Kama mwuungwana tokea pande za Pwani niliyeukataa ukanjanja katika nyanja zote, nina lazimika kutia neno juu ya maneno ya hekima yake Mwamba Aboubakar Laigwanan Mbowe (Mola amjalie maisha marefu).
Uhalisia kuhusiana na chanjo yoyote ni huu hapa:
"Chanjo ina maana kama tu idadi kubwa na ya kutosha katika jamii inakuwa imeipokea. Vinginevyo inakuwa haina maana."
Kiuhalisia chanjo ni kwa manufaa ya wanayoipokea. Serikali zina wajibu wa kuona watu wake wananufaika chanjo husika.
Kuweza kuwapata idadi kubwa kadri iwezekanavyo mbinu mbali mbali hutumika zikiwamo kutoa elimu, ushawishi na hata kutumia nguvu ikibidi.
Kwa wanaume wa shoka, pande za Rwanda na Uganda, huko hakuna cha lele mama au mswalia mtume. Huko kuchanjwa ni lazima na bakora kumhusu mtu anayeleta ujuaji wala si issue.
Kwingine uthibitisho wa chanjo huhitajika kabla ya kupata huduma kama vile usajili, usafiri, ruhusa nk kama kishawishi. Chanjo inakuwa hiari, lakini ni lazima kabla ya huduma husika.
Kwa jamii zilizostaarabika vilivyo na zenye kujitambua, huko chanjo ni vitu vinavyoeleweka.
Rejelea hali halisi ya kwetu ambapo tokea Apr 2020 hazipo takwimu mpya za Corona. Yaani tokea hapo hakuna mgonjwa wala aliyekufa kwa Corona isipokuwa kaka yake Mbowe.
Katika kipindi hicho pia watu wameaminishwa kuwa huu ugonjwa haupo. Bali Corona ni vita vya kiuchumi na chanjo hizi ni sehemu tu katika kuwaangamiza wao.
Hiiiiii bagosha!
Waliowaaminisha hivyo ni Rais wa nchi akishirikiana na wizara yenye dhamana na afya za watu. Katika walioaminishwa hivyo, wengi wao ni "the ignorant mass" vijijini; wakiwamo sungu sungu, wapiga debe, machinga, vibaka vibaka na wa namna hiyo.
Una ibadili vipi mitizamo ya watu kama hao, huku watu wakiendelea kufa?
Ikumbukwe kuwa hadi sasa serikali yetu haitoi takwimu zozote na hayupo ajuaye hali ni njema au mbaya kiasi gani.
Kwa hakika mwenye kujua faida za chanjo na kuthamimi maisha ya watu hatachelea kutumia nguvu kuwataka watu kuchanjwa ambayo aghalabu ni kwa faida yao.
Ama kwa hakika itakuwa jambo la kushangaza kwa serikali yoyote, kama itakaa kimya iache watu kufa iwapo matumizi ya nguvu tu yangali nusuru maisha dhidi ya ujinga wao.
Viva Museveni na viva Kagame kwa kuyajali maisha ya watu wenu vilivyo kiasi cha kutumia nguvu stahiki inapobidi katika kuwanusuru.
Kwa hakika waja nyie mnayo thwawabu kubwa huko mbinguni, Inshallah!
wa mpuuzi unajifungia na kuandika bila kufanya utafiti. Waliochanjwa wanaendelea kupata
Unaambiwa British health minister Sajid Javid has said he tested positive for COVID-19, but that his symptoms were mild and he had had two doses of vaccine against the disease.
Ahahaha Mbowe yeye anatafuta gia ya kumgonganisha rais na wananchi.maana akilazima watu wachanjwe watu hawatamlaumu Mbowe Bali rais,akikubali tu kitakachotokea huko mbele sijui.
Fikiri tu agizo la kuvaa barakoa wananchi wamelipa kisogo kana kwamba hajatamka kiongozi wa juu,la chanjo ndo itakuwa Moto.
