#COVID19 Chanjo za Kupambana na Corona (COVID-19): Nini Maoni na Mtazamo wako?
Hivi hii michuano ya uefa euro inayoendelea inafanyika wapi... Je huko hakuna Corona...??
 
Watanzania bana jitokeze basi utengeneze chanjo yako wewe ili watu wa tumie kama cha jirani mtego
 
Badala ya kuwa na taifa linalojitambua tutakuwa na taifa linalotambulika
Chanjo sawa ni jambo zuri lakini hatujui miaka 5 au 8 mbeleni nibi kitakuja kutokea
Tusiuziwe ng'ombe kwa mlio
 
Wizara ya Afya Uganda imeeleza kuwa wanaochanjwa ndio hawatoboi wakipata maambukizi.

Hii ni yakukataa kabisa
 
Beberu hajawahi kuwa na urafiki na muafrika
Tajiri hajawahi kuwa na urafiki na masikini
Mwajiri hajawahi kuwa na urafiki na mwajiriwa
Serikali haijawahi kuwa na urafiki na wananchi
Hospitali tu ndio ina urafiki na wagonjwa.
Ikiwa watoto mpaka leo wanapigwa chanjo inayo tengenezwa na mabeberu na tupo wazima mpaka leo(au sijui zile chanjo zime mega nusu ya ubogo[emoji848][emoji23][emoji23])


Lunatic [emoji2957][emoji2957][emoji2957]
 
Huu ujinga wenzetu washauona na sisi tunataka kuwafuata
IMG-20210625-WA0005.jpg
 

Attachments

  • IMG-20210625-WA0005.jpg
    IMG-20210625-WA0005.jpg
    44.9 KB · Views: 1
Hivi hii michuano ya uefa euro inayoendelea inafanyika wapi... Je huko hakuna Corona...??
Michuano ya Euro inafanyika katika miji mbalimbali barani ulaya na kutokana na covid-19 huwezi kuingia uwanjani bila chanjo wala negative test. Vivyo hivyo kwa wachezaji na wahusika wengine
 
Beberu hajawahi kuwa na urafiki na muafrika
Tajiri hajawahi kuwa na urafiki na masikini
Mwajiri hajawahi kuwa na urafiki na mwajiriwa
Serikali haijawahi kuwa na urafiki na wananchi
Hospitali tu ndio ina urafiki na wagonjwa.
Ikiwa watoto mpaka leo wanapigwa chanjo inayo tengenezwa na mabeberu na tupo wazima mpaka leo(au sijui zile chanjo zime mega nusu ya ubogo[emoji848][emoji23][emoji23])


Lunatic [emoji2957][emoji2957][emoji2957]

Nini kinafanya udhani uko sawa?

Kwanini usihusishe huu uwezo mdogo wa kuelewa/kuhoji mambo na hizo chanjo za utotoni!
 
Sawa, ila sio kwa sababu ya hicho kichapisho uchwara cha Uganda.
Yapo malalamiko kutoka nchi nyingi Kenya na UK waliwahi kulalamika kuwa chanjo zimeharibu mizunguko ya HEDHI na kupelekea UGUMBA case zipo nyingi ila wewe unajipofusha kwa kuangalia chapisho.


UKISUBIRI OFFICIAL DECREE hutaisikia popote maishani kwako maana hii ni Global movie na JIANTS kama WHO watakusakama kama walivyofanya kwa JPJM. So akili kichwani kwako
 
Huu ni uhuni unaotaka kuletwa na watu wachache wenye tamaa wa fedha tu mpk leo tunasubr kimbunga Jobo na hyo 3 wave ya corona lakini maisha ya watanzania hayawezi kuyumbishwa na hawa wahuni wanaotaka kujipatia fedha kupitia watu... baada ya kuwekeza katika kukusanya kodi wanataka kujiwekeza ktk kujipatia fedha kwa njia za kutengeneza

Najiuliza hawa wanaosema Sijui 3 wave haya wakina Mbowe wameshapiga vaccination kwa maana ya kinga lakini kutwa wanavaa barakoa utadhani madoctor wa chumba cha upasuaji sasa najiuliza kama mtu umepiga kinga dhidi ya ugonjwa fulani mfano leo watuambie hii ni kinga dhidi ya ukimwi lakini hao hao waliotuuzia kinga bado wanatusisiza matumizi ya Condom wkt wa mibunyo , mtu mwenye akili lazima ashangae huu ujinga na uhuni unaotaka kuletwa na hawa wahuni.

Serikali yote ilikuwepo ktk wave zote 2 wengine mpk wakajikuta kama madoctor manyau nyau hv leo waziri wa afya na msaidizi wake wakiangalia ule uganga waliokuwa wanaufanya leo wanaongea mengine ndo maana nasema Mwafrica ni kiumbe wa ajabu kabisa kuwahi kuwepo Duniani
 
kwanini na wewe umshinikize raisi kwamba watu wasivae barakoa??? ina maana unawaona watu ni wajinga kiasi cha kutokujua nini wanataka? UTAKUFA WEWE NA FAMILIA YAKO tutumie akili, ukiona barakoa inafaa sawa ukiona haifai sawa pia.
 
Corona ipo na wananchi tunatakiwa kuchukua tahadhari zote ndugu, nakushauri uvue hilo blanketi la ujinga ulilojifunika ili upate ufahamu japo kdg.
 
Akili za kimasikini siku zote hazipendi kusikia kuna gharama za ziada za kufidia, ama kulipa ili kukabiliana na janga ama tatizo lolole lile. Siku zote akili kama hizi hupenda sana kusaidiwa, kupata vitu kwa njia za mkato ama kupewa vitu vya bure,

Gonjwa aina ya UVIKO 19 lenye sura ya "biological weapon" pamoja kuripotiwa kila siku kuwa linaisumbua dunia yote hivi sasa bado kweli kuna watu hawaamini kuwa lipo! Je! Tahadhari zote hizi zinazotolewa na wataalamu wa afya kuna watu wanathubutu kuzibeza?

Kwani kuna yeyote yule kati ya Magufuli ama Mama Samia ambaye amewahi kukanusha kuhusu uwepo wa visa vpya, maambukizi mapya ya virusi na hata vifo vitokanavyo na UVIKO 19? Je! Ama kuna yeyote kati yao kama Rais wa nchi yetu ambaye amewahi kuthubu kuwasihi wananchi kuacha kuchukua hatua stahiki katika kutaka kukabiliana na janga la gonjwa hili tishio kwa maisha ya mwanadamu?

Maandiko matakatifu yanatuambia, "Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa". Naam! Tuache siasa, tuache ushabiki, tuache mzaha juu ya wimbi hili jipya. Ni lazima tuchukue tahadhari, kama wewe binafsi huoni ulazima wa kuvaa barakoa ama kuchukua hatua nyingine zinazo shauriwa basi huo ubaki kuwa ni msimamo wako binafsi wala usishawishi watu wengine kufanya hivyo.

Lakini la mwisho ijapokuwa si kwa umuhimu, ni suala la chanjo, bado nakubaliana na wote wale wenye kushauri kuwa liwe jambo la hiari kwa mtu mwenye kutaka kuchanjwa. Wale wenye kusitasita bado wanahitaji kujiridhisha zaidi juu ya usalama wa chanjo hizi mara zitakapoanza kutumika rasmi hapa nchini.
 
Back
Top Bottom