Changamoto za kutokuwa na mtoto wa kiume kwenye familia

Naogopa kuongeza kwa huyu mama kwani tunaweza ambulia wa kike tena.

Kimsingi sasa natafuta niweke mbegu huko Pembeni nipate kidume na nimlete kumlea na hawa wenzake. Kuna changamoto nyingi kwa nyumba kukosa mtoto wa kiume.
Kama kuna uwezekano wa watoto wote kuwa wa mama mmoja ni vizuri zaidi.

Kama uwezo wa pesa unakuruhusu tumia njia ya kupandikiza (iVF). Hii ni hakika 100%., hata ukitaka mapacha kama afya ya mama inaruhusu unapata.

Hiyo ya kwenda kutembeza bakora nje huko ni sawa na kucheza kamari tu, unaweza kuendelea kupata mabinti
 
Je wewe mwenye watoto wa kike tu, una changamoto zipi?
Nina watoto wa kike tu, ninaishi na mke, mama mkwe , wadogo wawili wa kike wa mke na housegirl, kwa kifupi nyumba nzima imejaa wanawake na kidume ni mimi tu, sijajua kama kuna changamoto yoyote. Sidhani kama ni lazima awepo, if I were to die today watakaobaki wataendelea.
 
Unaweza kupata mtoto wa kiume akawa tofauti na unavyotegemea, shoga, mwizi, tapeli, jambazi au akaangukia kwa familia ya mke wake.
WAtoto umleavyo ndivyo akuavyo mara nyingi watoto wa kike hawasahau kwao.
Hayo ni matokeo ambayao hakuna mzazi huyategemea kamwe.

Hata watoto wakike wengi wao pia wanabadirika kifupi mwanaume ni muhimu sana kuwa naye kwenye siecle yako
 
Umeeleweka?.
Uko mkoa gani?.
Njoo inbox
 
Huyo mtoto wa nje ya ndoa hana mamlaka ya kurithi pindi utakapokufa wewe, au tafuta mwanamke umuoe, mtengenezee familia yake na urithi wa watoto wake, nakuhakikishia huyo mtoto hataweza kupata chochote pindi utakapokufa ukimuunganisha ktk family kubwa. Mimi babu yangu mzee Dotto alikuwa ni mfugaji wa ng'ombe,ana maeneo makubwa lakini alipofariki hao ng'ombe walianza kuisha pasipo hata kujua wanaishaje maana alifanikiwa kuzaa watoto wa kike pekee watano. Hivyo kwa kweli kupata watoto wa jinsia moja pekee kuna hasara/faida pia.
 
Nenda hospitali, kliniki ya baba na mtoto utapewa ushauri mzuri wa namna ya kupata mtoto wa kiume
.

Usizae nje.
 
Kama una uwezo nenda kapandikize kwa huyo mkeo upate wa kiume hata mapacha. Badala ya kuleta mgogoro kwenye famillia. Kuzaa nje hasa kwa ndoa za kikristo na kama una uchumi wa kuunga unga inakuwa changamoto sana Hasa kwenye mgawanyo wa mali. Kama una uchumi mzuri basi kila mwanamke mfanye amiliki uchumi na watoto wake bila kuingiliana utakuwa na amani sana. Ushauri wangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…