#COVID19 Chanjo ni Lazima: Hoja ya Mbowe ina Mashiko

Wanaotengeneza chanjo wenyewe hawajalazimisha chanjo kwa watu wao, mpaka hapo hujaona tatizo kwenye kulazimisha?

Unaelewa kwamba maadili ya kitabibu hayaruhusu kulazimisha chanjo?

Waisoma wapi shuruti mkuu?

Weka muziki wacha maneno.
 
Nimegundua mtoa mada ni kichwa dafu hopeless kabisa
Wewe chukua familia yako kaichanje man1na
 
Wanaochomwa wachomwe ila iwe hiari sio lazma
 
Ahahaha Mbowe yeye anatafuta gia ya kumgonganisha rais na wananchi.maana akilazima watu wachanjwe watu hawatamlaumu Mbowe Bali rais,akikubali tu kitakachotokea huko mbele sijui.

Fikiri tu agizo la kuvaa barakoa wananchi wamelipa kisogo kana kwamba hajatamka kiongozi wa juu,la chanjo ndo itakuwa Moto.
 
Wanaochomwa wachomwe ila iwe hiari sio lazma

Na ndivyo ilivyo mkuu. Na zingine.za hiari ziko hapa:


Mengine yote ni mazungumzo baada ya habari.

Kivyetu vyetu tuko hapa:

 

Hii ngoma nzito. Agizo la barakoa limepigwa kisogo? Hata huku pia?


Mdogo mdogo tulianzia Corona haipo. Hata hivyo:

 
Nimegundua mtoa mada ni kichwa dafu hopeless kabisa
Wewe chukua familia yako kaichanje man1na

Bila shaka ugunduzi wako ni kama wa babu Loliondo aliyegundua kinga na tiba ya Corona ya jero kwa kuota ndoto tu.

Hii ndiyo Tanzania ya viwanda na madini tuliyorithi tokea awamu ile.

Eti kuwa wagunduzi wenyewe na wewe umo 😂😂😂😂😂!

Hiiiiii bagosha.
 
Sawa....ila huenda nahitaj kudukua vzur zaid......maana kama ni hvyo...yaan antibodies znazotokana na kutengenezwa naturaly na mwil baada ya wadudu kuingia huwa znakua za mda mfupi huo wa 5month na zile znazotengenezwa baada ya antigen zilizoingizwa kwa sindano ndio znaish mda mref etc etc...inaweza ikawa kwel...au pia si kwel..

Na unaongeleaje kuhusu variants wa hyo covid19...inamana itatuhitaj kirus kikibadilika tu tuchomwe tena antigen wake..sasa tutachoma mara ngap?maana mpaka sasa huyo kirus keshabadilika sanaa...kwann hzo chanjo wasichomwe watu dhaifu..yaan wazee...wenye magonjwa ya mda mref etc etc...sis wazima wenye afya tuachwe na miil yetu itengeneze kinga yenyew....kwan kuna ubaya gan.watu tushaumwa na kupona na tuko fit mpaka leo..tatzo ni nin wao kutaka fanya ulazima kwa watu.
 
Waisoma wapi shuruti mkuu?

Weka muziki wacha maneno.
Msikilize Chairman Mao kuanzia dakika ya 6 hapo. Kwanza anadanganya kusema kwenye nchi za wenzetu chanjo ni lazima, nchi gani hizo?

 
Nisiache kukupa pole wakati nikikukumbusha haya niliyoyasema mwanzo kabisa ili tuweze kufahamiana:

"Kama mwuungwana tokea pande za Pwani niliyeukataa ukanjanja katika nyanja zote .."

Pia nisiache kukumbusha hili nililokudokeza baadaye:

"-- si haba kukubali kuwa beberu yuko mbali na si mwenzetu."

Si nia yangu kukushawishi kwa lolote wala kuingia katika marumbano na yeyote kwa ajili ya mabishano yasiyo na tija ( yaani - just for the sake of argument).

