#COVID19 Chanjo za Kupambana na Corona (COVID-19): Nini Maoni na Mtazamo wako?
Hakuwaamini mabeberu lakini ka pacemaker kao kalikokuwa kanamsukumia damu alikaamini?

Tena ashukuru hao wazungu maana bila wao angeshapotea siku nyingi hata tusingemfahamu

Unasemaje tukiachana na uhuru wetu tuirudishe nchi iwe koloni la wazungu?

Maana naona akili yako imeganda kabisa.
 
Anasema wanalazimisha chanjo wakati serikali haijalazimisha mtu.
Anatisha watakaomjibu na kuwaita wajinga na kwamba atawasemesha mpaka watafute taulo ya kuvaa.
Anasema chanjo haijathibitishwa kama ni salama ( hizi habari kazitoa wapi)- uongo mtupu.
Anadai watakaozaliwa baadae watageuka - uongo mtupu.
watanzania 60m kuwa majaribio, hapa anakolezea chumvi.

Gwajima anadai walichochanjwa uingereza na USA. ni tofauti na tunachochanja sisi (ametunga na hana ushahidi wowote) - uongo mtupu

Anasema wazungu wangependa tufe wote huku kashika mic aliyotengeneza mzungu - amelaza ubongo.
Anabeza hatua za kuweka record wakati magonjwa mengi tu record zinwekwa
Hela wanazotoa wazungu ni mkopo siyo bure kama anavyodai yeye- amedanganya

Cha kusikitisha hajui kwanini mtu aliyechanjwa aendelee kuchukua tahadhari.
Anadanganya waumini kuwa chanjo ina kazi nyingine. (Haya maneno kamnukuu jamaa mmoja mitandaoni) chanzo ambacho si reliable source.anadanganya tena.

Tunajua lengo lake,, ni legacy ya jiwe.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app

Legacy ya Magufuli ipo tu, wala haimtegemei Gwajima.

Badala ya kuhangaika na kila neno alilosema, jiulize swali jepesi tu. Je huko ilikotoka chanjo wamemaliza tatizo?

Je sisi hapa tuna tatizo mpaka kuhitaji chanjo?

Maana watu wanapromoti korona, lakini je kwa kipimo gani?

Kitendawili cha kipimo bado hakijatenguliwa hadi leo.
 
🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾👍🏽
Chanjo na dawa zote zinazotumuka Tanzania, majaribio yake yamefanyika Tanzania?!

Unaweza kunionesha ripoti ya chanjo za surua, ndui, polio na magonjwa mengine kama hayo ikiwa ni matokeo ya majaribio ya chanjo hizo kufanyika Tanzania?
 
Mkishaanza kuchanganya siasa na sayansi mnaharibu. Kama hizi chanjo siyo nzuri kwetu, toeni sababu za kisayansi na siyo za kisiasa za kwa nini watu wasichanjwe. Kama ni side effects za chanjo, kila dawa ina side effects. Kama chanjo hazifanyi kazi, leteni takwimu zake tuzisome.
Swali la kwanza ni kipimo.

Unaongelea korona kwa kipimo gani?

Kimetestiwa kwa blind test kama ile ya mapapai na mbuzi na oil chafu?
 
KWANINI CHANJO YA KORONA IMELETWA

Kama kuchanja ni hiyari, na Mh. Rais ameamua kupigia debe chanjo, basi ni haki pia kwa wale ambao hawaungi mkono chanjo nao kupigia debe upande wao.

Sioni sababu ya wanaopinga chanjo kama Mh. Gwajima kutolewa kauli za vitisho na baadhi ya wana-CCM. Ndo maana ya hiyari hiyo. Hiyari ina pande mbili.

Sababu kuu haswa ya kuletwa chanjo nchini Tanzania ni kwa sababu Magufuli hayupo. Angekuwepo zisingekanyaga hapa. Kifo cha Magufuli kitatugharimu sana waTanzania.

