Mkuu dhiki kuu itatokea kabla ya unyakuo, soma ufunuo sura ya 6 yote na sura ya 7. Ukisoma ufunuo 7:2-3 utaona malaika akiwazuia wale malaika waliopewa kuidhuru nchi na bahari wasiidhuru nchi, wala bahari, wala miti, hadi watakapokwisha kuwatia muhuri watumwa wa Mungu juu ya vipaji vya nyuso zao. Baada ya hilo zoezi la kutiwa muhuri ndipo unyakuo ulipofanyika ukisoma ufunuo 7:9, watu kutoka kila taifa, kabila, jamaa na lugha wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele za mwanakondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao.......
Sasa ukisoma ufunuo 6:9, katika kipindi cha dhiki kuu kabla ya unyakuo ulioelezwa kwenye ufunuo 7:9 kuna wale watakaouawa kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao. Kwa hiyo hii inadhihirisha kwamba kipindi cha dhiki kuu kitaanza kabla ya unyakuo......
Ubarikiwe na bwana, asante sana....