Sina shaka kuwa hadi sasa utakuwa umeipata ladha ya kuwa mkazi wa Pwani na kuukataa ukanjanja.

Kwani hata tuna cha kuficha? Hali zetu ndiyo hizi zenye kujilisha upepo - utaalamu wa nyungu, mikaratusi, michai chai, malimao na matango pori mengine.

Sana sana kikichanganya zaidi tunatoka kivyetu vyetu kama babu wa Loliondo na kikombe chake cha kutibu na kuzuia Corona cha jero, alichoota usiku.

Tuacheni kuwasikiliza wataalamu "at our own peril!"


Ninakubaliana na mzee Warioba (Mola amjalie maisha marefu) janga hili ndilo lililo kipaumbele kweli kweli kwetu kwa sasa.
 
Nimegundua mtoa mada ni kichwa dafu hopeless kabisa
Wewe chukua familia yako kaichanje man1na
Hivi mkuu brazaj ndipo umemgundua leo. Mbona sie tulimjua tangu anahangaika na barabara za Rusumo, ni mpuuzi hakuna mfano huyu mrundi
 
corona ni hatari sana imetugawanyisha

Hii ni kwa sababu ya kuingiza siasa uchwara kwenye ugonjwa huu hatari ambao unaoua.

Wangapi wamekufa kwenye ujinga huu wa nyungu,malimao, mikaratusi, michai chai na matango pori mengine? Wengi wa hao hawakupaswa kufa hivi.

Sasa hivi tuko njiani kuelekea Loliondo kwa babu na kikombe chake cha jero.

Hata hivyo kwa vile tuko huku:



Kwa maoni yangu tunaelekea kuzuri kwani tangia Mama kushika hatamu busara inazidi kutamalaki.
 
Msikilize Chairman Mao kuanzia dakika ya 6 hapo. Kwanza anadanganya kusema kwenye nchi za wenzetu chanjo ni lazima, nchi gani hizo?


Nimeisikiliza hotuba yote ya Mh. Mbowe. Mwili umenisisimka. Sikuwa nimeisikia kabla.

Katika hotuba hii, sioni popote ambapo ina tatizo lolote na mtanzania yeyote.

Kwamba kuna wagonjwa wa Corona na watu wanakufa nchini kote? Kwamba wahanga hawa wanalazimika kujigharimia wenyewe kwa ajili ya matibabu dhidi ya ugonjwa huu na kwenye bei kama anazozielezea mheshimiwa huyu mwenyewe akiwa shahidi?

Kwamba msimamo wa serikali ya awamu ile ulikuwa ule tulioujua, na hali ya msimamo wa serikali hii ni huu tunaouona sasa?

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.

Mkuu, kwamba ulipo wewe labda hata umekwisha pokea chanjo, na sasa ndiyo kuwa tatizo lako hapa ni kwa Mh. Mbowe kuwa tu, eti?:

"Kwanza anadanganya kusema kwenye nchi za wenzetu chanjo ni lazima, nchi gani hizo?"

Seriously?!

Au hii ni kuamua tu kutucheza shere sisi tulio wahanga wa moja kwa moja wa hili janga?


Acheni basi kutucheza shere....!

Ni vizuri ukafahamu kama ulikuwa hujui, sisi tunaokabiliwa na hatari ya wazi ya kifo kutokana na ugonjwa huu tunakubaliana na hotuba ya Mh. Mbowe kwa 100%.

Kiufupi ni kuwa, tunajua pia asiyekubaliana na hotuba hii atakuwa labda kesha pokea chanjo, hayupo hapa nchini, au ni ile kuwa na uelewa mdogo tu.

Uelewa mdogo hapa nao ni bila shaka kutokana na upotoshwaji mkubwa tuliyorithi kutokea awamu ile kama anavyosema Mh. Mbowe.