Sababu ya pili ni ikumbukwe kwamba maudhui ya kuleta chanjo ilikuwa ni kuwasaidia mahujaji na waTanzania wengine wanaotaka kusafiri kwenda kwenye nchi ambazo zinahitaji chanjo. Lakini hata waSaudi wenyewe ni kwamba hawana imani na chanjo; na ndo maana wameamua kupiga marufuku mahujaji wa kutoka nje ya nchi yao.

Kwa mfano tuna chanjo ya homa ya manjano hapa Tanzania, lakini hakuna mtu anayehangaika nayo isipokuwa tu kama unataka kusafiri kwenda kwenye nchi ambayo wanataka uwe umechanjwa ndo wakupokee. Na hata hiyo chanjo yenyewe ya homa ya manjano kuchanja ni hiyari. Unaweza ukailipia tu na kupewa kadi kuwa umechanja ili usisumbuliwe huko uendako.

Sababu ya tatu ni ubeberu. Mh. Rais tuliona aliwapigia simu mabeberu wa EU siku ile akawaweka na loudspeaker. Kwa kuwa amejipendekeza mwenyewe kwenye anga zao ni lazima wampelekeshe wanavyotaka wao. Mabeberu siku zote hawapendi kuona fikra huru ya Mwafrika. Hawakufuruhishwa kabisaaaa na msimamo tofauti na ambao ulikuwa unaonesha matokeo chanya wa Magufuli. Matokeo chanya kwa maana ya kwamba waTanzania tumeishi kwa uhuru bila matatizo yoyote wakati wao mabeberu wakifungia ndani kama kuku.

Kwa wale wenye uzoefu naamini mtakubaliana nami kwamba Mzungu hata siku moja hayuko tayari kupokea wazo jipya na tofauti na anachojua yeye kutoka kwa ngozi nyeusi. Duniani huko watu wanatudharau ngozi nyeusi kwa kiasi kikubwa. Hilo sio tatizo. Tatizo ni pale sisi wa ngozi nyeusi tunapoanza kujidharau wenyewe. Hilo ni tatizo kubwa sana ambalo linawatafuna waAfrika wengi sana.

Leo hii mTanzania ukimwambia aachane na Ukristo au Uislam kwa kuwa sio falsafa za kiAfrika mtazozana sana.

Sasa kwa kujidharau huku leo hii tunaona serikali ikiwa imekamatwa akili na mabeberu, inaanza kufuata miongozo yao na kuagiza chanjo. Kwa hiyo sababu ya tatu ni hiyo ya ubeberu. Mabeberu walikuwa wanapambana kuhakikisha kuwa mwafrika anaendelea kuwa kwenye usingizi na kuwa kwenye himaya yao kifikra. Mwafrika kama Magufuli aliyezinduka dunia nzima kwa fikra tofauti alikuwa ni tishio kubwa kwa ubeberu.

Sasa kinachotia wasiwasi ni kauli kama ile ya kusema "Tutachanja 60%".

Ila tukirejea kwenye sababu ya pili, ni kwamba Mh. Rais ameonesha kwamba ni mpenzi wa safari za nje ya nchi. Kwa yeye kuchanja inawezekana kuwa ni lazima, maana hatujui atakwenda nchi gani safari zijazo.

Na Mh. Rais akishakuwa ni msafiri, viongozi wengine nao kama mawaziri, wakurugenzi, n.k. nao wataanza tu kusafiri.

Sasa kuyatambua mambo kama haya ndo msingi wa kujua ni tatizo gani haswa wanalojaribu kutatua kwa kupitia hizi chanjo. Sio unafuata mkumbo tu, wakati wewe maisha yako ni ya hapahapa Bongo.

Ingekuwa chanjo zimeletwa kwa ajili ya kupambana na "korona" basi zisingekuwa hiyari. Hatua zingine zinazoletwagwa kwa ajili ya kupambana na "korona" huwa si za hiyari (kama vile amri za kuvaa barakoa kwenye majengo na mabasi).

