Chanjo na dawa zote zinazotumuka Tanzania, majaribio yake yamefanyika Tanzania?!
Unaweza kunionesha ripoti ya chanjo za surua, ndui, polio na magonjwa mengine kama hayo ikiwa ni matokeo ya majaribio ya chanjo hizo kufanyika Tanzania?
Hiyo ni hoja ya kusema kwamba kama zamani ilikuwa safi basi na leo itakuwa safi. Yaani ni hoja ya kuuza akili yako na kuweka imani 100% kwa mtu baki.
Ngoja nikufunue kichwa ili usiendelee kulala kwenye mambo ya zamani.
Chanjo ya Polio ndo inaleta Polio Afrika.
Haya sio maneno yangu bali ni maneno ya WHO wenyewe. Wameandika kwenye ukurasa wao
hapa, aya ya sabab kutoka juu kuwa:
--- nukuu ----
Today, the fight continues against all forms of poliovirus. A rare
vaccine-derived version of the poliovirus is affecting African countries with low immunization coverage, particularly among remote communities and those experiencing migration or conflict. Renewed efforts are underway to rid Africa of all remaining vaccine-derived polioviruses.
--- mwisho wa nukuu ---
Sasa unapoonza maneno kama hayo ni kwamba wamejaribu kudogosha ishu ili wale waliolala muendelee kulala.
Na pili unaijua historia haswa ya chanjo ya polio ilivyopatikana?
Unafahamu kuwa chanjo ya polio ndo ilitengeneza virusi vya HIV?
Hiyo historia ipo katika kitabu kinaitwa, "
The River : A Journey Back to the Source of HIV and AIDS" (kiko Amazon)
Kwa ufupi ni kwamba polio sio ugonjwa Afrika. Ulikuwa ni ugonjwa wa wazungu (kama ilivyo korona). Katika kutafiti chanjo wakaenda kufanya experiments kwa nyani nchini Congo (enzi hizo ikiwa chini ya Ubelgji, pamoja na Rwanda-Urundi).
Utafiti huo ukapeleka kutengenezwa kwa kirusi cha HIV. Majaribio ya chanjo ya polio waliyafanya mwaka 1957 kwa wakongomani na wanyarwanda-urundi. Na kwa kule Marekani waliwafanyia watu wasiowapenda (mashoga) na watu ambao hawana ndugu wa kuwalilia (yatima 20 kwenye kituo kimoja cha kulelea yatima jijini NYC).
Mwaka 1959 kesi ya kwanza ya HIV ikaibuka Kinshasa. Huku Tanzania kama unakumbuka ugonjwa uliingilia Kagera kwa wahaya kutokana na ukaribu wao na Rwanda-Urundi.
Dr. Remmy anatokea eneo la Mashariki ya Kongo ambako ndo maabara ilikuwepo kwenye mji wa Kisangani (enzi hizo ukiitwa Stanleyville). Aliujua UKIMWI mapema sana kutokana na ndugu zake na watu kadhaa anaowajua kufariki huko Kongo. Ndo alikuwa mwanamuziki wa kwanza kuimba kuhusu UKIMWI kwenye wimbo wake wa "Mambo kwa soksi"
Ila alikuwa mbele ya wakati, maana huku Bongo UKIMWI ulikuwa bado haujashika chati. Wimbo wake huo ulifungiwa na BASATA kwamba ni matusi. (Soksi alikuwa anamaanisha ni kondomu. Sasa enzi hizo za Nyerere bado yuko hai, kuongelea kondomu ilikuwa ni ishu nyeti sana).
Na kwa Marekani kama unaijua historia ya UKIMWI kule ulipoingia ulikuwa unaitwa ugonjwa wa mashoga.
Kwa hiyo mdau kuna mengi sana nyuma ya pazia. Haya ni machache yanayojulikana. Mengi yanafichwa.
Ukiona kichwa kama Magufuli anakupa warning ujue kuna vitu ameshaviona.
Sasa ni uzembe sana wa akili kuwaza kwamba "Kama zamani tumefanya basi tuendelee kufanya"
Nyerere angekuwa na akili hiyo unadhani angedai Uhuru? Maana kama amezaliwa ameukuta ukoloni sasa anadai uhuru wa nini?