Unaendeleza ukoo ili iweje?
Nani amekupa majukumu ya kuendeleza ukoo?
Ukoo usipoendelea kuna tatizo gani??
1. Ukoo unaendelea ili kuendeleza Bloodline, undugu, ujamaa, mila na desturi za watu. Kila mtu ana kwao, kila mtu ana chanzo. Hakuna mtu anaanguka tuu kutoka mbinguni.
2. Nature ndio inayoendeleza ukoo, umezaliwa na jinsia gani. Kelele iliyopo hapa ni juu ya jinsia ya mtoto, mtoa mada anaona wazi anakwenda kupoteza ukoo wake. Anakwenda kuzaa kwa ukoo wa mtu mwingine na kuundeleza kwa kuzaa kwake. Mwanamke hana jina, na hana ukoo kiasili wala dini. Atakapoolewa ndipo kutakuwa ukoo wake, atapewa jina huko na atakuwa wa huko. Ndio maana leo unasikia mtu anaitwa Asharose Migiro, Salma Kikwete, Magreth Sitta, Hillary Clinton, Michelle Obama, Margaret Kenyatta. Janetg Museveni, Rachel Ruto. Wale wamekuja kwenye koo hizo kwa kuhama, koo zao (surnames) ziliishia pale walipoolewa. 😁
3. Ukoo usipoendelea maana yake kizazi hicho kimepotea.