?

Unaelewa "argument from tradition" ni logical fallacy?

Wewe kuchukulia "Traditional argument" kama logical fallacy, namna yako unavyotazama mambo "point of view" na sio jambo baya ni mtazamo tuu na nauheshimu.

Swali lako kwamba "Mwanamke ndiye anayebeba mimba kwa miezi tisa takriban, utasemaje haendelezi kizazi chake cha asili?".

Nimeshakujibu, kuhusu hili huko juu, kwamba kisayansi mwanamke hana mbegu ana yai. Mbegu inatunzwa na kuzalishwa kutoka katika kiumbe cha kiume. Hii sio tamaduni ni sayansi. Kwa mantiki hiyo, mwanamke anapokea mbegu toka kwa kiumbe cha kiume, mwanamke ni mapokeo ya mbegu. Mwanaume ndiye mwenye mbegu hiyo, ndipo fact ya kuendeleza "Asili/Ukoo/familia" inapozaliwa.
Mwanamke anapewa mbegu azae mtoto, ni mchakato wa kisayansi.
Ndio maana tamaduni haiwezi ruhusu Mbegu ya Kiranga, mtoto azaliwe aitwe Dangote. Ataitwa Kiranga mwenye mbegu ile. Huyo mzaliwa kuwa na haki ya kujiita atakavyo, hakuindoi fact kwamba asili yake ni Kiranga. Usiibeze tamaduni wakati inaakisi sayansi.

Tamaduni ni matokeo ya sayansi/nature. Tamaduni inatambua jinsia ME na KE, upatikanaji wa jinsia ni sayansi/nature, tamaduni ikatambua hilo, ikatoa utaratibu na majina ya jinsia na asili ya mtu. Kwanini tamaduni ionekane haina fallacy kwenye eneo hili, wakati imeakisi sayansi?

"Mbona kama huelewi kuwa hizi ni tamaduni zlkizowekwa na watu tu na tunaweza kuzikataa kama tunaona zimepitwa na wakati?"

Tamaduni kwamba mwanamke sio mwendelezaji wa kizazi chake cha asili, haiwezi kupitwa na wakati. Tamaduni haiwezi kupitwa na wakati, tamaduni ni matokeo ya nature/sayansi. Tunaweza ikataa tamaduni kwenye baadhi ya mambo, lakini tukaikubali kwenye mambo mengine.

Tamaduni hii inaakisi sayansi inayotuambia kwamba, mwanamke ana yai, mbegu anategemea kiumbe kingine cha kiume. Hii ni fact ya kisayansi.

Kuhusu kujua mtoto ni wa nani; Njia zote za kisanyansi na kitamaduni zinatumika na zina matokeo ya uhakika. Ni suala dogo sana hilo kitamaduni.
 
Back
Top Bottom