Mkuu wa wilaya ya Moshi Mkoani Kilimanjaro Said Mtanda Julai 19.2021 amezitaka mamlaka za usafirishaji kuzuia magari kuondoka stendi ikiwa abiria wake hawaja vaa barakoa kujikinga na virusi vya Corona. Nimekuja kuwaambia ukweli na Rais na Serikali yake wamesha sema Corona ipo tena wimbi la tatu...

Mkuu sikuwa nimeiona comment yako hii kabla. Bila shaka kutokana na kuwa imekuwa ni siku ndefu yenye uhitaji mkubwa na kuweka kumbukumbu nyingi sawa sawa.
Kujibu maswali yako:
1. Kwa nini mtu anahitaji kuchomwa chanjo?:
-- kwa kawaida mwili una namna kujikinga (antibodies) na viingiavyo mwilini vyenye kuweza kuleta magonjwa (antigens).
-- kila antigen inahitaji antibody yake.
-- mwili unaposhambuliwa na antigen fulani, huugua wakati ukipambana kutengeneza antibody husika.
-- mwili ukisha tengeneza antibody husika sasa unakuwa unaijua antigen hiyo na kuwa uko tayari kwa mpambano.
-- si antibodies zote zinabakia mwilini siku zote.
-- antibodies za Corona kwa mfano hubakia mwilini kwa takribani miezi 5.
-- antibodies za ebola hubakia kwa muda mrefu zaidi ambapo hata ni sahihi kusema mtu akiugua ebola hawezi kuugua tena.
2. Kwa nini mtu anachomwa chanjo?:
-- mtu anachomwa chanjo ili kuufanya mwili kutengeneza antibodies kabla ya hatari.
-- hii huwa si tu kuwa ni wadudu waliodhoofu.
-- wanaweza kuwa ni wadudu dhoofu yaani walioodhofishwa, au waliokufa, au hata vipande (au kipande chao) yaani inactivated, attenuated, particles au wakiwa wafu.
-- si haba kukubali kuwa beberu yuko mbali na si mwenzetu.
-- hivi vikiingizwa mwilini, mwili huhamasishwa kutambua ujio wa antigen mwenye ufanano nao ili kutengeneza antibody stahiki kumsubiria.
-- antigen huyo akija mwili huwa katika nafasi nzuri zaidi ya kupambana naye ukiwa katika afya njema.
3. Kama ulishaugua Corona kwanini kuchanjwa tena?
-- kama ilivyo elezwa kabla antibody kwa Corona kutokana na ugonjwa zinakaa kwa takribani miezi 5.
-- ikumbukwe hizi zinakuja kukiwemo na kusukwa sukwa na ugonjwa wenyewe, kama vita kamili.
-- haiyumkiniki kuuacha mwili ukiwa pia na irreparable damages.
-- ipo tofauti ya maisha antibodies za kutokana na chanjo na za kutokana na maisha mwilini.
-- tofauti hii ikutokana na sababu mbalimbali zikiwamo technologies, dozi na labda pia ile kuwa mwili unapokea kichocheo ukiwa uko mzima.
-- kumbuka chanjo nyingi zina dozi 2 - 3.
-- antibody ya chanjo ina nafasi ya kuwapo kwa muda zaidi ikiwamo hata vikorombwezo zaidi.
Kulikuwa na uzi huu humu jamvini labda pia ungeupitia kwa kumbukumbu zaidi:
Mabibi na mabwana kumekuwa na habari nyingi kuhusiana na tiba na au chanjo za ugonjwa huu. Kujiridhisha nimelazimika kujivinjari kiselule selule pale katika shule ya tiba, Muhimbili. Yafuatayo ni niliyokusanya na kwa kweri tunaongopeana sana: 1. Antigen - hiki ni kitu kigeni katika mwili...