Mwisho kabisa nimalizie kwa kusema kuwa kama wewe ni Mwafrika unayeamini kwamba kichwa chako kina akili, na unaweza kufikiri, kwamba hauna haja ya kutegemea fikra za Mzungu, basi usimsahau huyu kiongozi wetu aliyetutoka. Uthubutu alioonesha na jinsi alivyokataa kabisa kushikwa akili na wazungu katika masuala fulani muhimu (madini na korona) ni jambo moja la muhimu sana katika ukombozi wa Mwafrika, ambayo bado ni safari ndefu sana. Kila kizazi kina jukumu la kusukuma gurudumu.

View attachment 1870885

Na kwa CHADEMA mliokuwa mnamlalamikia sijui mambo ya demokrasia naamini sasa hivi mmeshamuelewa kama kweli mna akili za kikubwa. Ni kwamba alikuwa anayajua matatizo yake ya moyo na kwamba alijua anakufa saa yoyote ndo maana alijitahidi sana kupeleka mambo kwa kasi atimize kabla hajafa.

Haya mambo ya kutaka kupigapiga siasa kila saa (zile Operesheni Operesheni mlizokuwa mnazipenda) hayana tija yoyote kwa mustakabali wa taifa. Naamini mnaendeshwa kwa falsafa za kiMarekani. Sasa Marekani hawajaendelea kwa sababu ya demokrasia, basi wameleta demokrasia baada ya kuendelea. Na kama mnavyoona demokrasia yao ni upuuzi mtupu, hakuna kinachofanyika kule wanazozana tu kila siku.
Upuuzi mtupu.......
 
Hoja za Rais zinatokana na matokeo ya study na majaribio ya kitaalamu yaliyofanywa kuhusu chanjo husika!!!

Sasa wewe unataka Wahuni kama akina Gwajima nao waachwe waendelee kuwajaza watu ujinga kwa kuzingatia study zipi alizofanya?!

Huyo Gwajima amefanya study yoyote kuthibitisha madai yake?

Huyo Gwajima ana utalaamu wowote wa field husika kuthibitisha madai yake?

Huyo Gwajima ana maabara wapi aliyotumia kufanya uchunguzi wa hizo chanjo?!

Btw, unadai eti huoni sababu ya Gwajima kutolewa vitisho... umemsikia Gwajima kaongea nini hasa?!
Chanjo ni hiari yako. Nenda kadungwe mkuu
 
Unasemaje tukiachana na uhuru wetu tuirudishe nchi iwe koloni la wazungu?

Maana naona akili yako imeganda kabisa.
Hahahaha hivi wewe hapo unajiona huru?

Hujioni kuwa ni koloni la mzungu tayari?

Uko mjinga sana wewe
 
Ninesoma bandiko ili nijiandae kukujibu, lakini kwa mujibu wa ulichokiandika inaonesha wazi una upeo mdogo sana wa kuchambua mambo. Kuna msemo unaosema " Asie jua maana usimwambie maana".
 
Sielewi kwa nini kitu kilicho cha hiari kinabishaniwa kiasi hiki!

Asiyetaka kuchanjwa na asichanjwe tu.

Anayetaka, achanjwe.

Very simple.
 
Anasema wanalazimisha chanjo wakati serikali haijalazimisha mtu.
Anatisha watakaomjibu na kuwaita wajinga na kwamba atawasemesha mpaka watafute taulo ya kuvaa.
Anasema chanjo haijathibitishwa kama ni salama ( hizi habari kazitoa wapi)- uongo mtupu.
Anadai watakaozaliwa baadae watageuka - uongo mtupu.
watanzania 60m kuwa majaribio, hapa anakolezea chumvi.

