Changamoto za kutokuwa na mtoto wa kiume kwenye familia

Changamoto za kutokuwa na mtoto wa kiume kwenye familia

Hujui unachosema, Hawa wote waliachiwa urithi na baba zao na wanazo pesa za kuwabadilisha jina la ukoo wanaume wote kwenye ukoo wenu.
1.Alice Walton,
2.Françoise Bettencourt Meyers
3.Julia Koch
4.Ann Walton Kroenke
5.Jacqueline Mars
6.Abigail Johnson
7.Gina Rinehart

Yoda, mbona unawataja wazungu tuu! Waafrika huwataji wala kuwasemea.
 
Ni utamaduni tu unakusumbua, kuna mabilionea wengi duniani ambapo hata wewe ukipewa maisha ya miaka elfu moja hutakaa uweze kupata hata 1% ya pesa walizo nazo na bado wao hawana wototo kabisa, sio hata hao wa kike ambao nyie mnaona sio watoto kamili.
1.Klaus-Michael Kühne
2.Walter P.J. Droege
3.Ma Jianrong
4.Reid Hoffman
5.Pang Kang
6. Oprah Winfrey
7. Alice Walton
Wote hawa ni mabilionea$ na hawana watoto.
Siku yamaziko wanatiwa kijinga chamoto sehem zasiri
 
Mimi nadhani mtoa mada yupo sahihi kulingana na utashi wake.....

Katika uhalisia wa nafsi ya mwanadamu kila mmoja huwa na matamanio juu ya jambo fulani katika kukamilisha furaha au lile analoona ni sahihi kwake.....

Tofauti yake yeye na Sisi hapa jukwaani ni kwamba yeye kaamua kuyaweka bayana matamanio ya nafsi yake na sio kubakia nayo kifuani mwake!!!

Anaweza kuwa sahihi au asiwe sahihi kulingana na jinsi ambavyo kila mtu alivyolipokea hapa jamvini...lakini ukweli ni kwamba mwanadamu hana ukomo wa matamanio na hafanyi jambo pasi na matarajio!!!

Mimi sina cha kumshauri huyu bwana kwa kuwa sina ninalolijua kuhusu namna ya kupanga au kufanya ili upate mtoto unayemtaka.....lakini kilichonivutia zaidi kutoa mchango ni namna ambavyo baadhi ya wadau walivyolipokea swala hili la huyu ndugu yetu!!!

Kusema ukweli sasa hivi JF imepotelewa na michango ya hekima na yenye kujenga.....JF imepotelewa na mijadala ya stara, adabu na weledi badala yake imekuwa jukwaa la watu kutukanana na kukebehiana na hata kusutana!!!!

JF inaaminika kuwa ukurasa wa watu weledi, werevu na waliokomaa kiakili lakini sasa hivi inasikitisha Sana!!!!

Nawasihi wanajukwaa tupunguze munkari kwenye kuchangia na kujadiliana!!

Nawasilisha!!!?
 
Ni sahihi. Nipo kwenye harakati. Nataka mrithi wangu. Siwezi kuwa nafukuza kuku baba mzima wa kuchinja Pasaka hii.

Nikisafiri saa moja wameshajifungia ndani. Wanaogopa.
Sasa hapo si uajiri tuu mtu wa kukuchinjia kuku na mlinzi, ila wabongo bana, kwahiyo wewe ndio sababu zako za msingi hizo, sasa nikwambie hao wasichana unaowazarau ndio mali
 
Na declare interest. Mi ni Baba wa watoto 4 wote wa kike. Mtoto Mkubwa yupo Form 3 na mdogo yupo Class four.

Kwanza nashukuru Mungu kwa kunipa mabinti 4. Kimsingi baada ya wawili wa kwanza kuwa wa kike, nikiongea hao wengine niliamini nitapata kidume nyumbani kwangu.

Hawana changamoto yoyote na wanaendelea na masomo vizuri tu wakiwa na afya na ukuaji mzuri ila kama baba kuna muda napata mawazo kwa kukosa mtoto wa kiume. Naogopa kuongeza kwa huyu mama kwani tunaweza ambulia wa kike tena.

Kimsingi sasa natafuta niweke mbegu huko Pembeni nipate kidume na nimlete kumlea na hawa wenzake. Kuna changamoto nyingi kwa nyumba kukosa mtoto wa kiume.

Changamoto ya Kwanza ndio mrithi wa familia na atakayeendeleza Jina na damu yangu. So kukosa mtoto wa kiume hadi sasa sina mrithi wa mali yangu na atakayeendeleza jina langu.

Pili, kushindwa kufanyika kwa baadhi ya kazi nyumbani kama utunzaji wa mifugo na mbwa ninazofuga, kukosa wa kunichinjia mbuzi au kuku.

Changamoto ya tatu, kukosa wa kuniuguza uzeeni ambaye atanisaidia pia kama mwanaume mwenzake.

Changamoto ya nne kukosa mlinzi na msimamizi wa nyumba kipindi nasafiri kwani huwa nasafiri sana kikazi na kibiashara.

Kimsingi, ni ngumu sana nyumba kukosa mtoro wa kiume. Sasa natafuta mwanamke ambaye atakuwa tayari kuzaa nami na nitamfungulia na kumjengea alee mwanangu na akiwa na miaka 7, nachukua mwanangu.

Ni raha sana kuwa na jamaa anayecheza mpira hapa nyumbani na atakayeniletea kesi za kutia mimba huko nje.

Je wewe mwenye watoto wa kike tu, una changamoto zipi?
Nimekuelewa hapo atakaeendeleza jina lako tu baada yako . Mengine uliyoandika hayana tija na Afya

Mtoto wa kike akiolewa anaenda kuendeleza familia nyingine: wengine hubadili hadi majina ya wqzazi wao na kujiita majina ya wanaume zao , saddest part

Nilimkataza wife wangu asibadili jina lake mimi sio babake ni life mate tu .ni mambo ya hovyo tuliyorithi
 
Back
Top Bottom