Sawa....ila huenda nahitaj kudukua vzur zaid......maana kama ni hvyo...yaan antibodies znazotokana na kutengenezwa naturaly na mwil baada ya wadudu kuingia huwa znakua za mda mfupi huo wa 5month na zile znazotengenezwa baada ya antigen zilizoingizwa kwa sindano ndio znaish mda mref etc etc...inaweza ikawa kwel...au pia si kwel..
Na unaongeleaje kuhusu variants wa hyo covid19...inamana itatuhitaj kirus kikibadilika tu tuchomwe tena antigen wake..sasa tutachoma mara ngap?maana mpaka sasa huyo kirus keshabadilika sanaa...kwann hzo chanjo wasichomwe watu dhaifu..yaan wazee...wenye magonjwa ya mda mref etc etc...sis wazima wenye afya tuachwe na miil yetu itengeneze kinga yenyew....kwan kuna ubaya gan.watu tushaumwa na kupona na tuko fit mpaka leo..tatzo ni nin wao kutaka fanya ulazima kwa watu.

Nisiache kukupa pole wakati nikikukumbusha haya niliyoyasema mwanzo kabisa ili tuweze kufahamiana:
"Kama mwuungwana tokea pande za Pwani niliyeukataa ukanjanja katika nyanja zote .."
Pia nisiache kukumbusha hili nililokudokeza baadaye:
"-- si haba kukubali kuwa beberu yuko mbali na si mwenzetu."
Si nia yangu kukushawishi kwa lolote wala kuingia katika marumbano na yeyote kwa ajili ya mabishano yasiyo na tija ( yaani - just for the sake of argument).
Sina shaka kuwa hadi sasa utakuwa umeipata ladha ya kuwa mkazi wa Pwani na kuukataa ukanjanja.
Kwani hata tuna cha kuficha? Hali zetu ndiyo hizi zenye kujilisha upepo - utaalamu wa nyungu, mikaratusi, michai chai, malimao na matango pori mengine.
Sana sana kikichanganya zaidi tunatoka kivyetu vyetu kama babu wa Loliondo na kikombe chake cha kutibu na kuzuia Corona cha jero, alichoota usiku.
Tuacheni kuwasikiliza wataalamu "at our own peril!"
Utu uzima dawa, na ya kale ni dhahabu. Mzee Warioba ni mtu wa kuonwa kwa ushauri (consultation) na wote wenye nia njema na nchi hii na hasa wale walio wazalendo. Hii ni kwa wote tokea serikalini na hata wanaopambania kupatikana katiba mpya. Mzee Warioba yuko wazi kuhusu umuhimu na udharura...
www.jamiiforums.com
Ninakubaliana na mzee Warioba (Mola amjalie maisha marefu) janga hili ndilo lililo kipaumbele kweli kweli kwetu kwa sasa.
Nimeisikiliza hotuba yote ya Mh. Mbowe. Mwili umenisisimka. Sikuwa nimeisikia kabla.
Katika hotuba hii, sioni popote ambapo ina tatizo lolote na mtanzania yeyote.
Kwamba kuna wagonjwa wa Corona na watu wanakufa nchini kote? Kwamba wahanga hawa wanalazimika kujigharimia wenyewe kwa ajili ya matibabu dhidi ya ugonjwa huu na kwenye bei kama anazozielezea mheshimiwa huyu mwenyewe akiwa shahidi?
Kwamba msimamo wa serikali ya awamu ile ulikuwa ule tulioujua, na hali ya msimamo wa serikali hii ni huu tunaouona sasa?
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.
Mkuu, kwamba ulipo wewe labda hata umekwisha pokea chanjo, na sasa ndiyo kuwa tatizo lako hapa ni kwa Mh. Mbowe kuwa tu, eti?:
"Kwanza anadanganya kusema kwenye nchi za wenzetu chanjo ni lazima, nchi gani hizo?"
Seriously?!
