Changamoto za kutokuwa na mtoto wa kiume kwenye familia

Katika kuendeleza himaya ya biashara zake barani Afrika, bilionea Aliko Dangote kutoka Nigeria, aliwateua mabinti zake watatu, kushika nafasi za juu katika Kampuni ya Dangote Group.

Matajiri kina Dangote wanatoa mali kwa binti zao.

Maskini wenye mali za kubangaiza bangaiza wanaona ngumu sana kumwachia binti mali.

Hata umwachie kidume mali, zitaliwa tu.

Ukishakufa, umekufa. Utasahaulika tu. Ni suala la muda tu.

Watoto wako ndio watakuenzi na kukukumbuka.

Wajukuu, Vitukuu na vilembwe wako wala hawatakuwa na time ya kukukumbuka.

Na jina lako litapotea polepole tu.
 
Ni sahihi. Nipo kwenye harakati. Nataka mrithi wangu. Siwezi kuwa nafukuza kuku baba mzima wa kuchinja Pasaka hii.

Nikisafiri saa moja wameshajifungia ndani. Wanaogopa.
Kwa nini usinunue kuku aliyechinjwa? Kama wewe, mke wako na watoto wako wa kike hamuwezi kuchinja kuku kwa nini msimtafute mtu wa kuwachinjia hapo kijijini kwenu?
Unataka mtoto wa kiume ili aje kukimbizana na kuku na kuchinja, vipi kama hataweza hilo jukumu la kuwa mchinjaji??
 
Watoto pia wanatamani wangekuwa na kaka,nyie hamjui TU family kuzaliwa jinsia moja.
Unafikiri pia wakina Sasha na Malia Obama, Jenna na Barbara Bush, Maria na Katerina Putin, Georgina na Emma Bloomberg au Chelsea Clinton nao wanatamani wangekuwa na kaka zao au ni mabinti wa makupuku tu ndio wana hayo mawazo??
 
Siku hizi watoto wa kike ndo wanaendeleza mali za familia.....Game imebadilika mzee...
Anazo hizo mali kwanza kwa kuanzia?!, Ni nadra mtu mwenye mali kuanza kulalamika kukosa mtu wa kuchinja kuku au familia kujifungia ndani mapema jioni asipokuwepo, hii inamaanisha hata nyumba kama anayo basi haina ukuta na hawezi kuajiri hata mlinzi.
 
Sidhani kama atakuelewa..muache tu akatangetange aendelee kuongeza idadi ya watoto wa kike
 
Huo ni mfumo wa maisha wa Waafrika masikini hasa wa bara, kwa familia za matajiri na jamii za Pwani mambo ni tofauti kabisa.
 
Kwanza watoto wa kiume wengi wao wanapenda kuhonga hovyo hovyo, unashangaa kaachiwa kampuni ilikuwa na mtaji (shares)wa 900m, ghafla mtaji (shares)unashuka
 
Wewe ni MPUMBAVU,na hizo zote zinazokusumbua ni Illusions,unaweza kua na watoto 10 wote wa kiume na wasifanye hata kimoja ulichotaja hapa,maisha ni Qadar,......furaha ipo kwenye akili yako
 
Unaweza mtoa nyani mbugani, lakini huwezi itoa mbuga kichwani kwa nyani. Ipo siku nyani atarudi mbugani.
Ni mjinga tuu ndio anaweza jenga ujombani. 😁
Kwa nini mnasubiria kujengewa na watoto badala ya kujenga nyie wenyewe? Kwa nini Waafrika bado mnaendelea kuwafanya watoto vitega uchumi, uwekezaji na pensheni za uzeeni??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…