Gwajima anadai walichochanjwa uingereza na USA. ni tofauti na tunachochanja sisi (ametunga na hana ushahidi wowote) - uongo mtupu

Anasema wazungu wangependa tufe wote huku kashika mic aliyotengeneza mzungu - amelaza ubongo.
Anabeza hatua za kuweka record wakati magonjwa mengi tu record zinwekwa
Hela wanazotoa wazungu ni mkopo siyo bure kama anavyodai yeye- amedanganya

Cha kusikitisha hajui kwanini mtu aliyechanjwa aendelee kuchukua tahadhari.
Anadanganya waumini kuwa chanjo ina kazi nyingine. (Haya maneno kamnukuu jamaa mmoja mitandaoni) chanzo ambacho si reliable source.anadanganya tena.

Tunajua lengo lake,, ni legacy ya jiwe.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app

The first pharmaceutical used to treat malaria, quinine, was derived from the tree bark of Cinchona calisaya [5]. Quinine synthesis was first attempted in 1856 by William Henry Perkins, but synthesis was not successful until 1944.

But antimalarial drugs can cause serious side-effects. “Mefloquine may cause dizziness, balance problems, and ringing in the ears. These symptoms can occur at any time during use and can last for months to years after the drug is stopped or can be permanent,” the FDA cautions.29 Jul 2013
 
Do pharmaceutical companies bribe doctors?


In fact, drug company whistleblowers and federal prosecutors have said explicitly that in some cases the payments were actually bribes and kickbacks. And this behavior has continued despite tools like Dollars for Docs.17 Oct 2019
 
Doctors Prescribe More of a Drug If They Receive Money from a Pharma Company Tied to It. Pharmaceutical companies have paid doctors billions of dollars for consulting, promotional talks, meals and more. A new ProPublica analysis finds doctors who received payments linked to specific drugs prescribed more of those drugs ...20 Dec 2019
 
Mleta mada ninakubaliana na wewe kuwa chanjo iwe ni hiari hata hivyo wananchi wana haki ya kuelimishwa kuhusu umuhimu wa chanjo.

Ni jukumu la serikali kuleta chanjo kwani Ina dhamana ya afya na tiba ya raia. Hospitali zikifurika kwa wagonjwa serikali inatumia pesa kutoa tiba ambayo ingeweza kuzuilika na wakati huo huo inapoteza nguvu kazi.
 
How much does Big Pharma lobbying cost?

Leading lobbying industries in the U.S. 2020

In 2020, the pharmaceuticals and health products industry in the United States spent the most on lobbying efforts, totaling to about 306.23 million U.S. dollars.4 Mar 2021
 
Hzo chanjo zote zilipita hatua mbalimbali kuanzia na majaribio mbalimbali mpk kufikia matumizi ambapo si chini ya miaka 5-10

Pia Chanjo zote zinakuwa kinga ya ugonjwa hii ya covid si kinga kwa maana unaweza kupata covid ,unaweza kuambukiza covid na unatakiwa kuchukua hatua zote ambazo wasio na chango wanazifata sasa kama unakili kazi ya hii chanjo ni nini kama sina tofauti na wale ambao hawana chanjo?
Kwa kuongezea tu, JPM aliwahi kusema kama kutengeneza chanjo ni rahisi hivyo mbona mpaka leo hao wazungu hawajawahi kuleta chanjo ya UKIMWI wala TB na ni magonjwa yaliyoua watu wengi zaidi Duniani kuliko hata hiyo Corona.

Sent from my SM-A730F using JamiiForums mobile app
 
How much does Big Pharma lobbying cost?

Leading lobbying industries in the U.S. 2020

In 2020, the pharmaceuticals and health products industry in the United States spent the most on lobbying efforts, totaling to about 306.23 million U.S. dollars.4 Mar 2021
This is not uncommon

hata kura za Akina Gwajima tu they spent billions of shillings

marketing and lobbying is part of any business especially when there are competitors in the market
 
Back
Top Bottom