Au hii ni kuamua tu kutucheza shere sisi tulio wahanga wa moja kwa moja wa hili janga?
Huu ni waraka wa wazi kutoka kwetu tulio wahanga watarajiwa wa covid-19 kuja kwenu nyie tuliowapa mamlaka na sasa mnatutoa kafara wakati nyie mko pema. Ninaandika waraka huu kwa kudra za mola nikiwa ningali hai na nikiwa na imani ya dhati kuwa marehemu wengi mliowatoa kafara wangeandika waraka...
www.jamiiforums.com
Acheni basi kutucheza shere....!
Ni vizuri ukafahamu kama ulikuwa hujui, sisi tunaokabiliwa na hatari ya wazi ya kifo kutokana na ugonjwa huu tunakubaliana na hotuba ya Mh. Mbowe kwa 100%.
Kiufupi ni kuwa, tunajua pia asiyekubaliana na hotuba hii atakuwa labda kesha pokea chanjo, hayupo hapa nchini, au ni ile kuwa na uelewa mdogo tu.
Uelewa mdogo hapa nao ni bila shaka kutokana na upotoshwaji mkubwa tuliyorithi kutokea awamu ile kama anavyosema Mh. Mbowe.
Haiyumkiniki mwenye matatizo na hotuba ya Mbowe ambaye yuko hapa nchini kuwa, bila shaka atakuwa pia ni muumini mwaminifu wa yale mambo yetu ya kishirikina zikiwamo nyungu, mikaratusi, michai chai, malimao, na yale matango tango pori mengine.
Haiyumkiniki pia muumini kama huyo atakuwa alipo sasa atakuwa yuko safarini kuelekea Loliondo kwa ajili ya kwenda kupata tiba na kinga timilifu sasa tokea kwa babu akiwa na jero lake kibindoni.
Bila kujali wewe binafsi ulipo, nisiache kukuitisha japo kuwa angalau chembe chembe za utu au ubinadamu kidogo. Ukayatambue madhila na magumu ya wazi wanayoyapitia waja wa mola sisi ambao wahanga watarajiwa wa ugonjwa huu chini ya tawala hizi zisizokuwa na chembe hata kidogo ya huruma wala kujali maisha ya wananchi wake.
Ninapendekeza kuipandisha clip ya hotuba hii ya Mh. Mbowe kama uzi kamili ili wengi waweze kuiona.
Ninaelewa sasa kuwa kumbe makelele haya ni ya nini? Kumbe itakuwa ni jitihada zile zile za kuyafunika mengi ya msingi yaliyomo kwenye hotuba ya Mh. Mbowe.
Nimeisikiliza hotuba yote ya Mh. Mbowe. Mwili umenisisimka sikuwa nimeisikia kabla.
Katika hotuba hii, sioni popote ambapo ina tatizo lolote na mtanzania yeyote.
Kwamba kuna wagonjwa wa Corona na wengine wanakufa nchini kote? Kwamba wahanga hawa wanalazimika kujigharimia wenyewe kwa ajili ya matibabu yao dhidi ya ugonjwa huu na kwenye bei anazozielezea mheshimiwa huyu mwenyewe akiwa shahidi?
Kwamba msimamo wa serikali ya awamu ile ulikuwa ule tulioujua, na hali ya msimamo wa serikali hii ni huu tunaouona sasa?
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.
Mkuu, kwamba ulipo wewe labda hata umekwisha pokea chanjo, na sasa ndiyo kuwa tatizo lako hapa ni kuwa tu, eti kwamba:
"Kwanza anadanganya kusema kwenye nchi za wenzetu chanjo ni lazima, nchi gani hizo?"
Seriously?!
Au ni kuamua kutucheza shere tu sisi tulio wahanga wa moja kwa moja wa hili janga?
Acheni basi kutucheza shere....!
Ni vizuri ukafahamu kama ulikuwa hujui, sisi tunaokabiliwa na hatari ya wazi ya kifo kutokana na ugonjwa huu tunakubaliana na hotuba ya Mbowe kwa 100%.