Haiyumkiniki mwenye matatizo na hotuba ya Mbowe ambaye yuko hapa nchini kuwa, bila shaka atakuwa pia ni muumini mwaminifu wa yale mambo yetu ya kishirikina zikiwamo nyungu, mikaratusi, michai chai, malimao, na yale matango tango pori mengine.

Haiyumkiniki pia muumini kama huyo atakuwa alipo sasa atakuwa yuko safarini kuelekea Loliondo kwa ajili ya kwenda kupata tiba na kinga timilifu sasa tokea kwa babu akiwa na jero lake kibindoni.

Bila kujali wewe binafsi ulipo, nisiache kukuitisha japo kuwa angalau chembe chembe za utu au ubinadamu kidogo. Ukayatambue madhila na magumu ya wazi wanayoyapitia waja wa mola sisi ambao wahanga watarajiwa wa ugonjwa huu chini ya tawala hizi zisizokuwa na chembe hata kidogo ya huruma wala kujali maisha ya wananchi wake.

Ninapendekeza kuipandisha clip ya hotuba hii ya Mh. Mbowe kama uzi kamili ili wengi waweze kuiona.

Ninaelewa sasa kuwa kumbe makelele haya ni ya nini? Kumbe itakuwa ni jitihada zile zile za kuyafunika mengi ya msingi yaliyomo kwenye hotuba ya Mh. Mbowe.

Si mbaya mkajua kwa mara nyingine kimedunda!

Wakuu Erythrocyte BAM Salary Slip technically Missile of the Nation @extroverts ni vizuri upande uzi wenye hotuba mheshimiwa Mbowe kama uzi kamili.

Hapa kuna mkakati ulioshindwa wa kuifunika hotuba hii kuielekeza kwenye yasiyo na chembe ya maslahi kwa nchi hii.
 
Nimekuuliza nchi iliyolazimisha chanjo ni ipi?

Hujajibu.

Wamarekani waliotengeneza chanjo hawalazimishi chanjo.

Unafikiri wao ni wajinga?
 
Nimekuuliza nchi iliyolazimisha chanjo ni ipi?

Hujajibu.

Wamarekani waliotengeneza chanjo hawalazimishi chanjo.

Unafikiri wao ni wajinga?

Mimi ni mhanga mtarajiwa wa wazi wa upuuzi unaoendelea hapa. Naweza kugeuka mfu dakika yoyote kwa sababu ya watu hawa. Unaniuliza ya wamarekani? Give me a break!

Wewe ulipo si umeshanjwa?

Ulipo wewe Corona haikuhusu. Ama kweli hawakukosea waswahili waliosema mzigo wa mwenzio kwako ni kanda la sufu(Sufi). Tuko kati ya janga wewe unadhani we are enjoying ourselves?! Tunapambana wenyewe kwani hata kuna hata tulichowaomba?

Iko wapi shida kwenye speech ya Mbowe kwa nchi hii?

Acheni unafiki huku nyie mkiwa salama.

Hatuko wajinga kiasi hicho.
 
Kwani wewe utakuwa wa kwanza kufariki?? Hizi chanjo ni hatari hivyo ni kheri watakaosalimika bila kuchanjwa waendeleze vizazi wakiwa na immune system imara na sio kudungwa hii michanjo
 
Kwani wewe utakuwa wa kwanza kufariki?? Hizi chanjo ni hatari hivyo ni kheri watakaosalimika bila kuchanjwa waendeleze vizazi wakiwa na immune system imara na sio kudungwa hii michanjo

Waungwana wanadadavuwa kuwa sababu za vifo ni 4:



Kwa mujibu wa:


Sina taabu na kufa au ndugu na jamaa yangu yeyote kufa kwa sababu yoyote isipokuwa #2 na #4.

#2 na #4 tutawajibishana tu hata kama nitakuwa binafsi zipo duniani:


Kama kwenu maisha hayana thamani si kwa wote.

Chanjo ni hiari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…