Kiufupi ni kuwa, asiyekubaliana na hotuba hii atakuwa labda kama kesha pokea chanjo, hayupo hapa nchini, au ni ile kuwa na uelewa mdogo.
Uelewa mdogo hapa nao ni bila shaka kutokana na upotoshwaji mkubwa kutoka awamu ile kama anavyosema Mh. Mbowe.
Haiyumkiniki mwenye matatizo na hotuba ya Mbowe aliyeko hapa nchini nchini, bila shaka atakuwa pia ni muumini mwaminifu wa yale mambo ya nyungu, mikaratusi, michai chai, malimao, na yale matango pori mengine.
Haiyumkiniki pia muumini huyo atakuwa alipo yuko safarini kuelekea Loliondo kwa babu kwa ajili ya tiba na kinga timilifu tokea kwa babu akiwa na jero lake kibindoni.
Bila kujali wewe binafsi ulipo, nisiache kukuitisha japo kuwa angalau na utu au ubinadamu kidogo, ukayatambue madhila na magumu ya wazi wanayoyapitia wahanga wa ugonjwa huu chini ya tawala hizi zisizokuwa na chembe ya huruma wala kuwajali wananchi wake.
Ninapendekeza kuipandisha clip ya hotuba hii kama uzi kamili ili wengi waweze kuiona.
Ninaelewa sasa kuwa kumbe makelele haya ni ya nini? Kumbe itakuwa ni jitihada zile zile za kuyafunika mengi ya msingi yaliyomo kwenye hotuba ya Mh. Mbowe.
Mimi ni mhanga mtarajiwa wa wazi wa upuuzi unaoendelea hapa. Naweza kugeuka mfu dakika yoyote kwa sababu ya watu hawa. Unaniuliza ya wamarekani? Give me a break!
Wewe ulipo si umeshanjwa?
Ulipo wewe Corona haikuhusu. Ama kweli hawakukosea waswahili waliosema mzigo wa mwenzio kwako ni kanda la sufu(Sufi). Tuko kati ya janga wewe unadhani we are enjoying ourselves?! Tunapambana wenyewe kwani hata kuna hata tulichowaomba?
Iko wapi shida kwenye speech ya Mbowe kwa nchi hii?

Kwani wewe utakuwa wa kwanza kufariki?? Hizi chanjo ni hatari hivyo ni kheri watakaosalimika bila kuchanjwa waendeleze vizazi wakiwa na immune system imara na sio kudungwa hii michanjo
Kwani wewe utakuwa wa kwanza kufariki?? Hizi chanjo ni hatari hivyo ni kheri watakaosalimika bila kuchanjwa waendeleze vizazi wakiwa na immune system imara na sio kudungwa hii michanjo
Mabibi na mabwana zimekuwapo nadharia nyingi na zingine nyepesi nyepesi kuhusiana na vifo na wendazao. Mtumishi huyu wa Mungu katika udadavuzi wake kwa hakika ana hoja za msingi: Kwamba pana vifo vya aina 4: 1. Uzee (wa miaka ma Mia wako hapa) 2. Vya kusababishwa na kusababishiwa (wa kwenye...
www.jamiiforums.com
Sina taabu na kufa au ndugu na jamaa yangu yeyote kufa kwa sababu yoyote isipokuwa #2 na #4.
#2 na #4 tutawajibishana tu hata kama nitakuwa binafsi zipo duniani:
Katika ule mukthadha wa kukubali kutokubaliana, ikumbukwe kuwa iliombwa watu kuweka orodha ya wahanga wote wa hizi changamoto za kupumua, kila inapowezekana. Kuondoa tashwishi hapa ninaweka tarehe tulizopoteza wanasheria nguli hadi kufikia 09.07.2020 idadi yao mbele katika mabano (kama...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.